Watanganyika msinug'unike, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utavunjika wenyewe automatically

Kwa vile rais ajaye sio Mtanganyika, ni Mtanzania, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, hivyo hakuna Mtanganyika, tuna Mtanzania tuu, ila ndani ya Mtanzania, tuna Mzanzibar mkaazi, ila Wazanzibari wote wana haki zote za Mtanzania, huo Uzanzibari ni ziada. Huyo rais ajaye!, atawanyorosha!, na ikitokea akaingia kabla ya katiba mpya, atawashikisha adabu Wazanzibari. Trends Reading: Japo Rais wa 2030 Namjua, Simtaji ili Kumlinda!. Be The First to Know Good News Kawe-2030, MB.ni Mwanamke!, Kawe Itapaa kwa Maendeleo!

P
 
ni mtanzania anayetokea tanganyika
 
Kusubiri embe kwenye mchongoma ndio hivi sasa
 
Kwa nini jina la Tanganyika likitajwa watu wanasisimka sana na kuliogopa kabisa kulitaja wakati Zanzibar inatajwa kwa madaha na mbwembwe zote ila hali inaitwa Tanzania visiwani
 
Uliwahi kuandika humu kwamba Tundu Lissu hatorejea Tanzania, Je hakurejea?
Mimi ni mwalimu wa kujitolea humu, soma vizuri thread Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Je unajua ni mimi ndiye nilimshauri kugombea?, GE2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Je wajua aligoma kurejea nchini, ni mimi tena nilimshauri na akarejea Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Na aliporejea nilimkaribisha
P
 
Muungano hakuna sheikh! Huu muungano wa kulazimishana kula kambale?
Sisi Wazanzibar na kambale wapi na wapi? Samaki wetu ni wa bahari... Ushaona bana! Jodari, kolekole, ngisi, kibua... heee!
 
Mama kawashika watanganyika pabaya.

Sasa hivi ni vilio kwa kila mtanganyika kuanzia kule Nanjilinji hadi kule Katoro. Mmeisha.

Na mimi namuambia mama hiviii: abane hapo hapo. Ukiona vipi hamia Bujumbura.
 
Huu muungano ni kama kijana wa kiume aliyejipata kiuchumi anaenda kuoa single mama mwenye watoto watano hao watoto kila mmoja na baba ake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…