WATANZANIA ELITES: Kabla ya kuja kwa internet, mgogoro wa Middle East mlipataje habari zake??

Zamani watu walikuwa wanapata habari redioni kupitia station za masafa ya kati na mbali...

Umenikumbusha mbali sana, nimesikiliza DW, BBC , VOA , SABC, KBC nk kupitia radio za aina hii enzi za utoto wangu, Tangu nikiwa mdogo mpaka leo ni mdau mkubwa wa kusikiliza habari kwenye radio kuliko kutazama kwenye tv.
Enzi hizo masafa yanapatikana kwa SW na AM kabla ya ujio wa FM.Hakika tunetoka mbali
 
Wewe jamaa umeeleza uhalisia wa miaka hiyo
 

Wengine mahali tulipokuwa tunaishi huko vijijini, tulikuwa tunafunga mnara/antenna nje ya waya za aluminium na kuunga na waya wa copper hadi kwenye antenna ya radio ili tu usikose kusikiliza taarifa na chambuzi mbalimbali za idhaa za mashirika ya habari...
 
Uko sahihi kabisa mkuu, na tulikuwa tunatumia betri hadi zinakoroma kabisa, wakati mwingine tunazichaji juani.siku zinaenda kwa kasi sana
 
Wasomi wa zamani hao
Miaka ya nyuma kulikuwa na mwamba alikuwa anauza magazine pale samora avenue
Basi watu wanaenda pale wanapitia kusoma hizo magazine
Na magazine mengi yalikuwa yanatoka nje ya nchi
Kwa hyo watu walijitahidi kupata taarifa kadri kwa uwezo wao

Ova
 
Think tanks? I'm afraid you meant shit tanks! Unachanganya pure intelligence na wealth acquisition. Wala rushwa, wasaliti, wanyonyaji, mafisadi, na wafukia vibunda vya pesa ardhini ndio utawakuta kule. Kujibu swali lako, ukiwa na pesa utapata chochote unachokitaka.
 
Salute kwako umepita humo humoo
 

Umemaliza juzi ndo shida! Na akili huna
 
Mzee Kiranga uko deep kinyama.
 
Mimi kwenye utoto wangu nadhani nimesikiliza KBC ya Kenya kuliko radio nyinngine yoyote. Maeneo mengi ya Mkoa wa Arusha tulikuwa tunaipata KBC kiuhakika zaidi. Nakumbuka tukio la watu kufukiwa wakiwa wazima kwenye mgodi wa dhahabu huko Shinyanga liliripotiwa na KBC. Ulikuwa ni unyama wa hali ya juu. Nilikuwa mdogo ila nakumbuka mama alisema RTD hawatatangaza.
 
Mkuu, hili ndio tukio ambalo Mrema alikuwa DSO??
 
Mwalimu nyeyerere aliwafanya watu mazuzu sana yeye kwakwe ana TV na dishi alafu anawaambia kaoteshwa.Nasikia wanamuita mtakatifu
Siyo mwalimu Nyerere kama mtu ni mfumo wa ujamaa ndiyo unaataza uhuru wa habar
 
Mamako alikuwa na akili na maarifa mengi. Hata leo habar za maana hazitabgazwi TBC zaidi ya vipindi vya TUNAKELEZA
 
Home tulikua na TV tunaangalia TVZ na pia kulikua na Dish 📡 , Arab TV
 
Sawa sawa Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…