Watanganyika msinug'unike, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utavunjika wenyewe automatically

Hiyo ni ngumu kumesa rafiki , 😳 !
 
Hakuna Muungano hapo. Kama amiri jeshi wa JMT ni mmoja hatakiwi kiongozi mwingine kupigiwa mzinga hata mmoja.
 
NYUFA YA KWANZA 1995
1. MUUNGANO.

"Ninalolisema kwa wazanzibar nalisema kwa watanganyika Zanzibar wakitaka kujitenga tu kwa Ulevi tu na Ujinga hasa ujinga wa viongozi wao watanganyika watabaji wameduwaa Lo!!!! Wenzetu hawa wanafanyaje wanakwenda zao, watanganyika walioachwa WAMEDUWAA WATABAKI WAMOJA.".

MWALIMU JK NYERERE
 
Sio jeuri. Hakuna Muungano ni utapeli wa Nyerere na Karume
 
Kwa hiyo kabaki mama tuu!
No sio kabaki mama tuu, bali huyu mwanaume kijana rijali, kidume cha mbegu, Tanganyi ni Mkristu, baada ya kampenda huyu mwanamke binti mrembo wa Kiislamu Zanzi, akamchumbia, kwa kawaida ndoa za Kikristo hufungiwa nyumbani kwa mwanaume, ili ukipenda mwanamke wa Kiislamu wa siasa kali, lazima mwanaume ubadili dini usilimu kuwa Muislamu na ndoa za Kiislamu hufanyikia nyumbani kwa mwanamke, kwa walii au msikitini, ndoa ya Tanganyi na Zanzi ilifungiwa kwa mwanamke, tarehe 22 April, 1964 na picha za ndoa zipo!. Walii wa Zanzi alikuwa Sheikh Abedi Karu, Kiislamu mwanamke hata akiolewa, huendelea kutumia jina lake la ubini la kwao Binti Zanzi, kwa ndoa za Kikristu, mwanamke hutumia jina la mume, hivyo jina la Zanzi lilipaswa kuwa Zanzi Tanganyi, lakini jina la ndoa liitwa Jamuhuri ya Muungano. ya Tanganyi na Zanzi.

Mwanaume Tanganyi kafa kaoza, kwa binti Zanzi, akaamua kubadili jina, badala ya kuendelea kuitwa Tanganyi, kwa vile sasa ana mwenza, jina likabadilishwa kuwa TanZani, jina lake la Tanganyi akalifuta, ila kwa upande wa mkewe, jina lake la Zanzi linaendelea.

Kama nilivyoeleza mwanzo, ndoa ya mwanzo ni ndoa ya Kiislamu, ilifungiwa Zanzibar tarehe 22 April, 1964, na walii Karu, mzazi wa mwanaume ni yule Mwalimu Julikamba Nyere ambaye ni Mkristo Mkatoliki. Ndoa za Kiislamu zina talaka, toka talaka moja ambayo ni talaka rejea, talaka mbili hadi talaka tatu, ndoa Kikristu Kikatoliki hazina talaka ni ndoa za milele na hutenganishwa na kifo tuu!. Walii wa Binti Zanzi wakati akiwafungisha ndoa na Tanganyi, alisema ndoa hiyo ni kama koti tuu, likikubana, unalivua!.

Baada ya hiyo ndoa ya Tanganyi na Zanzi kufungwa Kiislamu kule Zanzibar ile tarehe 22 Aprili, ndoa hiyo ilifungwa tena Kikristo Kikatoliki, April 26, mwaka 1964, ndoa hii ya pili haina talaka!. Zile hati za ndoa hii zilizosainiwa April 25 na Bunge la Tanganyika, hazina kipengele cha talaka!, ni ndoa ya milele!.

Kama Tanganyi kakubali kufuta jina lake kwa ajili ya Zanzi, kama kuna mnaofikiri kuna siku binti Zanzi, atapewa talaka, mtasubiri sana!. Hii ndoa iliyopo sasa ya Tanzani, (Tanganyi na Zanzi), ni ndoa ya milele, haina Talaka kamwe!.

Japo kwa sasa, ndugu wa Binti Zanzi wanaleta chokochoko ya kuichokoa hii ndoa, Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Niliwahi washauri humu Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
P.
 
Hakuna Muungano hapo. Kama amiri jeshi wa JMT ni mmoja hatakiwi kiongozi mwingine kupigiwa mzinga hata mmoja.
Mkuu wa nchi ndiye hupigiwa mizinga 21, VP na Rais wa Zanzibar mizinga 19, Waziri Mkuu mizinga 17,
P
 

Mkuu wa nchi ndiye hupigiwa mizinga 21, VP na Rais wa Zanzibar mizinga 19, Waziri Mkuu mizinga 17,
P
Haipo kisheria.
 
Mkuu wa nchi ndiye hupigiwa mizinga 21, VP na Rais wa Zanzibar mizinga 19, Waziri Mkuu mizinga 17,
P
Kwanza kitendo cha rais wa Smz kuwa wa mwisho kuondoka kwenye sherehe za mapinduzi ya Zanibara ni dharau kwa rais wa JMT.
 
Muungano hauwezi kufa auto matic, lazima panahitajika pressure nzito
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…