Watalaamu wa Afya hivi inakuaje mtu anapofanyiwa upasuaji asizinduke anapitiliza kufa?

Watalaamu wa Afya hivi inakuaje mtu anapofanyiwa upasuaji asizinduke anapitiliza kufa?

Hapa ni mpaka ukafanye ufatiliaji wa nini kilitokea kwenye mazingira husika/Root cause analysis(RCA).
Mfano:
1: Vifo viliyokea kwenye mazingira yapi wakati wa upasuaji.

2: Hali ya wagonjwa kabla ya upasuaji.

3: Maandalizi ya wagonjwa kabla ya upasuaji.

4: Uwepo wa viafaa wezeshi.

5: Uwepo wa wataalamu husika.

6: Usimimiaji wa miongozo husika/utimizaji wake

Nk.
Maswali haya yamekaa kitaalamu zaidi na mimi sitaweza. Swala la kujua hali ya wagonjwa kabla ya upasuaji ni ngumu kwanza sitaruhusiwa hata kuangalia vifaa pia sitaruhusiwa mi raia tu wa kawaida
 
Ni bora ungeitaja tu mi naitaja mloganzila pale somshauri mtu aende pale ni.lango.la kifo yani kufa pale sekunde na hakuna anaejali kuna mgonjwa alikuwa pale walimtoa damu mpaka akaishiwa damu akafa yani katolewa mara ya kwanza hakaja majibu hawaonimkitu wakatoa tena wakatoa tena mara tatu mgonjwa akafa ni uzembe wa kupitiliza mi.mloganzila hunipeleki heri nifie nyumbani ukienda pale kuna vilio si vya kawaida kuna ndugu yangu pona yake alikimbia na dripu akaenda private wamtoe akawauliza dripu la ugonjwa gani hili cha ajabu alikuwa na homa lakini nurse alishangaa dripu halihusani na homa kabisaa akamwambia yani ungekufa soon.

Pale hata ukijifanya una kikohozi kikali ukatest mitambo aisee utaibuliwa ugonjwa wa ajabu hadi ulazwe na ukilazwa hutoboi!

Wanafunzi wamejazwa pale ndo wanaoharibu title ya mloganzila ionekane Israel.
 
Sema kifo cha usingizini ni kizuri kweli, yani unachomwa sindano ya ganzi ukishalala inakua ni moja kwa moja wewe unastarehe usingizini tu 😊
Eti Demi si unajua raha ya usingzi?
 
Takwimu nyingi haziko sawa.

Mfano, Mtoa maada kaleta watu walio kufa peke ake kua anawajua 4, Lakini walio toka wazima hawapo.

Pia ukisema sikuiz, Nazani hata rate ya kufanya upasuaji imeongezeka kuliko hapo nyuma hivo kuongeza no. ya wanao kufa na kuishi.

Mwisho, Ni kweli bado sector ya Afya, Kuna kigugumizi kwenye General Anestezia(Nusu kaputi), Mwaka 2013 tulimpoteza mwalimu wetu alienda kufanya upasuaji wa Tumbo kutoa minyama nyama

Aliingia mzima, Akatoka Maiti.

Niwakati sasa wizara kuwekeza nguvu kwenye hiki kitengo.
 
Back
Top Bottom