Tanzania kinadharia tulikuwa na classless society kwa hiyo tuliokaa Oysterbay hakukuwa na elites ila kulikuwa na wengine tunasoma Newsweek, Time Magazine au hata The Economist. Nakumbuka siku moja Mzee Mwapachu aliniwekea magazeti hayo matatu akaniuliza nachagua lipi kati ya matatu hayo? Kabla sijachagua akaniambia "You get the most from The Economist, not Newsweek or Time Magazine"
Tulikuwa pia tunaangalia Televisheni ya Zanzibar iliyokuwa na vipindi vya nje na baadaye CNN. Wengine walikuwa mpaka na satellite dishes.
Vitabu vya kutoka nje pia vilisaidia sana.
Mambo mengine tulijua kutoka kwenye mitandao ya kifamilia ya watu waliokuwa ndani ya serikali, waliokuwa kwenye kada za kibalozi na kiusalama. Ukiongea na Mr X anakuambia hivi na vile, ukiwa unamjua Mr. X alifanya kazi gani Tanzania utajua kuwa hiyo ni source ya juu sana na inaaminika.
Mambo mengine yalijulikana kwa kutokea mitaani kwetu. Mfano Captain Aziz alipokamatwa na Augustin Lyatonga Mrema kwa kupitisha dhahabu za Yassir Arafat/PLO airport Dar, tuliokuwa tunakaa jirani na Captain Aziz au Mkurugenzi Mkuu wa ATC, tulijua Mrema kaingilia deals za wakubwa kwa sababu tulipata habari nzima kutoka network ya mtaani.
Mambo mengine tuliweza kuyapata kwenye mitandao ya kibalozi kama ya Wamarekani kule karibu na baharini, tafrija za watoto wa kibalozi na mitandao ya watoto wa kimataifa kama ya International School of Tanganyika, wale watoto ilikuwa uki hang nao wana vitu vingi sana vyenye habari za nje kuanzia vitabu mpaka movies, documentaries etc. Watoto wa balozi za Indonesia na Romania walikuwa wanapenda sana kujuana na Watanzania. Ubalozi wa Romania ulisaidia sana shule ya msingi ya Oysterbay.
Speaking of movies and documentaries, Oysterbay Video Centre ilikuwa ni sehemu muhimu sana ya kuazima mikanda ya video yenye habari nyingi sana za nje hususan kwenye documentaries.
Washua waliporudi safari za kikazi pia walirudi na vitu vingi vyenye habari za nje. Kuanzia vitabu na majarida mpaka mikanda ya video.Ndugu zetu na majirani waliotoka Ulaya na Marekani pia wengi walikuwa wanarudi na mikanda ya video yenye mambo mengi ya nje. Mimi nilikuwa na majirani Wajapan walikuwa wananiambia mambo mengi kuhusu dunia ya nje ya Tanzania.
Mtaani kulikuwa na jamaa anasoma high school Hawaii kila akirudi ilikuwa tunabweda anakuja na mikanda ya video yenye mambo mengi sana ya nje, na yeye akija anataka kujua mambo mengi ya Bongo.
Mitandao ya maktaba kuanzia Tanganyika Library, British Council na United States Information Services (American Library, Peugeot House) ilisaidia sana. Nakumbuka nilikuwa napenda sana kwenda American Library kuangalia habari kwenye televisheni, hususan nikienda sana kumuangalia mtangazaji Peter Jennings wa televisheni ya Kimarekani ya ABC, hususan kwenye kipindi chake cha "ABC World News Tonight"
View attachment 3271389
RIP Peter Jennings.
Mambo ni mengi na umenikumbusha mbali.
Kwa sasa niishie hapa.