Watanganyika tuwe Makini: Kauli ya Nchimbi inayotututaka Wananchi kupigania katiba mpya inafikirisha sana

Kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwamba Watanzania tunapaswa kupambana kupata Katiba Mpya ni kauli kubwa na yenye uzito mkubwa kisiasa.

Soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Kwa muda mrefu, madai ya Katiba Mpya yamekuwa yakisukumwa zaidi na vyama vya upinzani, wanaharakati, wanasheria na wananchi tunaoamini kuwa mfumo wa sasa haujatoa ulinzi wa kutosha kwa haki za raia, uwajibikaji wa viongozi na mgawanyo wa madaraka.

Kwa hiyo, kiongozi mkubwa wa CCM anapotumia lugha hiyo, tunapaswa kujiuliza: Je, huu ni mwanzo wa mageuzi ya kweli, au ni mkakati wa kisiasa wa yeye binafsi na chama chake kujijenga kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030 na mateso ya milele kwa watanganyika?.

Binafsi mimi mwehu ndama nimefanya tafakuri ya kina na kugundua hii pia inaweza kua ni geresha ama changa la macho lingine, hapa ccm wanajibadirisha kama kinyonga kwa lengo la kutuumiza zaidi na sababu zangu ni kama ifuatavyo

1. Political repositioning — kujibadilisha nafasi kisiasa​

Inawezekana Nchimbi anajitengenezea taswira ya kuwa mwanasiasa wa maridhiano na mageuzi kutoka ndani ya CCM.

Kwa kuzungumzia Katiba Mpya, haki za binadamu na mwafaka wa kitaifa, anaanza kutumia lugha ambayo kwa kawaida imekuwa ikihusishwa na wapinzani.

Mkakati huu unaweza kumjenga kama mtu anayekubalika si tu ndani ya CCM, bali pia kwa wananchi wasio wanachama wa chama hicho.

Hii huitwa political repositioning: mwanasiasa anabadilisha au kupanua taswira yake ili kuonekana anafaa kwa mazingira ya kisiasa yanayokuja. Tupo macho maamae

2. CCM kuchukua hoja za upinzani​

CCM ina uzoefu mkubwa wa kuchukua hoja zinazopendwa na wananchi na kuzifanya kuwa sehemu ya lugha yake ya kisiasa.
Hii inaweza kuwa njia ya kupunguza nguvu ya vyama vya upinzani.

Hapa nikama wanatuambia kiaina tena kwa njia njia isiyo ya moja kwa moja kwamba:
“Hatuhitaji kuiondoa CCM ili kupata Katiba Mpya, kwa sababu hata viongozi wa CCM wanaitaka.”

Katika siasa, mbinu hii huitwa co-optation. Chama tawala kinachukua hoja za wakosoaji wake na kuanza kuzizungumza, ili kupunguza ushawishi wa wale waliokuwa wameziasisi. Nasisitiza watanganyika sio wajinga tuko macho maamae

3. Kupima upepo wa kisiasa​

Kauli hii ya bwanyenye Nchimbi inaweza pia kuwa trial balloon, yaani njia ya kupima mwitikio wa wananchi.

Hapa wafuasi wa chama cha mauaji (ccm) wanaweza kutaka kuona:

Je, wananchi watampokea Nchimbi vizuri akizungumza lugha ya Katiba Mpya?

Je, wanaharakati na wapinzani watamwamini?

Je, wanachama wa CCM watakubali msimamo huo?

Je, taswira hiyo inaweza kumjenga kama mgombea anayekubalika mwaka 2030?

Akikubalika, kauli kama hizi zinaweza kuendelea kuongezeka. Asipopokelewa vizuri, anaweza kusema alikuwa anasisitiza tu wajibu wa wananchi na siyo kutoa msimamo binafsi wa kisiasa. TUKO MACHO MAAMAE

Watanganyika tunasema katiba mpya haitopatikana kupitia hotuba za kindezi na mchongo kama hii ya Nchimbi leo, kauli kama hii itaaminika iwapo Serikali ya CCM itaweka ratiba rasmi ya mchakato wa Katiba Mpya, itaendelea kutumia maoni yaliyokusanywa katika mchakato uliopita, itahakikisha wananchi wanashiriki kwa uhuru, itatoa nafasi sawa kwa vyama vya upinzani, wanaharakati na wadau wengine, itarekebisha sheria zinazobana uhuru wa kisiasa na haki za raia, na Nchimbi ataendelea kusimamia msimamo huo hata pale utakapogusa maslahi ya CCM.
Tushastuka
 
www.katibampya.com

Mimi nimekataa kulaghaiwa!
 
Hawawezi kutoka kirahisi hivi hizo janja janja tu ukiona wameanza kusukuma agenda kama za wapinzani hapo jua Kuna upepo wanaupoza kusahaulisha yaliyotokea alafu baadae game linaendelea vilevile,nyoka ni nyoka tu hata avue gamba nashauri asiaminike hata kidogo huu ni mtego
Kwa kweli,hata kama ni non venomous!
 
Ukiachilia mbali yote hayo, mama mwenye nyumba lisema atajitahidi atupatie katiba mpya kabla hajaondoka madarakani mwaka 2030, nadhani Nchimbi alikuwa anakazia tu pointi ya bosi wake. Na hii ishu ya katiba mpya imewekwa kabisa katika ilani ya chama chao, kwa hio sio jambo la ajabu kuisemea katiba mpya!
Mkuu unaamini soga za hawa watu?
 
Mbona hamnajema nyie. Lengo lenu ni nini hasa? Vurugu nchini au mnataka nini. Ujue hata sisi ambao hatuna upande hatuwaelewi.

Mnaungwa mkono mnabeza. Mkikaziwa mnalia. Mnataka mfanyiwe nini? Au mnataka kitokee kipi?
Mbona wewe una upande? Halafu wewe ni binadamu wa kawaida huwezi kupangia watu kesho yao
 
Iwe ni mkakati wa ccm au hila zao, ki kivyovyote wanaharakati wamepata pa kushikia. Ni kupiga kwenye mshono. Wanapita humo humo kupiga spana. Hutuba ya nchimbi ni upenyo mzuri
 
Mbona wewe una upande? Halafu wewe ni binadamu wa kawaida huwezi kupangia watu kesho yao
Sishabikii siasa kitoto hivyo mpaka nichague upande. Ila nafurahishwa na kuona taifa langu linasonga mbele kwa amani na upendo.

Sisemi wanaopigania haki hawafai, ila hawaeleweki wanataka nini. Adui yao ameanza kushusha silaha chini wao bado hawataki.

Unataka nisiulize mnataka nini? Machafuko, watu wadhalilishwe, kinuke, muonyeshe jeuri, hali iendelee kama ilivyo ili muendelee kulalamika? Nini mnataka.

Sisi watazamaji tunataka amani, umoja, ushirikiano ili tuweze kufaidi huduma bora
 
KAURI HII YA NCHIMBI ITATUFANYA TUFANIKISHE JAMBO LETU LA KUICHUKUA NCHI KUTOKA KWA WAHUNI WALIOMUUA POLEPOLE SIKU YA TAREHE 8 MWEZI WA 8 MWAKA 2026 AMBAPO TUTAFANYA MAANDAMANO MAKUBWA MARA 100 YA ILIVYOKUWA MO29.WATANGANYIKA TUJITOKEZE KWA WINGI SIKU HIYO YA KUKINUKISHA MARA YA PILI.
Nakuunga mkono..na kubwa kuliko tutafanya siku ya usinduz wa Afrcon..bora lihamishiwe nchi nyingine..wauwaji na watekaji wasipate platform
 
Ukiachilia mbali yote hayo, mama mwenye nyumba lisema atajitahidi atupatie katiba mpya kabla hajaondoka madarakani mwaka 2030, nadhani Nchimbi alikuwa anakazia tu pointi ya bosi wake. Na hii ishu ya katiba mpya imewekwa kabisa katika ilani ya chama chao, kwa hio sio jambo la ajabu kuisemea katiba mpya!
Kwa bungs lipi la kuipitisha hyo katiba?
 
Nakuunga mkono..na kubwa kuliko tutafanya siku ya usinduz wa Afrcon..bora lihamishiwe nchi nyingine..wauwaji na watekaji

Nakuunga mkono..na kubwa kuliko tutafanya siku ya usinduz wa Afrcon..bora lihamishiwe nchi nyingine..wauwaji na watekaji wasipate platform
Naunga mkono hoja.siku ya uzinduzi wa afcon lazima nchi tuichukue kwa nguvu ya miamoja ya nguvu ya siku ya MO29
 
Kwa dalili nazoziona, tutapata katiba mpya kabla ya mwaka 2030 kwa sababu CCM wameishasoma alama za nyakati, wanapunguza kutumia nguvu.

Swali: Je, tutapata katiba mpya ya maoni ya wananchi?

Kutokana na nyakati za sasa, inakuwa ngumu kuendelea kuwadanganya wananchi hasa Gen Z na Millenials.
Vitendo haviongei hivyo. Kuna vizee vipo pale CCM havitaki kusikia katiba mpya, ndio vile vilikataa katiba ya Wariona vikaleta katiba pendekezwa. Vimerithisha upumbavu huo kwa akina Kawaida, Sufiani, Hapi nk
 
Back
Top Bottom