Watani zangu wasukuma hebu punguzeni matumizi ya vyakula, mnaharibu

Mkuu unanichekesha sana [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Asante mkuu [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kula si kuharibu kabisa. Tunakula ili tuishi. Ukipata nafasi kula haswaaaa
 
Hatuna desturi ya kuharibu kazi sehemu yeyote ile never and ever big up team mangosha
 
Baba yangu alikuwa hali wali kama chakula rasmi. Siku ya ubeche lazima kupikwe ugali kwa ajili ya Baba. Ubeche atasuuzia tu!

Nimemiss ugali wa Kijijini.
Yaani nikifika lazima Kuku aangushwe na samaki juu. Halafu Wasukuma ni mwiko kuwa mchoyo. Chakula kinaliwa nje. Anayepita nje anajumuika tu.

Nakalabhagha kumongho
 
Umenikumbusha siku moja tulialikwa dinner ubalozi wa china hapa DSM. Tukiwa kule tukapewa menu ya vyakula vilivyoandaliwa... Ilikuwa round saba... Kiduchu kiduchu... Wenzetu wachina na kenye ufahamu kidogo wakwa wanakula kidogo wanaacha... Wengine wakawa wanamaliza kila sahani... Kuna mto aliishia round ya tatu na nusu... Wachache tukaenda round ya sita... Hizi ndo zile za kuleni mtori nyama ipo chini...
 
Sababu havina hata uwezo wa kujilisha vyenyewe.

Familia ikifikishq watu watatu tu kinaishi kwa mawazo wakati sisi tunatunza hata familia ya watu hamsini na wakala wakashiba kila siku na vyakula vinabaki. Hahaha
Na hivi vikabila vidogo vina husda sana...hahaaaa
 
Nimecheka sanaaaaa!! Huko ndo ukandani mkuu, huo si utaratibu wa wasukuma tu, utaratibu wa wakanda ya ziwa karibu woteee, kuanzia ukerewe, kwa wakara, wazinza, wajita, wakurya na wengineo.
hivi Bihalamuro na chattle ni kanda ya ziwa? naomba kufahamishwa.
 
Trust me, kwa ukarimu na uaminifu Tanzania hakuna kama wasukuma!

Hawa jamaa wana roho za ajabu sana, ni watu poa sana kuishi nao!
Hivi hao wasukuma unaowaongelea wanaishi mikoa gani huku kahama wenye huo ukarimu sijawaona. Niliowaona wanapenda Kupokea sio kutoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…