Watanganyika msinug'unike, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utavunjika wenyewe automatically

Muungano unakufa wenyewe. Dalili zipo wazi.
 
Kawe 2030 mbunge wetu ni Halima Mdee. Vinginevyo tutagawana mbao.
 
Umechelewa.
 
Ukisikia uzalendo ndio huu, twende kwenye serikali moja!.
p
Suala ni kwamba wao Zanzibar hawataki hiyo serikali moja kwasababu itawafanya kuwa kama mkoa ndani ya Tanzania, uliza vizuri hata wananchi wao wanakazia sana kuwa Zanzibar ni nchi na ni nadra sana wak kujitambulisha kama waTz hasa wakiwa nje ya nchi wakiulizwa utaifa wao wanajibu Zanzibar, hata wangepewa nafasi passport zao ziandikwe uraia wanaoutaka wangefuta ile Tanzanian na kujiandikia Zanzibarian. Tulipofika ni pabaya sana na tumeshachelewa kuwaza serikali moja.
 
Ulinzi wa press card inaendelea
Ni kweli kabisa, kama unaitegemea press yako kuendesha maisha yako, utailinda kwa gharama yoyote kwa jinsi ile ile Tanzania ni nchi moja ya JMT, hivyo huu muungano wetu adhimu na adimu, tutaulinda kwa gharama yoyote na hata Ikibidi kugharamiwa kwa gharama ya machozi, jasho na damu, tutailipia tuu!.

Hawa Wazanzibar wanaoleta chokochoko kuuchokoa muungano, nawashauri hizo chokochoko zao, wamchokoe pweza, muungano hawatauweza!.
P
 
Baba Tanganyika alimpenda sana binti mrembo Zanzi akamuoa na kufuta utaifa wake na kugeuka Tanzania, bila muungano hakuna Tanzania na Tanganyika alikufa na tukazika kitambo.

P
Bado sijapata faida kwa mimi, nipe faida mkuu mana mimi sikuepo
 
wazanzibari sio Watanganyika
 
wazanzibari sio Watanganyika
Yes Wazanzibari sio Watanganyika, baada ta Tanganyika na Zanzibar kuungana, ilizaliwa nchi moja mpya ya Tanganyika, Uzanzibari na Utanganyika ulikufa, ukazaliwa Utanzania, hivyo Wazanzibari ni Watanzania, na waliokuwa Watanganyika ni Watanzania, nchi inaitwa Tanganyika ilikufa, ikageuka Tanzania, na nchi iliyoitwa Zanzibar, nayo ilikufa, ila likabaki eneo la iliyokuwa nchi ya Zanzibar, ambalo bado linaitwa Zanzibar ila sii nchi, ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani.

Kitendo cha mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, kuifufua nchi ya Zanzibar ni uhaini Tanzania Nchi 1 ya JMT, Zanzibar Kujiita Nchi, Sio Uhaini?. Zanzibar Iadabishwe Kuondoa Ubatili wa Katiba Yake ili Tuitambue au Tumchelee Mwana Kulia?

P
 
Mpaka sasa hakuna nchi moja. Usitudanganye. Wadanganye wajinga wenzako. Kwa nini rais wa Zanzibar anapigiwa mizinga 21 wakati wa sherehe za mapinnsuzi ya Zanzibar?
 
Tunajua, dunia yote ni shahidi: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni mradi wa CCM(ASP,TANU), ulioimbwa kwa sauti yake na kuchezeshwa kwa ngoma yake. Lakini upepo wa nyakati hubadilika, na hakuna kinachodumu milele. Siku upinzani utakapovaa joho la mamlaka, Muungano huo utasimama mbele ya mahakama ya historia, ambako uimara wake utapimwa na hatima yake kuandikwa.
 
Mpaka sasa hakuna nchi moja. Usitudanganye. Wadanganye wajinga wenzako. Kwa nini rais wa Zanzibar anapigiwa mizinga 21 wakati wa sherehe za mapinnsuzi ya Zanzibar?
Mkuu Idu, Idugunde , kiukweli hii ni jeuri tuu, ila maadam ina mamlaka yake ya ndani, ilitakiwa apigiwe mizinga 19 na sio 21!, nchi moja yenye rais mmoja, ambaye ni amiri jeshi ni mmoja tuu wa kupigiwa mizinga 21, huyu rais wa Zanzibar amejiita amiri jeshi mkuu wa wale migambo wa KMKM, JKU na Vikosi maalum, ila hayo ni mambo yake ndani sisi hayatuhusu.

P
 
Kwani wadanganyika wanataka kuvunja muungano au marekebisho ya ukweli?!
UK haikuwa kama Sasa, twataka bunge letu kama lao, twataka haki kwa wote, twataka rais wa wadanganyika toka bara, twataka wabunge wa bara wadanganyika, twataka bara iongozwe na wadanganyika, period...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…