Watanzania hatuna shukrani Mungu atusamehe kwa huu ujinga tunaofanya

wasikuchanganye

1.wengi wanaopiga kelele kama Nape, Membe n.k ni wale ambao mrija ulikatwa


2. wako ambao wanakubali chuki kwa bluetooth tu


nje ya mitandao,JPM anaishi
 
Mimi ninachowashangaa nyie ni kwamba sasa kama pesa haijaibiwa si ndiyo vizuri ukaguzi ufanyike kama alivyosema Nape ili tujue mbivu na mbichi? Mbona mmepaniki? Kama amejenga hayo yote tuachie sasa tume huru ifanye ukaguzi kujua je ni kweli SGR imetumia this much? Ni kweli kwamba barabara zimetumia this much?
 
kulikua na mtu mwenye uwezo wa kuhoji kipind kile? au unaongea tu mkuu pasipo uhalisia...unajua ht kashfa za awamu ya nne zilijulikana sana kwasababu watu waliziongea bungeni na kwenye media bila hofu ndio maana wengi tukafahamu
 
home kwako.
Hebu tulia, tena kwenye hii special audit tumeamua kumuita mstaafu Prof Assad na yule mtangulizi wake Ludovick Utto ndiyo waongoze timu ya uchunguzi. Na zoezi zima litakuwa linarushwa mubashara TBC ana Azam TV ambapo miradi yoooteee itakaguliwa kujua value for money, tutakagua mpaka zile zilizokuwa zinagawanywa barabarani wakati wa ziara...
 
10 Nyerere + 10 Mwinyi + 10 Mkapa + 10 Kikwete + Samia = 5 Magufuli [emoji3]

This man was a Legend! Uthubutu mkubwa umefanyika katika awamu ya tano.Huyu mwamba ameweka standard ya uongozi/Urais unapaswa uweje.
Nyerere ni 26 jombaa...
 
Tukifanya uchunguzi ndiyo tutajua hizo Trilioni zilienda wapi na wapi.
 
Meli mpya kujengewa maziwa yote makubwa na kukarabati Meli nzee.
Kufufua reli zilizo kufa miaka 30 iliyopita etc
 
hio ndio shida ya wabongo sie, mtu katoa hoja badala waipinge hoja yake wanampinga yeye, wanaoleta hizo hoja za matumiz awamu iliopita wapingwe kwa hoja, km kila kitu kilikua shwari wanaogopa nn kupitiwa upya hizo hesabu?, waunde tume tu wampe assad achunguze loh
 
Unafki hautaisha bongo,huyu ni yule aliyepiga magoti kwa JPM(RIP) Na akasamehewa na kurudishwa kambini jana anatoka mate kumlaumu marehemu.
Naona support ndogo sana alipewa.
 

Ni miradi gani ya 20t imefanyika hapo nchini. Kipindi cha Magufuli data zilikuwa zinapikwa, na hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari, lakini sio kwamba hakukuwa na wizi. 1.5t ndio zilimtoa CAG baada ya serikali ya Magufuli kutaka kuficha wizi. Usidhani hatuna ufahamu wa mambo.
 
Yaani siku ya kufunguka akili ikifika sijui nani atakuwa mtoa nasaha, maana kila jambo huwa na kipindi chake as Bible says na Dolly Patton akaimba "TO EVERY THING .... THERE IS A SEASON ...

 
Balaa na janga kubwa sana kwa Watanzania na Mwenyezi Mungu akasikia vilio na maombi ya Watanzania wengi dhidi ya yule dhalimu mwendazake na akafanya kweli. Tumshukuru sana Mwenyezi Mungu. 🙏🏾

Alikuwa mwizi,muuaji na asiyependa kuona watu wakiishi vzr kwa haki!

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Hizo data zote unazoleta sasa ni feki.. maana marehemu Jiwe alikuwa bingwa wa kutunga data za uongo. Alitunga data za idadi ya samaki eti wapo Bilioni 6 baharini, kwenye maziwa na mito yote, alisema uchumi unakua kwa 7%, wakati ni uongo upo 4.8, alisema ATCL inatoa gawio la faida wakati ni uongo, alisema nchi Ina viwanda 68,000... yaani ni uongo uongo mtupu!! Hivyo hizo data zako zote ni takataka 🚮🚮🚮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…