Watanganyika tuwe Makini: Kauli ya Nchimbi inayotututaka Wananchi kupigania katiba mpya inafikirisha sana

Watanganyika tuwe Makini: Kauli ya Nchimbi inayotututaka Wananchi kupigania katiba mpya inafikirisha sana

KAURI HII YA NCHIMBI ITATUFANYA TUFANIKISHE JAMBO LETU LA KUICHUKUA NCHI KUTOKA KWA WAHUNI WALIOMUUA POLEPOLE SIKU YA TAREHE 8 MWEZI WA 8 MWAKA 2026 AMBAPO TUTAFANYA MAANDAMANO MAKUBWA MARA 100 YA ILIVYOKUWA MO29.WATANGANYIKA TUJITOKEZE KWA WINGI SIKU HIYO YA KUKINUKISHA MARA YA PILI.
 
tupe neno la faraja tafadhali
Hii nchi hata apewe nani kama baadhi ya mambo yasipofanyiwa mabadiliko malalamiko hayatakoma kamwe

Kuna wengine kutwa wanapiga makelele kuhusu demokrasia lakini ukichunguza wao wenyewe demokrasia hawaiwezi wala hawaiishi

NB :Siasani ndipo sehemu nomero uno kwa maigizo mfano wa cinema zetu
 
Wanawachezea Akili tu ili kutuliza vugu vugu la uvunjifu wa amani lililopo nchini ,

Wana push hiyo agenda ili wananchi wasahau Yale yaliyopita halafu mkisha sahau Mtaletewa agenda nyingine itakayo wafanya matoke kwenye mkakati wa kudai Katiba mpya
jamaa Wana sifa ya kujua kusukuma kete, bahati mbaya kwao watanga na njia tanganyika wamechoka kitu kinaitwa CCM Kwa jema au baya
 
Usiwamini kichwa kichwa
Sawa, lakini kuongea hadharani kauli ambazo watu wa serikali na chama chako wamekuwa wanazikwepa, walau apongezwe kwa hilo

IMG-20260724-WA0030.jpg
 
Hawawezi kutoka kirahisi hivi hizo janja janja tu ukiona wameanza kusukuma agenda kama za wapinzani hapo jua Kuna upepo wanaupoza kusahaulisha yaliyotokea alafu baadae game linaendelea vilevile,nyoka ni nyoka tu hata avue gamba nashauri asiaminike hata kidogo huu ni mtego
NAKAZIA
 
Hii nchi hata apewe nani kama baadhi ya mambo yasipofanyiwa mabadiliko malalamiko hayatakoma kamwe

Kuna wengine kutwa wanapiga makelele kuhusu demokrasia lakini ukichunguza wao wenyewe demokrasia hawaiwezi wala hawaiishi

NB :Siasani ndipo sehemu nomero uno kwa maigizo mfano wa cinema zetu
Nakubali mtoto mzuri, na ndio maana katiba mpya itakayotoa mazingira sawa ya ushindani na kura za wananchi kuheshimika ni muhimu , ili kila baada ya miaka mitano wananchi tuwe na nguvu ya kumuweka mtu mwingine au chama kingine , hakuna nchi isiyokua na lawama na hazijawah kuisha lakini angalau maamuzi ya wananchi kuhusu wanaetaka awaongoze yaheshimike
 
Kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwamba Watanzania tunapaswa kupambana kupata Katiba Mpya ni kauli kubwa na yenye uzito mkubwa kisiasa.

Soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Kwa muda mrefu, madai ya Katiba Mpya yamekuwa yakisukumwa zaidi na vyama vya upinzani, wanaharakati, wanasheria na wananchi tunaoamini kuwa mfumo wa sasa haujatoa ulinzi wa kutosha kwa haki za raia, uwajibikaji wa viongozi na mgawanyo wa madaraka.

Kwa hiyo, kiongozi mkubwa wa CCM anapotumia lugha hiyo, tunapaswa kujiuliza: Je, huu ni mwanzo wa mageuzi ya kweli, au ni mkakati wa kisiasa wa yeye binafsi na chama chake kujijenga kuelekea uchaguzi wa mwaka 2030 na mateso ya milele kwa watanganyika?.

Binafsi mimi mwehu ndama nimefanya tafakuri ya kina na kugundua hii pia inaweza kua ni geresha ama changa la macho lingine, hapa ccm wanajibadirisha kama kinyonga kwa lengo la kutuumiza zaidi na sababu zangu ni kama ifuatavyo

1. Political repositioning — kujibadilisha nafasi kisiasa​

Inawezekana Nchimbi anajitengenezea taswira ya kuwa mwanasiasa wa maridhiano na mageuzi kutoka ndani ya CCM.

Kwa kuzungumzia Katiba Mpya, haki za binadamu na mwafaka wa kitaifa, anaanza kutumia lugha ambayo kwa kawaida imekuwa ikihusishwa na wapinzani.

Mkakati huu unaweza kumjenga kama mtu anayekubalika si tu ndani ya CCM, bali pia kwa wananchi wasio wanachama wa chama hicho.

Hii huitwa political repositioning: mwanasiasa anabadilisha au kupanua taswira yake ili kuonekana anafaa kwa mazingira ya kisiasa yanayokuja. Tupo macho maamae

2. CCM kuchukua hoja za upinzani​

CCM ina uzoefu mkubwa wa kuchukua hoja zinazopendwa na wananchi na kuzifanya kuwa sehemu ya lugha yake ya kisiasa.
Hii inaweza kuwa njia ya kupunguza nguvu ya vyama vya upinzani.

Hapa nikama wanatuambia kiaina tena kwa njia njia isiyo ya moja kwa moja kwamba:
“Hatuhitaji kuiondoa CCM ili kupata Katiba Mpya, kwa sababu hata viongozi wa CCM wanaitaka.”

Katika siasa, mbinu hii huitwa co-optation. Chama tawala kinachukua hoja za wakosoaji wake na kuanza kuzizungumza, ili kupunguza ushawishi wa wale waliokuwa wameziasisi. Nasisitiza watanganyika sio wajinga tuko macho maamae

3. Kupima upepo wa kisiasa​

Kauli hii ya bwanyenye Nchimbi inaweza pia kuwa trial balloon, yaani njia ya kupima mwitikio wa wananchi.

Hapa wafuasi wa chama cha mauaji (ccm) wanaweza kutaka kuona:

Je, wananchi watampokea Nchimbi vizuri akizungumza lugha ya Katiba Mpya?

Je, wanaharakati na wapinzani watamwamini?

Je, wanachama wa CCM watakubali msimamo huo?

Je, taswira hiyo inaweza kumjenga kama mgombea anayekubalika mwaka 2030?

Akikubalika, kauli kama hizi zinaweza kuendelea kuongezeka. Asipopokelewa vizuri, anaweza kusema alikuwa anasisitiza tu wajibu wa wananchi na siyo kutoa msimamo binafsi wa kisiasa. TUKO MACHO MAAMAE

Watanganyika tunasema katiba mpya haitopatikana kupitia hotuba za kindezi na mchongo kama hii ya Nchimbi leo, kauli kama hii itaaminika iwapo Serikali ya CCM itaweka ratiba rasmi ya mchakato wa Katiba Mpya, itaendelea kutumia maoni yaliyokusanywa katika mchakato uliopita, itahakikisha wananchi wanashiriki kwa uhuru, itatoa nafasi sawa kwa vyama vya upinzani, wanaharakati na wadau wengine, itarekebisha sheria zinazobana uhuru wa kisiasa na haki za raia, na Nchimbi ataendelea kusimamia msimamo huo hata pale utakapogusa maslahi ya CCM.
Sawa, sasa tuendeleze hapo hayo aliyoyasema na tuipambanie katiba mpya sasa kwa nguvu zaidi.
 
Deni la Oktoba 29 malipo yake hawana ..nje ya kuchapika Uchaguzi wa 2030.
Hasira iliyoko Mtaani huku haidhibitiki...ajabu wanaongeza chuki kwa kufungua kesi za Ugaidi ili kutisha na kukomoaa watu.
hajui wanachotaka
 
Mbona hamnajema nyie. Lengo lenu ni nini hasa? Vurugu nchini au mnataka nini. Ujue hata sisi ambao hatuna upande hatuwaelewi.

Mnaungwa mkono mnabeza. Mkikaziwa mnalia. Mnataka mfanyiwe nini? Au mnataka kitokee kipi?
 
Back
Top Bottom