Watanzania acheni chuki kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) sheria za kodi hutungwa na bunge. TRA ni wasimamiaji tu

Watanzania acheni chuki kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) sheria za kodi hutungwa na bunge. TRA ni wasimamiaji tu

Watakua wanafanya uhuni maana account ya mtu inaweza pokea hela popote
T/A haina mipaka mkuu, unaweza pekuliwa hadi Mpesa. Angalau kidogo kampuni ndo kuna limit japo wanaweza pia itisha taarifa zako binafsi kukagua complience.
 
Sheria ziko wazi bosi, ukiona umebambikiziwa kodi tofauti masharti ya sheria za kodi, unaruhusiwa kwenda mahakamani kuishitaki mamlaka na wala hautokuwa wa kwanza kufanya hivyo. Harafu umetumia neno nyie, mimi siyo wao.
Mahakama zipi, hizihizi kibogoyo ya ccm zinazokaa na mashauri zaidi ya miaka minne bila kutoa hukumu?
 
Yani bank imruhusu afisa wa kodi kuchungulia account yako?
Hyo labda kipindi cha JPM.
Nijuavyo bank zina Sheria Kali za kutoruhusu mtu/taasisi kuchunguza account ya bank za watu.
And pia account ya bank haihusiani na biashara kabisa maana pesa unaweza toa na kuweka mara nyingi tu na mzunguko ukawa mdogo
Jichanganye, unapoandaa hesabu utaonesha cash & bank balance ambapo Commissioner general wa TRA ukirejelea ITA Cap 332 amepewa power kuitisha documents yeyote hata cheti cha ndoa sembuse bank statements.
Jichanganye
 
Sio kuchungulia tu wanaweza printiwa Bs.
Huyu jamaa anafikiri kukusanya mapato ni kazi lelemama?
TRA amekuomba bank statements wewe kataa uone kifuatacho.....

Aachane na wahuni wa mtaan watampoteza,
Kwa CG TRA hana mamlaka ya BANK Account, hiking kichekesho jaman.
 
Mbuzi wa bwana heri anamjua master.

Bwana heri anajua tabia za mbuzi wake.
 
Hakuna bunge linatunga sheria,Sheria zinaandikwa na watumishi wa Taasisi husika,kisha hupelekwa huko Bungeni kupitisha.
Mfano,leo hii uongozi wa TRA ukaona kitu kinatakiwa kianzishwe basi zinaandikwa hizo sheria kisha zinapelekwa huko kupata idhini.

Kiufupi Duniani wabunge hawana kazi yoyote zaidi ya kula mishahara ya bure.
Eti jamani 😁😁 wabunge wenyewe wa kukaa waandike sheria wako wapi
 
Wewe sio mfanya biashara Wala haujawahi kufanya biashara

Mfanyabiashara anaenda kulipa Kodi TRA unamwambia alipe na 10% ya Kodi ya pango
Sasa ebu niambie kama Kodi ya pango anatakiwa alipe mmoliki wa jengo Kwa TRA inamlazimisha alipe mfanya biashara
Nitajie kifungu Cha Sheria kilichopitishwa na bunge kinachomtaka mfanyabiashara alipe Kodi ya jengo ambalo yeye sio mmiliki

Alafu ati wanakuambia kamwambie mmiliki wa jengo akurudishie Kwa Nini TRA wasiende wenyewe Kwa wamiliki wa majengo kuchukua hiyo Kodi?

Kuna kipindi nilienda TRA kumbadirisha jina la TN yangu lisome jina kampuni

Meneja akaniambia ukitaka hii TN ibadirike na Kodi inabidi ipande

Nika bro hizi ni principal gani za biashara?
Maana biashara ni ilele mtaji ni ilele mauzo ni yaleyale Sasa iweje jina likibadirika ndio Kodi ipande akashikiria msimamo wake mi nikaondoka

Kwahiyo wewe unataka kusema bunge ndio limeoitisha Sheria kuwa mfanya biashara akibadirisha jina la biashara na Kodi ipande?
Huyo ni afisa wa Tiharahei we hujamuona tu?
 
Back
Top Bottom