SI KWELI Watanganyika wawili ndiyo walikuwa na shahada ya kwanza mpaka kufikia Desemba 9, 1961

SI KWELI Watanganyika wawili ndiyo walikuwa na shahada ya kwanza mpaka kufikia Desemba 9, 1961

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Habari ndio hiyo wakuu,

Mpaka Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961, ni wananchi wawili tu walikuwa wamesoma kwa kiwango cha shahada ya kwanza(Degree).

Wa kwanza alikuwa ni Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa ni Rais wa kwanza na baba wa Taifa. Mwalimu Nyerere alikuwa na Degree ya Uchumi, akachanganya sheria na mambo mengine.

Mtu wa pili alikuwa mzee mmoja wa Kisambaa, jina limenitoka. Huyu mzee alikuwa na shahada ya kwanza ya Uhandisi(engineering).

Asante sana

Nyerere.jpg
 
Tunachokijua
Kabla ya Uhuru Tanganyika ilipitia chini ya Utawala wa Wakoloni mbalimbali Wajerumani wakiwa wa kwanza na Baadaye Waingereza wakafuata baada ya vita ya pili ya Dunia.

Suala la Elimu Kabla ya Tanganyika kupata uhuru lilikuwa la kimatabaka, ambapo kwa kiasi kikubwa watoto wa wakoloni walipata fursa ya kupata Elimu Bora wakati Waafrika wachache walipata Elimu ya ngazi ya chini isipokuwa kwa watoto wa Machifu na viongozi wa kiafrika.

Kama alivyodokeza mleta mada hii kutokana na historia hii ya Elimu zipo fununu kwamba mpaka kufikia Miaka Desemba 9, 1961 ni Nyerere pekee ndiye alikuwa Mtanganyika aloyefanikiwa kuwa na Shahada (Bachelor Degree). Fununu hizi zimesambaa na kuaminiwa na watu mbalimbali kutokana na historia ya Elimu kwa Watanganyika wengi kutopatikana kirahisi. Kwa asilimia kubwa historia inakulika zaidi Watanganyika walioshiriki kwenye harakati za kupigania uhuru.

Je, ni kweli Mwalimu Nyerere alikuwa ni Mtanganyika pekee Mwenye Shahada?

JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vinavyoelezea historia ya Elimu kwa Watanganyika Ili kupata uhalisia wa hoja hii ambapo tumebaini yafuatayo:

Ukurasa maalum wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Tanzania umeeleza kwa kina Wasifu wa Mwalimu Nyerere ukijumuisha historia ya maisha yake pamoja na Elimu yake.

Ukurasa huu unadokeza kwamba Mwalimu Nyerere alihitimu Shahada yake ya kwanza mnamo 1945 katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Na akachukua Shahada Umahiri mwaka 1949 katika Chuo Kikuu cha Edinburgh nchini Uingereza.

Zaidi ya hayo, ukurasa huu unatudokeza kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mtanzania wa pili kupata Shahada Kabla ya Uhuru. Andiko linaeleza:

Alihitimu mwaka 1952. Alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Uingereza na Mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.
Sehemu hii ya andiko hili inatupa dokezo muhimu kuwa licha ya Mwalimu Nyerere kuwa Mtanganyika aliyepata Shahada Kabla ya Uhuru lakini kulikuwapo na Watanganyika wengine walikuwa na Shahada kwa wakati huo.

Zaidi ya hayo, mnamo Machi 14, 2023 Mwanachama wa JamiiForums anayeitwa Mwl.RCT alileta andiko lake lililoeleza na kutaja majina 30 ya Watanganyika walikuwa na Shahada ya Awali (Degree) mpaka Shahada ya Umahiri (Masters) Kabla ya Uhuru (Desemba 9, 1961). Zaidi ya Mwalimu Nyerere baadhi ya watu walioelezewa kwenye andiko lake ni hawa wafuatao.

Amon James Nsekela Alikuwa mhitimu wa awali wa Chuo Kikuu cha Makerere, akipata shahada ya kilimo. Baadaye alienda Marekani katika Chuo Kikuu cha Pacific ambako alipata Shahada ya Umahiri (Masters) mwaka 1960. Amon James Nsekela aliwahi kuwa alifanikiwa kibiashara na akahudumu kama mwenyekiti wa kwanza wa Tanzania Breweries Limited kutoka Afrika. Pia ameshawahi kuwa kiongozi wa Serikali kuanzia mwaka 1974 mpaka 1981.

Dkt. Wilbard Changula
huyu anaelezwa kuwa alipata Shahada ya Tiba kutoka Chuo Kikuu cha London. Baadaye alijiendeleza na kusoma Shahada ya Umahiri (Masters) nchini Marekani ambako alohitimu mwaka 1959. Inaelezwa kuwa baada ya kuhitimu masomo yake alikuwa daktari maarufu na kiongozi katika mapambano dhidi ya malaria nchini.

Anzaneth Lema alikuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kupata shahada kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza mwaka 1959 . Alikuwa mwalimu na kiongozi katika harakati za haki za wanawake nchini Tanzania. Wengineo kutoka katika andiko hili watazame katika kiambatisho hiki hapa chini:

1678782382087-png.2550291

Taarifa za wahusika wengi walio katika orodha hiyo hazipatikani katika mitandao, huenda kwa sababu hawakuwa watu maarufu lakini zinatupa dokezo muhimu kwamba si Hayati Mwalimu Nyerere pekee aliyekuwa na mpaka kufikia Desemba 9, 1961.

Zaidi ya hayo kuna taarifa zinaeleza kuwa Chifu Mwami Theresa Ntale aliyekuwa mtoto wa Chief wa Waha Kigoma alipata fursa ya kwenda Ulaya kusomea Sheria ma baadaye alisaidia masuala ya Sheria katika harakati za kudai uhuru. Vyanzo vinavyoeleza Elimu ya Chifu Mwami havibainishi alisomea Sheria katika kiwango gani.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo vilivyopitiwa na JamiiForums tunaona kuwa si kweli kwamba Watanganyika wawili akiwamo Mwalimu Nyerere ndiyo walikuwa na Shahada. Vyanzo vinaonesha walikuwapo Watanzania wengi ila kutokana na kutokuwa maarufu changamoto za kiteknolojia, taarifa zao hazikuhifadhiwa kimtandao na hazikufahamika na wengi.
Back
Top Bottom