kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Kwenye tukio la October 29, 2025 Walioua ni watanzania, waliouliwa ni watanzania na mali zilizoharibiwa ni mali za watanzania wote kwa ujumla wao. Mimi sioni haja ya maridhiano; maana huku mitaani tunakoishi simuoni mtu anaedai maridhiano.
Sisi watanzania wenye mali zilizoharibiwa na watanzania wenzetu tumekubali kuwa watanzania wenzetu waliuliwa na watanzania wenzetu tuliowakabidhi kazi ya ulinzi wa mali zetu kwasababu watanzania wenzetu waliharibu mali na miundombinu yetu kwa kushawishiwa na watu (watanzania na wageni) waliokuwa na agenda zao walizotaka kuzifanikiasha kwa kutumia watanzania wenzetu. Tumeshakubali kuwa watanzania wenzetu wameshakufa na mali zetu zimeshaharibika, wote tumepata funzo.
Dalili muhimu za kuonyesha kuwa tumeshakubaliana na hali ile ya Oct29 ni kama zifuatazo:
1. Watanzania bado wanaishi pamoja kwenye nyumba na mitaa bila kujali vyama, dini, waliokufa wala miundombinu na mali zilizoharibiwa.
2. Watanzania bado wanauza na kununua bidhaa bila kujali vyama, dini, kabila, mauaji wala mali zilizoharibiwa.
3. Watoto wetu bado wanasoma shule na vyuo vilevile kabla na baada ya tukio lile. hakuna aliyehamisha mtoto wake kwaajili hiyo.
4. Usafiri: Hata baada ya tukio lile Watanzania hawabagui vyombo vya usafiri vya kupanda. tunapanda bodaboda, bajaj, mabasi, maguta, treni wala ndege za kusafiria bila kujali anavimiliki nani.
5. kazini: Hata baada ya tukio lile watanzania bado wanafanyakazi ofisi moja, idara na taasisi moja bila kujali vyama na dini zetu
6. Msiba na maziko: Hata baada ya tukio lile watanzania wanazikana bila kujali vyama vya siana, mauaji wala uharibifu uliofanyika.
7. Michezo: Watanzania wanacheza na kushabikia michezo bila kujali kilichotokea Oct29.
8. Ibada: Wote bado tunasali palepale na vilevile tulivyokuwa tukisali kabla ya tukio
Kama hali majumbani, mitaani, sokoni, kwenye usafiri, kwenye ibada na mashuleni ni shwari Nani analazimisha maridhiano? Nani anataka maridhiano? nani atafaidika na maridhiano? Ni maridhiano kati ya nani na nani?
Sisi watanzania hatuhitaji maridhiano kwakuwa tumeshajua nini kimetokea na kwanini kilitokea, na mafunzo tumeyapata.
Kusalia majumbani kila yanapoitishwa maandamano mapya ni uthibitisho kuwa watanzania tumejifunza kitu kutokana na tukio lile. Hatuhitaji kukumbushwakumbushwa kila wakati, wenyewe tumeshaanza kuyasahau na maisha yanaendelea.
Tujikite zaidi kwenye kuzuia yasitokee kama yale tena huko mbeleni kwa kuiangalia nyumba yetu.