Nilipanda eicher la Gongo la mboto lilijaza sana sasa kuna mmama alikuwa kambeba mtoto kasimama sasa kuna abiria alikuwa amekaa kainuka ili ashuke yule mmama ile anaenda kukaa kuna baba hilo limetoka spidi kuwahi ile siti bila aibu yule mmama alikuwa ndio anaketi ikabidi apotezee sasa yule mbaba kakaa katikati ya wamama siti ya nyuma mbona walimchamba [emoji23] mwanaume MTU mzima unashindana na mama mwenye mtoto kukaa kwenye siti ,huna haya maneno kibao
Yule jamaa akawa kauzu anabishana nao na mwishoni kusema nyie simameni huyo mama akae kajikaza
Nilijisikia aibu sana japo sikuwa mm wale wamama waliongea sana kijamaa kauzu kimedinda tu