Watalaamu wa Afya hivi inakuaje mtu anapofanyiwa upasuaji asizinduke anapitiliza kufa?

Mkuu, mgonjwa akienda kupasuliwa,we muage kabisa manake anaenda kuzimu akirudi mshukuru MUNGU. nawahakikishia kuwa kupasuliwa manake njia zote za kitabibu zimeshndkana,na last chance ya mgonjwa kuendelea kuishi ni upasuaji tu. kama mungu alipanga kuwa siku za mgonjwa ziliandikwa zitaisha kwa namna ile atakufa tu bhandugu. ukisema tumekosa wataalamu tutakuwa tunakosea,wataalamu hawahawa tulionao wanapongezwa na wengi kwa kazi nzuri wanayoifanya, mimi mama yangu amepasuliwa mala tatu nawashukuru sana bado nitamba nae,pia mama yangu mkubwa wa kumfuata aliyepasuliwa mala3 pia nae alipasuliwa aliposhndwa kujifungua mpaka leo yupo. warest in peace waliotangulia kwa style hiyo ni mipango ya MUNGU.
 
Ni bora ungeitaja tu mi naitaja mloganzila pale somshauri mtu aende pale ni.lango.la kifo yani kufa pale sekunde na hakuna anaejali kuna mgonjwa alikuwa pale walimtoa damu mpaka akaishiwa damu akafa yani katolewa mara ya kwanza hakaja majibu hawaonimkitu wakatoa tena wakatoa tena mara tatu mgonjwa akafa ni uzembe wa kupitiliza mi.mloganzila hunipeleki heri nifie nyumbani ukienda pale kuna vilio si vya kawaida kuna ndugu yangu pona yake alikimbia na dripu akaenda private wamtoe akawauliza dripu la ugonjwa gani hili cha ajabu alikuwa na homa lakini nurse alishangaa dripu halihusani na homa kabisaa akamwambia yani ungekufa soon.
 
Vifo vya hivyo vinatokea kwa kutokuwa waangalifu na kufuata procedures
Kuna watu wana pressure na inapanda ila Dr hana habari bali anaendelea na upasuaji mtu akiwa kwenye nusu kaputi
Hapo hata kama mtu hajui kama ana High blood pressure wanauwa tu
Wengi wanaondoka hivi na nimeshuhudia mzee mmoja alifanyiwa upasuaji na pressure yake
Nafikiri walikuwa wanafanya ops akiwa kafa masikini
Inasikitisha sana na sijui kama ukishtaki utapata haki yako
 
Mbona wanasema kujifungua kwa op ni salama zaidi kwa mtoto pia
Halaf hiyo hospital ungeitaja labda kuna uzembe wanafanya

Jibu si la moja kwa moja.
Haya yote hutegemea na:

1: Kuwa mjamzito tu tayari ni risk/hatari.

2: Njia ya kujifungua pia hutegemea hali ya mjamzito.

3: Mazingira aliyopo na mapito ya mjamzito husika.

4: Upatikanaji wa wataalamu husika/wenye ujuzi, upatikanji wa vifaa husika ili kufanikisha kujifungua kwa njia husika
 
Kwenye OP kuna mambo mengi , ndo maana kabla ya op kuna basic investigation kufanyika , kutokana na aina ya op,

Pili inweza pia tatizo lipo kwawatoa usinginzi pia . Leo GA haina sababu sana kama hakuna huitaji wake , badala yake spinal ndo inatumika sana hasa kwa wajawazito na baadhi ya op zingine , Zoom ya wizara inatakiwa kuimulika iyo Hospital
 
Mgonjwa anaweza kupoteza sababu ya complications za surgery.
Hasahasa upande wa Anaesthesia.
Dawa zile za usingizi zina negative effects pia kwa mgonjwa,
mfano nyingine zinapandisha BP l, nyingine zinashusha.
NA effects nyingine nyingi.
Sasa mtalamu asipokuwa makini kudetect na na kucollect hizi inshu mapema ni rahisi kumpoteza mgonjwa.
Lakini pia wagonjwa wengine wana matatizo yao ya kiafya yanagondulika wakti wa surgry hasa kwenye moyo.
 

Hapa ni mpaka ukafanye ufatiliaji wa nini kilitokea kwenye mazingira husika/Root cause analysis(RCA).
Mfano:
1: Vifo viliyokea kwenye mazingira yapi wakati wa upasuaji.

2: Hali ya wagonjwa kabla ya upasuaji.

3: Maandalizi ya wagonjwa kabla ya upasuaji.

4: Uwepo wa viafaa wezeshi.

5: Uwepo wa wataalamu husika.

6: Usimimiaji wa miongozo husika/utimizaji wake

Nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…