Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Huko kwenye YouTube blogs ndio balaa kabisa. Hiyo Reginald ilivyokuwa ikitamkwa, pacemaker, coopers and Lybrand au pricewaterhousecoopers ni vichekesho. Wenyewe wanakusisitizia ujiunge nao, hata neno subscribe linavyotamkwa ni kituko!
Tz tuna safari ndefu sana, hapa tulipo sielewi kama tumeianza hiyo safari au tumeipa kisogo tunaelekea kusikojulikana!
 
Na jina "François" pia ni tatizo kubwa kwa watangazaji wengi. Hata jina "Jean". Na mengine mengi tu.

Nafikiri suala muhimu ni maandalizi hasa kwa wasoma habari (maana hapa urasmi ni mkubwa zaidi). Weweke utaratibu wa kujiandaa, kutafiti au hata kuuliza pale wasipojua. Tena kwa kizazi hiki cha .com ilipaswa kuwa rahisi zaidi....lakini ndio hivyo tena!
 
Kuna mchezaji anaaitwa MAGUIRE ( Tamka = Magwaya). Lakini jambo la ajabu kuna mtangazaji mmoja alikuwa anatamka kama anataja jina la Kiswahili
 
Mchukue mzungu atamke jina la mtanzania wa kabila la kimeru 'Palangyo'. Utamkaji wa maneno mara nyingi huathiriwa na lugha ya mahali husika.
 
Unatamka vocha Shtenzni hiyo ni kwa watu wa kwao Poland.

V inakuja mwanzo badala ya herufi "W"

Wazungu wa Uingereza wao wanatamka Wojech Shyzeny

Ila sisi chama la gunners tuliamua kumuita "Cheza".

🙂🙂
Mkuu hii hatari, sasa kule alikolazwa Tundu Lissu .... Brussels. Utasikia bluseliz!
 
Umeleta mada iliyonisumbua siku nyingi,juzi tu nilikuwa ninaangalia taarifa ya habari,mtangazaji kwa kujiaamini akasoma jina hili kama linavyoaandikwa JOE BIDEN,badala ya Jo Baiden,nimekuwa nikijiuliza huyu mtu ni mwana habari asiyesikiliza vyombo vya habari vingine,ili angalau aelewe matamshi.Kuna majina magumu kama ya watu wa Poland ambayo unaweza ukakuta jina lina consonant tupu bila hata vowel moja na ni refu kutoka bega la kushoto hadi bega la kulia ,nilizima usikilize ili uelewe linavyotamkwa.Kuna wanaopatia lakini wameathiriwa na ubantu kwa mfano one mtu badala ya kutamka wan,yeye anatamka wani.Hii ndio badala ya kutamka tongue=tang mtu anatamka tongue kama inavyoandikwa.

Huyo mtangazaji nguli wa michezo anatoka Nyota Tv,yule nadhani hata ukimtangazia dau hawezi kutamka Leicester kama inavyotakiwa,wewe ukiona mtu anatangaza mieleka ya WWE kana kwamba ni mchezo halisi na wa kweli,unapaswa kupambanua mwenyewe nini ni nini hapo.Ndiye mtangazaji pekee duniani anayetoa matokeo ya wwe,hata wenzake kwenye hicho kituo wakiwa zamu kusoma habari za michezo hawaleti hizo habari za wwe.
 
Kwenye "w"weka V=Vainadam,hata Wenger inapaswa kuwa Venga,badala ya wenga,mara nyingi majina yenye asili ya Kijerumani IKiandikwa W =V,kwanini Venga,badala ya Wenga,ni kwasababu anatokea ufaransa,kwenye jimbo linalo zungumza kijerumani.
 
Binafsi naamini kwa vile lugha sio yake, na maneno mengi ni lugha tofauti na yetu kiasili, lazima kuwe na makosa ya kimatamshi.

Mfano mtangazaji anasema Jirudi (Giroud), hili ni jina la kifaransa, wafaransa huwa majina yanayoishia na consonants hawatamki (Giroud-Girou).
 
Mkuu hii hatari, sasa kule alikolazwa Tundu Lissu .... Brussels. Utasikia bluseliz!

Kuna matamshi ya aina mbili kifaransa na kidachi

Kwa kidaransa wanaandika Bruxelles na inatamkkwa Bruiseil.

Kwa kidachi wanaandika Brussel na wanatamka brwseil yaani kwenye brv wanatamka bra na seil brvseil.

Kwa wale walosoma HGE ya uhakika watakumbuka yale maandishi ya phonology ambayo yanasaidia kupata sauti ya kutamka maneno na alama zake.

Hivyo vyuo vya uandishi wa habari wangeangalia wanafunzi hodari wa HGE na kuwaiba mapema wawe wataalam wa kutamka maneno kwa ufasaha.
 
Binafsi naamini kwa vile lugha sio yake, na maneno mengi ni lugha tofauti na yetu kiasili, lazima kuwe na makosa ya kimatamshi.

Mfano mtangazaji anasema Jirudi (Giroud), hili ni jina la kifaransa, wafaransa huwa majina yanayoishia na consonants hawatamki (Giroud-Girou).
Achana na hio, mtu ni mtangazaji wa tv,huyo ni pro inabidi ajue au atafute usahihi sio Lester(Leicester) unatamka lesesta.
Kwa watu wa mtaani kwenye vibanda umiza tunawasikia ila tunawaelewa ila hawa ma pro inabidi wajishughulishe kidogo,hata ukisikiliza watangazaji wenzio utasikia matamshi sahihi
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
"To-Te-ni-ham" badala ya "Tot-nam" 😁😁😁 tatizo lao kubwa ni kujifanya wanajua wakati hamna kitu. Angalia hata wakialika mtu Studio wao ndio hugeuka wajuaji wa kila kitu kuliko hata yule mtaalamu waliyemualika!
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Mbona yuko sahihi,!yeye kalitamka kwa lafudhi ya kiswahili na wewe unataka atamke kwa lafudhi ya kiingereza(wala si ya kizungu)ndio maana ukimsikia mzungu yeyeto akizungumza kiswahili anakiongea kwa lafudhi ya kwao.john (yohana)moses (mussa)marko(maiko),,,
 
Hii kitu nimewahi kuiona zaidi ya Mara mbili, Mfano mtangazaji badala ya kutamka "soul" kwa maana Seoul (Mji mkuu wa Korea kusini) mtangazaji anasema "seuli"

Kwa hiyo mkuu uko sahihi mi nadhan wanapaswa kujifunza namna sahihi ya kutamka baadhi ya maneno.
Inategemea anazungumza lugha gani,kama ni kiswahili lafudhi lazima iwe ya kiswahili,ndio maana huwezi sikia mtangazaji wa kiswahili akasema south africa,utasikia afrika kusini,england utasikia uingereza,ureno,nk
 
Back
Top Bottom