mwehu ndama
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 2,472
- 9,542
Kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwamba Watanzania tunapaswa kupambana kupata Katiba Mpya ni kauli kubwa na yenye uzito mkubwa kisiasa.
Soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya
Kwa muda mrefu, madai ya Katiba Mpya yamekuwa yakisukumwa zaidi na vyama vya upinzani, wanaharakati, wanasheria na wananchi tunaoamini kuwa mfumo wa sasa haujatoa ulinzi wa kutosha kwa haki za raia, uwajibikaji wa viongozi na mgawanyo wa madaraka.
Kwa hiyo, kiongozi mkubwa wa CCM anapotumia lugha hiyo, tunapaswa kujiuliza: Je, huu ni mwanzo wa mageuzi ya kweli, au ni mkakati wa kisiasa wa yeye binafsi na chama chake kujijenga kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030 na mateso ya milele kwa watanganyika?.
Binafsi mimi mwehu ndama nimefanya tafakuri ya kina na kugundua hii pia inaweza kua ni geresha ama changa la macho lingine, hapa ccm wanajibadirisha kama kinyonga kwa lengo la kutuumiza zaidi na sababu zangu ni kama ifuatavyo
Kwa kuzungumzia Katiba Mpya, haki za binadamu na mwafaka wa kitaifa, anaanza kutumia lugha ambayo kwa kawaida imekuwa ikihusishwa na wapinzani.
Mkakati huu unaweza kumjenga kama mtu anayekubalika si tu ndani ya CCM, bali pia kwa wananchi wasio wanachama wa chama hicho.
Hii huitwa political repositioning: mwanasiasa anabadilisha au kupanua taswira yake ili kuonekana anafaa kwa mazingira ya kisiasa yanayokuja. Tupo macho maamae
Hii inaweza kuwa njia ya kupunguza nguvu ya vyama vya upinzani.
Hapa nikama wanatuambia kiaina tena kwa njia njia isiyo ya moja kwa moja kwamba:
“Hatuhitaji kuiondoa CCM ili kupata Katiba Mpya, kwa sababu hata viongozi wa CCM wanaitaka.”
Katika siasa, mbinu hii huitwa co-optation. Chama tawala kinachukua hoja za wakosoaji wake na kuanza kuzizungumza, ili kupunguza ushawishi wa wale waliokuwa wameziasisi. Nasisitiza watanganyika sio wajinga tuko macho maamae
Hapa wafuasi wa chama cha mauaji (ccm) wanaweza kutaka kuona:
Je, wananchi watampokea Nchimbi vizuri akizungumza lugha ya Katiba Mpya?
Je, wanaharakati na wapinzani watamwamini?
Je, wanachama wa CCM watakubali msimamo huo?
Je, taswira hiyo inaweza kumjenga kama mgombea anayekubalika mwaka 2030?
Akikubalika, kauli kama hizi zinaweza kuendelea kuongezeka. Asipopokelewa vizuri, anaweza kusema alikuwa anasisitiza tu wajibu wa wananchi na siyo kutoa msimamo binafsi wa kisiasa. TUKO MACHO MAAMAE
Watanganyika tunasema katiba mpya haitopatikana kupitia hotuba za kindezi na mchongo kama hii ya Nchimbi leo, kauli kama hii itaaminika iwapo Serikali ya CCM itaweka ratiba rasmi ya mchakato wa Katiba Mpya, itaendelea kutumia maoni yaliyokusanywa katika mchakato uliopita, itahakikisha wananchi wanashiriki kwa uhuru, itatoa nafasi sawa kwa vyama vya upinzani, wanaharakati na wadau wengine, itarekebisha sheria zinazobana uhuru wa kisiasa na haki za raia, na Nchimbi ataendelea kusimamia msimamo huo hata pale utakapogusa maslahi ya CCM.
Soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya
Kwa muda mrefu, madai ya Katiba Mpya yamekuwa yakisukumwa zaidi na vyama vya upinzani, wanaharakati, wanasheria na wananchi tunaoamini kuwa mfumo wa sasa haujatoa ulinzi wa kutosha kwa haki za raia, uwajibikaji wa viongozi na mgawanyo wa madaraka.
Kwa hiyo, kiongozi mkubwa wa CCM anapotumia lugha hiyo, tunapaswa kujiuliza: Je, huu ni mwanzo wa mageuzi ya kweli, au ni mkakati wa kisiasa wa yeye binafsi na chama chake kujijenga kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030 na mateso ya milele kwa watanganyika?.
Binafsi mimi mwehu ndama nimefanya tafakuri ya kina na kugundua hii pia inaweza kua ni geresha ama changa la macho lingine, hapa ccm wanajibadirisha kama kinyonga kwa lengo la kutuumiza zaidi na sababu zangu ni kama ifuatavyo
1. Political repositioning — kujibadilisha nafasi kisiasa
Inawezekana Nchimbi anajitengenezea taswira ya kuwa mwanasiasa wa maridhiano na mageuzi kutoka ndani ya CCM.Kwa kuzungumzia Katiba Mpya, haki za binadamu na mwafaka wa kitaifa, anaanza kutumia lugha ambayo kwa kawaida imekuwa ikihusishwa na wapinzani.
Mkakati huu unaweza kumjenga kama mtu anayekubalika si tu ndani ya CCM, bali pia kwa wananchi wasio wanachama wa chama hicho.
Hii huitwa political repositioning: mwanasiasa anabadilisha au kupanua taswira yake ili kuonekana anafaa kwa mazingira ya kisiasa yanayokuja. Tupo macho maamae
2. CCM kuchukua hoja za upinzani
CCM ina uzoefu mkubwa wa kuchukua hoja zinazopendwa na wananchi na kuzifanya kuwa sehemu ya lugha yake ya kisiasa.Hii inaweza kuwa njia ya kupunguza nguvu ya vyama vya upinzani.
Hapa nikama wanatuambia kiaina tena kwa njia njia isiyo ya moja kwa moja kwamba:
“Hatuhitaji kuiondoa CCM ili kupata Katiba Mpya, kwa sababu hata viongozi wa CCM wanaitaka.”
Katika siasa, mbinu hii huitwa co-optation. Chama tawala kinachukua hoja za wakosoaji wake na kuanza kuzizungumza, ili kupunguza ushawishi wa wale waliokuwa wameziasisi. Nasisitiza watanganyika sio wajinga tuko macho maamae
3. Kupima upepo wa kisiasa
Kauli hii ya bwanyenye Nchimbi inaweza pia kuwa trial balloon, yaani njia ya kupima mwitikio wa wananchi.Hapa wafuasi wa chama cha mauaji (ccm) wanaweza kutaka kuona: