Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

Kwahio kujua Kiswahili ni moja ya requierments za kujiunga JF ?...
Hapana, lakini nakupa ushauri wa bure tu. Jifunze kuandika na kuongea kwa ufasaha; iwe ni lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Si vyema kudonyoa donyoa vijimaneno vya hapa na pale. Utaonekana ni limbukeni tu kwa kufanya hivyo.😂
 
Hapana, lakini nakupa ushauri wa bure tu. Jifunze kuandika na kuongea kwa ufasaha; iwe ni lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Si vyema kudonyoa donyoa vijimaneno vya hapa na pale. Utaonekana ni limbukeni tu kwa kufanya hivyo.😂
Ushauri wa Bure, hapa hatuandiki thesis.., ni muhimu ujumbe ufike... mwisho wa siku issue ni communication, ukianza kufuatilia uwasilishaji wa points za watu kwenye social media (na sio jukwaa la lugha) ni kupoteza muda wako; Pili ukifanya vitu kwa hofu watu wanakuonaje ni dalili za inferiority complex... (wewe fanya kinachokuja kwako kwa urahisi)
 
Unakuwa na mtangazaji Mauldi Kitenge, Eddo Kumwembe hawa hawana shule ya Uandishi wa habari ni ujanja wao na kulaghai watu. Baraka Mpenja kaenda shule ila mropokaji na wala sio mtangazaji. Fuatilia goli la Dube alivyotangaza kuna maneno aliropoka kuhusu Dube. Ama fuatilia goli la Aziz Ki alilofunga dhidi ya Simba alivyoropa maneno ya kijinga. Anaropoka baada ya kutangaza maneno ya kiswahili fasaha. Pia wamiliki wa hivi vyombo hawalipi vyema wafanyakazi wao. Mfano pale Azam media pana njaa ya kufa mtu. Na media zingine nyingi tu zina malipo hafifu kwa wafanyakazi wao.
 
Siku nasikiliza wasafi wanaelezea mpira maana sio kuchambua ,nikaacha kabisa kusikiliza kipindi cha michezo radio yao,

Lakin nashangaa humu ndani kuna watu wanawasifia sana wakina ambangile ,george job ,aiseee tz hakuna wachambuzi wa mpira.

Hawa jamaa hawana jipya kabisa ni wajanja wajanja tu wasio taka kupoteza mashabiki oya oya
 
Acha uongo. Kuna media inalipa vizuri kama Azam tz?
 
Na wewe nawe ni kama vile hujui vizuri Kiswahili. Yaani unabaki kudokoa dokoa vijimaneno ya Kiingereza alimradi tu uonekane unajua Kiingereza. Unakera kweli kweli na huo ulimbukeni wako.

KeyserSoze endelea tu na ulimbukeni wako. Sina shida na hilo kabisa.
Hivi unajua hata unachokielezea ?!!, Au ukiweka fullspot unasahau ulichokiandika kabla ?

Nadhani ni vema ukazipitia fikra zako kichwani mwako kabla haujazitoa katika hadhara...

Inaonekana kichwa chako kina internal conflicts
 
Bongo watangazaji wa hovyo kabisa ni hawa wa habari za michezo(wachambuzi) wemginwao ni waongo waongo mfano yule Tupatupa wa clouds sio mara moja anatoa matokeo ya uongo ya mechi zilizochezwa,,,na kuna vitu vingi hawajui
 
Kwahio kujua Kiswahili ni moja ya requierments za kujiunga JF ?

Ukitaka definition ya Ulimbukeni ni hicho ulichoweka hapo juu.....
Kwahio= kwa hiyo
moja ya requirements=moja ya vigezo
definition ya ulimbukeni=tafsiri ya ulimbukeni.

Endelea na huo ulimbukeni wako huku unajiona mjanja. Kama nilivyosema; sina tatizo kabisaa.
 
Hivi unajua hata unachokielezea ?!!, Au ukiweka fullspot unasahau ulichokiandika kabla ?

Nadhani ni vema ukazipitia fikra zako kichwani mwako kabla haujazitoa katika hadhara...

Inaonekana kichwa chako kina internal conflicts
fullspot = full stop, au unaweza kuandika nukta..
 
Kuna mmoja wa RFA huenda alikulia kwenye ubanda,ikiwa ni saa 12:30 asubuhi kwake ni saa 12:00 kamili asubuhi na hana marekebisho.
 
Baby Mama hanaga ufahamu wa vitu vidogo kabisa ambavyo kwa nafasi yake lazima ajue. Inafika kipindi hadi wenzake wanamrekebisha.
 
Mimi haswa na kerwa na Tv stations/ on line Tvs/ Radio station kupiga soga la watu watatu ama zaidi wakibishania jambo ambalo kika mtu halijui na hana majibu ya usahihi nalo.

Halafu kwenye blogs utakuta zinatupiwa takataka za uongo You Tube zenye kuleta taharuki katika jamii lakini mamlaka zimekenua tu meno bila kuchukua hatua madhubuti kukomesha kabisa hawa makanjanja wa tasnia ya habari.
 
Hii inaletwa na Kuwepo kwa mitandao ya kijamii. Karibu habari zote unazipata mitandaoni, Hata ukisema usikilize radio ama tv ni kama kurudia yale yale.
maana simu zinajitosheleza video picha , sauti na maelezo kiujumla.
Kwa hiyo uwepo wa mitandao ya jamii ndiyo kunafanya waajiri watangazaji wasio na weledi? Unakuta eti Kingwendu, Stan bakora, Mpoki na wengineo eti wanajadili habari na kuchambua magazeti kweli?? Walisomea journalism lini?
 
Kukemea mambo ambayo hayako sawa kwenye jamii ni jukumu letu sote. Hata kama mimi nina source ya kupata reliable information bado nina wajibu wa Kukemea upotoshwaji wa habari pale unapofanyika kwa sababu athari zake hurudi kwa jamii.
 
Kukemea mambo ambayo hayako sawa kwenye jamii ni jukumu letu sote. Hata kama mimi nina source ya kupata reliable information bado nina wajibu wa Kukemea upotoshwaji wa habari pale unapofanyika kwa sababu athari zake hurudi kwa jamii.
Kukemea na Kufungia ni vitu viwili tofauti..., Na huko Youtube kumejaa Channels ambazo ni Click Baits na nyingine ni conspiracies mwanzo mwisho, sasa tukianza kufungia vichaa wachache mwisho wa siku tutakuta hata wale ambao tunawaona kwa jicho letu kwamba ni vichaa tutawafungia..., Na wale vichaa wanaokubaliana na sisi tutawaachia...

Pia tukifungia kila kiumbe anayesema fulani kafufuka (kwamba haiwezekani) huoni tunaweza tukafungia Zaidi ya Robo tatu ya Dunia kwa Imani yao kuhusu Ufufuko ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…