Watangazaji wenye uwezo wa kifedha wasome Masters au PG Diploma darasani au Online lakini lazima wawe na Shahada yoyote ya kwanza

Watangazaji wenye uwezo wa kifedha wasome Masters au PG Diploma darasani au Online lakini lazima wawe na Shahada yoyote ya kwanza

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Sakata la Bodi ya Ithibati limezua janga na wengi wa watangazaji wamekwama kuendelea na shughuli za utangazaji kwani tasnia hiyo yahitaji uwe na cheti cha ngazi ya Diploma.

Lakini nina ushauri kwa watangazaji wengi ambao wana shahada yoyote ya kwanza kwamba wana uwezo wa kusoma shahada ya uzamili katika chuo chochote kikuu ndani ya nchi au nje ya nchi.

Naamini watu kama Maulidi Kitenge na wengine akiwemo baba Levo wana uwezo wa kifedha hivyo waweza kusoma kozi ya shahada ya uzamili katika chuo vikuu kama UDSM na SAUT mwanza.

Baba Levo endapo atashinda ubunge ataweza kusoma Online katika vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na Marekani hivyo kuendelea na shughuli zake na jioni aingia darasani.

Sina uhakika na elimu ya Maulidi Kitenge lakini kama hana hata cheti, basi aweza kujiunga na TSJ na kuanza upya na asiguse kipaza sauti kwa "considerable time" hadi atapofuzu.

Mwijaku nasikia ana shahada hivyo aweza kusoma Masters popote pale inohusu media.

Vyuo vikuu kama SAUT vyatoa kozi ya mawasiliano yaani Masters in Arts and Mass Communication na vingine barani Afrika.

Hapa nilipo Brooklyn kuna vyuo vikuu kama Columbia, Syracuse, Chuo kikuu cha New York kupitia taasisi yake ya Arthur L. Carter Journalism Institute na chuo cha Graig Newman Graduate School of Journalism.

Kwa mfano chuo cha Graig Newman chatoa shahada ya uzamili ya M.A. Journalism ambayo itamchukua mwanafunzi miezi 16 na wachagua topic moja kati ya Arts and Social reporting, business au economic reporting.

Baada ya hapo mwanafunzi ana uwezo wa kuchagua eneo moja la kua master au One media Format yaani kati ya Audio, Data, Broadcast TV News au Documentary.

Masharti ya kozi hii na kupata viza ni lazima uchukue 9 credits na uzionyeshe katika maombi ya viza hiyo la sivyo utanyimwa viza.

Hiyo upande wa Marekani lakini pia nchini Uingereza wana kozi nyingi mno za kuhusu Media na zenye mshiko khasa kwa wale wote ambao tiyari wana shahada ya kwanza, iwe ni BA (hons) kwenye Arts, Media, Economics na fani zingine.

Kwa habari zaidi soma hapa na uperuzi ndani kwa ndani :Online Master's Degree - NYU Journalism

Maombi kwa ajili ya ya kusoma kozi hii tiyari yamefunguliwa yaani Spring 2026 na maombi hayo yatafungwa tarehe 1 December 2025.

Kwa wale wanotaka kufaya maombi kwa ajili ya masomo ya 2026/2027, mwisho wa maombi hayo ni mweiz Julai 2026.

Uingereza kipo chuo kikuu cha Westminster ambacho kipo katikati ya jiji la London ambacho chatoa kozi ya ngazi ya Masters katika utangazaji iitwao Multimedia Journalism (Broadcast) MA ambayo yawafaa sana wale graduates ambao hawahitaji kurudi kwenye Diploma ya kawaida.

Kozi hii yachukua mwaka mmoja lakini ina ada kubwa kidogo yaani pauni za Uingereza zipatazo 17,500 kwa wanafunzi wa kimataifa. Kozi hii yajumuisha topics zifuatazo :

1. Digital Journalism Production
2. Media Law, Ethics and Regulation
3. Multimedia News reporting
4. Broadcast News
5. Documentary- Story telling
6. Final Journalism Project

Mwanafunzi pia una option ya kumaster eneo moja kati ya yafuatayo:

1. Digital magazine Publishing
2. Investigative Journalism
3. Podcast Production
4. Travel Journalism

Kwa taarifa zaidi kuhusu kozi hii ambayo yaanza mapema mwezi Spetember mwaka huu fuatilia kupitia hapa: Multimedia Journalism (Broadcast) MA - Courses | University of Westminster, London

Cha msingi hapa kuhusu kozi hii ni kwamba ni lazima uite timu nchini Uingereza kusoma kwa mwaka mmoja kwani hakuna option ya kusoma Online.

Hizi shahada za uzamili ni shahada murua kabisa kwa watangazaji mahiri lakini ambao wahitaji kujiongeza na pia ni fursa nzuri kwa vijana ambao wazee wao wamenenepa fweza za kutosha na wana akaunti zilonona kwenye mabenki huko.

Tanzania huko mbele ni lazima iwe na watangazaji ambao wamesomea mambo ambayo wayafanya ili kuweka heshima katika tasnia kama hii ya Habari na Utangazaji.

Nawatakia weekend njema.

BTW:
Richard ana BA (Hons) na Msc katika nyanja za usalama, siasa za jiografia na ulimwengu na yupo JF kitambo kama mshauri wa kamati ya ufundi.
 
Kwa Kitenge nadhani ana cheti, kwa Zembwela sina hakika...Daah wazee wa kunyamatika wamepigwa ndongaz......
Chumviiiiiiii
Chuma cha pua Beberu.....
 
Back
Top Bottom