Watanzania acheni chuki kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) sheria za kodi hutungwa na bunge. TRA ni wasimamiaji tu

Watanzania acheni chuki kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) sheria za kodi hutungwa na bunge. TRA ni wasimamiaji tu

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,952
Reaction score
5,263
Ukipita mitandaoni, sehemu mbalimbali mitaani, iwe mijini na vijijini, lawama za watanzania wengi zimekuwa zikielekezwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwamba ina uonevu mkubwa kwa wafanyabiashara na imekuwa ikianzisha tozo au kodi mbalimbali ambazo zinalenga kumkandamiza mfanyabiashara au mtanzania. Ningeomba ifahamike kuwa TRA hawatungi sheria za kodi na wala hakuna sheria ya kodi inayotekelezwa kama haijapitishwa na bunge. Unapoona kodi yoyote inasimamiwa na TRA basi imepewa go ahead na mamlaka husika na hii inakuwa baada ya kujadiliwa na wawakilishi wetu ambao ndo sauti za wananchi wengi.

Tunaamini kuwa wabunge tuliowatuma wana weledi wa hali ya juu na wanatathimini kwa kina kabla ya kupitisha sheria yoyote ya kodi. Tunaamini wanakuwa wamezingatia maslahi mapana ya nchi hasa ukizingatia kuwa nchi yetu anapambana ili kuhakikisha kuwa tunajitegemea sisi wenyewe na kujiweka mbali na misaada yenye masharti magumu.

Nimekuweka uthibitisho hapa chini kutoka kwenye katiba yetu ya nchi.

Naamini kuanzia sasa na kuendelea kwa wale ambao walikuwa hawaelewi halihalisi ilivyo wataondoa chuki kwa TRA na badala yake wakiwa na maoni watayawasilisha kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wao ili na wao wayapeleke kwenye mamlaka ya kibunge.

Masharti yakutoza kodi Sheria ya 1984 Na.15 ib.43 138.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwakwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge au kwa mujibu wautaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu kisheria nasheria iliyotungwa na Bunge.
Katiba ya nchi.PNG
 
Tatizo siyo sheria, nyie mnabambika kodi, kama sikupi rushwa unazuia mzigo na unanitishia kufilisiwa au kufungwa
Sheria ziko wazi bosi, ukiona umebambikiziwa kodi tofauti masharti ya sheria za kodi, unaruhusiwa kwenda mahakamani kuishitaki mamlaka na wala hautokuwa wa kwanza kufanya hivyo. Harafu umetumia neno nyie, mimi siyo wao.
 
Sheria ziko wazi bosi, ukiona umebambikiziwa kodi tofauti masharti ya sheria za kodi, unaruhusiwa kwenda mahakamani kuishitaki mamlaka na wala hautokuwa wa kwanza kufanya hivyo. Harafu umetumia neno nyie, mimi siyo wao.
Mie nilitaka kushitaki nikatishiwa kuwa serikali haishitakiwi yaani TRĄ na nikifanya hivyo mali zitanadiwa. Nikafyata
 
Sheria ziko wazi bosi, ukiona umebambikiziwa kodi tofauti masharti ya sheria za kodi, unaruhusiwa kwenda mahakamani kuishitaki mamlaka na wala hautokuwa wa kwanza kufanya hivyo.
Kesi nyingi za wafanyabiashara wa kati na chini kwenye makaratasi afisa anakuwa yupo sawa, anakuwa kashika mpini, hata ukienda wapi makaratasi yake yanashinda iwapo uhalisia hautazingatiwa. Sasa kwenye mazingira haya mfanya biashara halioni bunge pale, anamuona afisa muonevu ndo maana analalamika.

Mfano halisi wa kesi:

Afisa amekuta benki zimeingia M300 mwaka mzima ilihali Efd ina M50, anahoji kuwa kuna utofauti wa M250 kwanini? Afisa anahisi hayo ni mauzo hayakutolewa risiti na anapendekeza kodi na adhabu juu.

Lakini uhalisia ni kuwa huo mwaka mfanya biashara alihitaji mkopo, hivyo alikuwa anatoa na kuweka pesa ile ile kuongeza mzunguko, benki ione ana mzunguko, na alifanikiwa na akaupata mkopo, mkopo ambao collateral ni nyumba yake, na nia ni kukuza biashara ambayo ikikua na kodi inaongezeka.

Mfanya biashara anamweleza afisa uhalisia, afisa anasema leta ushahidi kuwa hayo si mauzo, sasa ushahidi gani na alikopa kweli?

Mbaya zaidi Afisa kodi anafanya udadisi wa kodi, duka lina mtaji wa M200, mfanya biashara hana utunzaji mzuri wa hesabu kutokana na gharama za kihasibu, afisa anakuja na mapendekezo ya kodi ya kwenye makaratasi M100 au 150, yaani nusu ya mtaji au zaidi.

Afisa anashindwa kuona kwamba huu si uhalisia wa hii biashara? Biashara inaendeshwa kwa mkopo, njia alizotumia kupata mkopo ndo zimempa afisa kisu cha kuchinja. Unadhani mfanyabiashara ataona bunge ni tatizo au afisa?

Halafu unakuta ni biashara ya miaka mi3 nyuma, afisa alikaa na hesabu miaka mi3 mi4 ndo anakuvamia afanye uchunguzi, marisiti yeshafutika, yamepotea wala hakuna nyaraka za kumbukumbu.
 
Ulitishiwa tu ila hakuna kitu kama hicho
Kodi zina taratibu zake. Unapambana na TRA wenyewe kwanza mkishindwana unaenda kwenye bodi za usuluhishi TRAB na TRAT sio mahakamani. TRA ndo inaweza kukupeleka mahakamani ili ikufilisi.
 
Labda wewe mgeni
Mie nakushangaa
Ukishangaa haiondoi uhalisia boss. Huwezi toka tu ukaenda mahakamani kuishtaki TRA na jalada likafunguliwa. Kuna taratibu za ulalamikaji na kila hatua ina nyaraka. Hatua ya juu zaidi ni bodi ya usuluhisi. Anyway, hii nchi huwa ina maajabu yake nisikupinge, inawezekana wewe una experience tofauti.

Halafu kwa mfanyabiashara wa kati na wa chini ambao ndo walalamikaji wengi hiyo bajeti ya kumlipa mtaalam afuatilie si bora ulipe tu hiyo kodi taratibu?
 
Ukishangaa haiondoi uhalisia boss. Huwezi toka tu ukaenda mahakamani kuishtaki TRA na jalada likafunguliwa. Kuna taratibu za ulalamikaji na kila hatua ina nyaraka. Hatua ya juu zaidi ni bodi ya usuluhisi. Anyway, hii nchi huwa ina maajabu yake sikupingi, inawezekana wewe una experience tofauti.

Halafu kwa mfanyabiashara wa kati na wa chini ambao ndo walalamikaji wengi hiyo bajeti ya kumlipa mtaalam afuatilie si bora ulipe tu hiyo kodi taratibu?
Ningemlipa mtaalamu lakini kwa Tanzania mtalaamu huyo huyo anaweza kucheza mchezo na mtetezi wa mshtakiwa ukashangaa wanagawana. Complicated
 
Tatizo wabunge wanaotunga Sheria ni watoto wa sa100.huwa wanatunga Sheria Kwa manufaa ya mama Yao na kuwa kandamizi Kwa watanzania wengine ambazo siyo ndugu wa Samia.Mfano Kwa Sasa wabunge waliochaguliwa na wajumbe wengi ni ndugu wa Sa100kikwete na baadhi ya mawaziri wastaafu.Yaani bunge Zima 99% ni watoto sa100.Nchi hii inachezewa sana
 
Unabambikiwa ambayo haijatungwa na BUNGE?
HICHO kitu hakipo komaaeni na WABUNGE sio TRA
Kodi haibambikwi nje ya sheria. Kila ongezeko la kodi unaloandikiwa huambatana na kifungu cha sheria. Afisa hapa ana appear clean ila haimaanishi yupo clean au sheria ni tatizo. Sheria % kubwa hazina shida ila mapungufu yapo. Tatizo ni zinavyotumika dhidi ya mifumo ya uhalisia field.

Ndo maana ikitokea afisa akataka pesa na ukampa pesa anajua afanye nini upate haki yako kwa kutumia sheria hizo hizo.
 
Kodi haibambikwi nje ya sheria. Kila ongezeko la kodi unaloandikiwa huambatana na kifungu cha sheria. Afisa hapa ana appear clean ila haimaanishi yupo clean au sheria ni tatizo.
Kodi hiyo Iko Kwa mujibu wa Sheria na Ina code zake kwenye mifumo ya TRA, Sasa AFISA ananufaikaje wkt makusanyo hayapiti kwake?

Ulikuwa unakutana na MAOFISA wavunja au wasiojua Sheria. Sasa pale unapokutana na AFISAValiyenyooka unakuja kulialia
 
Kodi hiyo Iko Kwa mujibu wa Sheria na Ina code zake kwenye mifumo ya TRA, Sasa AFISA ananufaikaje wkt makusanyo hayapiti kwake?
Kuna mazingira anahusika vizuri tu, anaona kabisa hapa uhalisia ni huu, haki ni hii ila kwa makosa ya uandishi na utunzaji wa nyaraka na uhalisia wa hili tukio naweza tumia sheria kupachika kodi hapa na nikawa sahihi. Hapa ndipo anapobeba lawama.

Ujue afisa mla rushwa hali rushwa hatarishi kimaandishi, anakula rushwa isiyo hatarishi, yenye mlango wa kutokea kisheria. Katika mazingira ya matukio ya kodi halali, kodi ya haki, Afisa mla rushwa hata apewe pesa hataitaka, atataka ufate taratibu, ulipe kodi maana si salama kwake likitokea la kutokea. Labda awe boss au katumwa na boss.
Ulikuwa unakutana na MAOFISA wavunja au wasiojua Sheria. Sasa pale unapokutana na AFISAValiyenyooka unakuja kulialia
Mkuu, ukishakuwa mfanya biashara mdogo na wa kati kwa miaka mingi hizi siasa unazielewa. Nina uzoefu kidogo na haya mambo na TRA naishi nao vizuri tu sababu ya uzoefu. Na wengi wao hawana shida ila wapo wapenda rushwa na wana uwezo wa kupachika kodi isiyo ya haki kisheria na wakipata wanachotaka wakafuta hilo pendekezo la kodi, hii haimaanishi kwamba sheria husika ina shida ila ni jinsi ilivyotumika.
 
Back
Top Bottom