Ninakubaliana na wewe, na nitakwenda mbali zaidi ya hapo; pamoja na kwamba umekwepa au hukuelewa nililenga nini juu ya swali hilo nililouliza kwa maksudi tu!Kipindi cha nyuma tulikuwa na Watangazaji wa Maaana na Waandishi pia, na ndioa maana wakawa aanapata Platform hadi kwenye vyombo vya nje kama BBC na VOA au Sauti ya Ujerumani, ila kuanzia awamu ya 5 ndio kila kitu kilichange hadi leo hii. Kwa saaa tuna Comediam, mtu kama Kitenge kutoka Mtangazaji hadi kuwa Comedian.
Angalia mtu kama Salim Kikeke kwa sasa yule ni Chawa. vyombo vya nje ndio maana kwa sasa vimejaa watangazaji kutoka Kenya tu.
Hapo kati kati ndio mambo yamekuja kuvurugika kabisa.
Jamii yetu ya kiTanzania ndiyo inayo poromoka, siyo watangazaji au waandishi wa habari pekee.
Kama unadhani nakosea, jaribu kutazama taasisi zetu zote, unitajie ni ipi unayoona inafanya shughuli zake ipasavyo!
Tafiti kwenye vyuo vyetu vikuu, umetazama huko, ukakuta kuna unafuu wowote? Ma-profesa wetu sasa hivi umesikia hata mmoja kachapisha chapisho lolote la mtu kusifia na kujivunia kazi hiyo?
Sasa sote tumebaki kuwa 'MAITI', kama tulivyo batizwa kiukweli kabisa. Hawa maiti wenye uhai kidogo ndio hao wanaojisalimisha CCM ili wawe maiti moja kwa moja.
Tumefikia hali mbovu kabisa kama nchi.