Watanzania 5 waripotiwa kufariki kwenye ajali ya Moto Afrika Kusini

Watanzania 5 waripotiwa kufariki kwenye ajali ya Moto Afrika Kusini

View attachment 2735421
Watu wasiopungua 70 wamepoteza maisha na wengine 52 wamejeruhiwa kufuatia moto uliozuka katika jengo la ghorofa tano katikati ya mji wa Johannesberg nchini Afrika Kusini.

Moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la jiji hilo kubwa la Johannesburg.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha jiji la Johannesburg, Robert Mulaudzi, moto huo umesababishapia watu wengine takriban 52 kujeruhiwa.

Hata hivyo Mulaudzi amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi kwa kuwa jitihada ya kutafuta miili ya watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine inaendelea.

Katika taarifa yake ya ziada aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, kampuni ya awali iliyokuwa ikijulikana kama Twitter, msemaji huyo amesema watu kadhaa wameokolewa.

Jengo lililozuka moto ni makazi holela ya watu.

Pamoja na hiyo, akinukuliwa na vyombo tofauti vya habari nchini Afrika Kusini msemaji huyo amesikika akisema jengo hilo lililowaka moto lilikuwa linafanywa makazi kwa wasio na majumba.

Lakini pia mbali ya vifo vilivyotokana na moto, vipo vya baadhi ya watu ambao wanatajwa kufanya jaribio la kuruka kutoka katika jengo hilo refu,katika nyakati za usiku, kipindi ambacho moto huo unaendelea kwa lengo la kutaka kunusuru uhai wao.
View attachment 2735426
Mimi huyo anayenyonga bangi
 
Upumbavu wake nini ndugu yangu, hoja hupingwa kwa hoja, wala siyo kwa kumshambulia mtoa hoja, mimi nimesikia toka BBC asbuhi, wengi wanaishi humo ni wahuni wasio kuwa na makazi, serikali imeenda mahamani mara kadhaa kwa ajili ya kuwaondoa ila ikawa inashindwa kesi.
Majengo sio ya Serikali majengo ni ya watu binafsi waliokimbia SA na kwenda kuishi sehemu zingine Serikali lazima ishindwe kesi maana haina hati za hayo majengo ila makampuni binafsi ya majengo huwa wanapewa vibali kwa kuyaendeleza kwa vipindi na majengo mengi hizo Kampuni zimeyachukua zinakarabati na kukodisha kwa wapangaji...
 
Siwezi kusema kama wamewachoma kwa makusudi ila mengi uliyoyasema yana ukweli.

Binafsi nimewahi kufika hayo maeneo Mungu atunusuru katika utafutaji niliyoyaona kule niliogopa sana halafu sasa nilienda kishua kwenye training SA nikapewa barua niifikishe kwa mwana Raras aka Buti Kubwa kutoka kwa mama yake so nilipofika Johanesburg nikamtafuta na kuna mbongo mmoja akanipeleka anapoishi kwenye hiyo mijengo halafu muda wa jioni giza lishaingia. Raras mwenyewe nilimkuta kazimika na mipombe sijui unga.

Kesho yake niliwasimulia watu nilipoenda wakaniambia mshukuru MUNGU umetoka salama. Nilikuwa nimevaa koti na tai na wakati tunapanda ngazi watu walikuwa wananishangaa sema nadhani giza ndio lilinisaida
You are very lucky boy!!
Maeneo ya wabongo waliochoka ukienda kishua unaweza kuporwa kila kitu including passports.
Miaka ya nyuma walikuwa wanakwenda parkstatiin kupokea wabongo kwenye mabasi wanajidai wanakupa msaada then wanakupeleka doorfontein , ukifika huko unaporwa kila kitu.
 
Si huwa mnasema maisha ni "do or die", sasa unalalamika nini? Huo ndiyo ujinga. Nani alikwambia kwenye maisha kuna "mapigano"?

Uislam unatufundisha rizki anayetowa ni Allah, siyo wizi, ujambazi na kuuza madawa ya kulevyo. Huo ni ujinga na njia za shetani tu.

Huwezi kupigana na maisha isipokuwa uwe ni mjinga tu, usiyeona wala kujuwa unalofanya. Nakushauri anza kuingia hizo "nyumba za ibada" unazozisema ukapate mafundisho ya maisha ni nini.

Pata kilichootokea huko kutoka kwa Watanzania wanaoishi huko kihalali:

Hilo jumba lililochomwa ni la ma "criminals" watupu. Kimeanza kutiwa moto chumba kimoja cha chini, ambacho kilikuwa na walengwa (kimepigwa moto, wakafungiwa ndani, kikapigwa moto kwa makusudi kabisa. Wanne wamekufa humo humo. Waliotia moto lango la kupanda ngazi na kushuka walilifunga asitoke mtu. Wote waliokuwamo ndani ya hicho chumba cha chini wamefia humo humo ndani, mmoja alitoka wapi sijuwi akawaona waliochoma moto, na yeye wakamuuwa wakamtia moto nje ya jengo, wakaondoka zao.

Hao ni criminals tu, tuuseme ukweli. Hata kama wanatafuta maisha, walikuwa hawayatafuri kwa njia za halali.
Mmoja wa wahanga
 
Attachments

  • 1693630085530.jpg
    1693630085530.jpg
    44.1 KB · Views: 3
You are very lucky boy!!
Maeneo ya wabongo waliochoka ukienda kishua unaweza kuporwa kila kitu including passports.
Miaka ya nyuma walikuwa wanakwenda parkstatiin kupokea wabongo kwenye mabasi wanajidai wanakupa msaada then wanakupeleka doorfontein , ukifika huko unaporwa kila kitu.
Wabongo waliopo sauz asilimia kubwa ni wale walioshindikana huku kwetu
 
Siwezi kusema kama wamewachoma kwa makusudi ila mengi uliyoyasema yana ukweli.

Binafsi nimewahi kufika hayo maeneo Mungu atunusuru katika utafutaji niliyoyaona kule niliogopa sana halafu sasa nilienda kishua kwenye training SA nikapewa barua niifikishe kwa mwana Raras aka Buti Kubwa kutoka kwa mama yake so nilipofika Johanesburg nikamtafuta na kuna mbongo mmoja akanipeleka anapoishi kwenye hiyo mijengo halafu muda wa jioni giza lishaingia. Raras mwenyewe nilimkuta kazimika na mipombe sijui unga.

Kesho yake niliwasimulia watu nilipoenda wakaniambia mshukuru MUNGU umetoka salama. Nilikuwa nimevaa koti na tai na wakati tunapanda ngazi watu walikuwa wananishangaa sema nadhani giza ndio lilinisaida
Hatari sana.
 
Acha upumbavu huu, kwako maisha yamekua bora kwa kudhulumu poor of the poorest, kesho unajifanya ni muumini mkubwa mwenye imani wakati umejaa roho ya kikatili, sijui hizi nyumba za ibada mnafanya nini mle,mchawi mkubwa, wewe unajua Mapigano na mahangaiko ya maisha? Endelea kuishi kwenye hiyo AC,but one day upepo utageuka tu, rambi rambi kwa waliofiwa na ndugu zao waliokwenda ku fight for better life, salute kwao wamekufa in the battleground, Amina
Punguza bangi.
 
Watanzania tulivyo waongo utadhani Tanzania hakuna uhalifu ni majuzi tuu nilikua Mbinga nilikaa Songea kama siku mbili pale na jamaa zangu yule jamaa alieuawa mwenye Jeep Nyekundu niliiona gari yake Songea nafika Chuga naona Taarifa ya habari kuwa kauawa na Mtoto wake nilisikitika sana ila haya matukio yapo hapa hapa Tanzania na wahuni walisukuma lile Jeep kwenye bonde kubwa wakitegemea litapindukapinduka lilienda na matairi mpaka huko Chini ndio Polisi wakahisi kuwa hawa wameuawa na kutupwa hapa...
 
Back
Top Bottom