Umeleta mada iliyonisumbua siku nyingi,juzi tu nilikuwa ninaangalia taarifa ya habari,mtangazaji kwa kujiaamini akasoma jina hili kama linavyoaandikwa JOE BIDEN,badala ya Jo Baiden,nimekuwa nikijiuliza huyu mtu ni mwana habari asiyesikiliza vyombo vya habari vingine,ili angalau aelewe matamshi.Kuna majina magumu kama ya watu wa Poland ambayo unaweza ukakuta jina lina consonant tupu bila hata vowel moja na ni refu kutoka bega la kushoto hadi bega la kulia ,nilizima usikilize ili uelewe linavyotamkwa.Kuna wanaopatia lakini wameathiriwa na ubantu kwa mfano one mtu badala ya kutamka wan,yeye anatamka wani.Hii ndio badala ya kutamka tongue=tang mtu anatamka tongue kama inavyoandikwa.
Huyo mtangazaji nguli wa michezo anatoka Nyota Tv,yule nadhani hata ukimtangazia dau hawezi kutamka Leicester kama inavyotakiwa,wewe ukiona mtu anatangaza mieleka ya WWE kana kwamba ni mchezo halisi na wa kweli,unapaswa kupambanua mwenyewe nini ni nini hapo.Ndiye mtangazaji pekee duniani anayetoa matokeo ya wwe,hata wenzake kwenye hicho kituo wakiwa zamu kusoma habari za michezo hawaleti hizo habari za wwe.