Watanzania hii ndio sababu ya kwanini tuliandika katiba mpya, mnamchosha rais na kero zenu kwenye misafara yake

Katiba Mpya Kenya imeongeza ufisadi, Ukabila, Njaa, Ukosefu wa kazi, Police Brutality,na Uchumi kushuka kutoka 8% hadi 4.5%
Hio ndio ukweli
 
Kwani GDP inahesabika pesa tu au pamoja na miundo mbinu ya nchi ?.
 
Ndio maana ukaambiwa hata kama nchi masikini ila Thamani yake uwezi kulinganisha na pesa ya nchi fulani maana thaman ya nchi haifanani na kiasichochote cha pesa yani mfano wake Roho ,huwezi ukathaminisha roho ya mwenzio Kwa kiwango fulani cha pesa utaona inakidhi sababu ya tamaa yako tu ila sio thamani yake hiyo ndio maana huyo mbulula mk 254 anaonekana pimbi kufananisha kiasi cha pesa eti Kwa Tz ,ke, Ug , Ethiopia , sijui Sudan mbili du kweli njaa ni sawa na uchizi sio bure atakua ana njaa huyu ,hivi mtu kama huyu anawaza kweli kabla ya kuongea au anaropoka tu maana unaposema nchi ni vitu vyote vilivyomo humo ndani pamoja na watu, mito , maziwa , bahari ,milima , misitu , mbuga , madini sasa unaposema madini usihesabu Kwa nini kwani hayapo
 
MK254,

Sioni sababu ya katiba mpya zaidi ya kutia hasara pesa za serikali tu katika kuiandaa maana katiba yenu haisaidii wananchi inasaidia polisi ktk kuuwa raia bila ya hofu maana Kwa kitu cha kipuuzi tu kama korona wameuawa watu zaidi ya 15 na hakuna chochote kilichofanyika kama kafa shogo tu.
 
Magufuli anafanya maigizo hao wote wamekua wamepangwa na kuandaliwa
 
Magufuli anafanya maigizo hao wote wamekua wamepangwa na kuandaliwa
Hata mbowe kwani alishambuliwa kweli c maigizo tu unazani muheshimiwa kama yule aseme ameanguka kwenye ngazi akiwa tungi unazani Jambo jepesi tena cha zaidi alikua na kicheche huku mke kamuacha nyumbani !! , Kuigiza mda mwengine kweli inawezekana kua ipo ingawa hatuna uhakika
 

Mimi nimemjibu kuhusu kununua nchi na wala sio hizo ulizoniorodhoshea.
 
Mbona umechanganya sn madesa mkuu.....kwani ww ndo unafanya maandalizi ya hizi sanaa za mkuu?
 
Mbona umechanganya sn madesa mkuu. Kwani wewe ndo unafanya maandalizi ya hizi sanaa za mkuu?
C tunazungumzia kupanga, hivi apange ili iweje kama kukubalika magufuli kashakubalika tu uraiani hana mpinzani sasa mpaka apange watu kutaka nini?
 
C tunazungumzia kupanga, hivi apange ili iweje kama kukubalika magufuli kashakubalika tu uraiani hana mpinzani sasa mpaka apange watu kutaka nini?
Kakubalika uraiani unamaanisha wapi mkuu.

WAKULIMA WANALIA
WAFANYAKAZI WANALIA SN
WAFANYABIASHARA WANALIA VIBAYA
WANAFUNZI NDIO USISEME

Uchaguzi ukiwa huru na haki hamna hata mmoja hapo juu atampa kura ndio maana hataki uchaguzi, hataki tumehuru, hataki katiba ya wananchi Ila yy anabadilisha hii mbovu iliyopo ili akivunja katiba asishitakiwe. Umewahi kuniuliza ni kwa nini?

Uraiani unemaanisha wapi mkuu
 

Hehehe Umeiweka vizuri sana, sijui kama hilo zwazwa litaelewa kitu.
 
Maneno ya chadema haya yanaonesha hisia tu sio uhalisia ,walimu wamelipwa kipindi chote cha korona Kenya wenye katiba mpya wameshindwa wanafunzi wanalia hiyo Kwa Imani yako labda ungefafanua wanalia wamefanyiwa kitu gani kibaya na Magufuli ambacho kilikua tofauti na utawala wa nyuma , sasa ukiwa tayar una chiki uwezi kuona uongoz kua bora hata kama bora miaka yote. Yani unachokizungumza wewe ni propaganda hauna tofauti na walibya. Hivi unajua kazi ya Rais
 
Mfanya biashara gani kafirisika kipindi hiki?
 
Hakuna mahali nimelinganisha thamani ya nchi fulani na pesa ya nchi fulani. Rudia kusoma post yangu pole pole ili uielewe. Kimsingi,huwezi kuringa na madini ambayo hujayachimba. Mali ni ile ambayo umeishika mkononi au ambayo umeichimba. Kama hujaichimba basi hiyo ni kama kuhesabu pesa ambayo bado hujapata. Pesa unahesabu tu ile ambayo umeipata. Kama huna technology na ujuzi wa kuchimba na kurefine dhahabu utaihesabu vipi kama sehemu ya utajiri? Na utaipea value ipi? Utasema sisi tuna dhahabu kiasi cha $30 billion? Hata ukisema hivyo kumbuka bado hujaichimba kwa hivyo huwezi kuirecord kwenye vitabu.
 
Umemsapoti mk 254 Kwa upumbavu aliouandika kua Uswisi uchumi wake unaweza kununua nchi ya Kenya, Tanzania, Uganda na Ethiopia na chenji ikabaki sasa huu si uwendawazimu huu
 
Mkuu acha kurukaruka kitembezembe.
Alafu kuhusu Libya nyie vijana wa lumumba mnaojua kukaa ofisini nyuma ya kibodi mnahitaji kujuzwa zaidi.

Ujue kua maendeleo ya wananchi sio hisani ni haki kwa sababu wananchi wanalipa kodi kwa hiyo ni lazima wapate maendeleo wanayoyataka rais ameajiriwa anapipwa mshahara mkubwa na kupewa raslimali zote ili kusimamia na kuleta maendeleo..MAENDELEO YA WATU maana maendeleo ya vitu hata wakoloni walileta na hawajawahi kujisifia.

Kwa kifupi tu. Walibya walikuja kugundua kuwa kumbe wanachopata ni 15% tu Cha kile wanachostahili na ikabainika namna Gadaffi anavotapanya mali za Wana Libya akijilimbikizia mali (uwekezaji binafsi na pesa nyingi) nje ya nji. Hujui kua walifreeze accounts na mali zake nyingi sn.

Ndio maana ccm haitakiwi kwa sababu watz hawapati hata 1% ya kile wanachostahili kupata.

WANANCHI WANA WAJIBU WA KULIPA KODI LKN WANA HAKI YA KUPATA MAENDELEO HUKU VIONGOZI WANAWAJIBU KUSIMAMIA RASLIMALI KUHAKIKISHA MAENDELEO YA WATU YANAPATIKAKA
 
Kakubalika uraiani unamaanisha wapi mkuu.

WAKULIMA WANALIA
WAFANYAKAZI WANALIA SN
WAFANYABIASHARA WANALIA VIBAYA
WANAFUNZI NDIO USISEME

Uchaguzi ukiwa huru na haki hamna hata mmoja hapo juu atampa kura ndio maana hataki uchaguzi, hataki tumehuru, hataki katiba ya wananchi Ila yy anabadilisha hii mbovu iliyopo ili akivunja katiba asishitakiwe. Umewahi kuniuliza ni kwa nini?

Uraiani unemaanisha wapi mkuu
 
Umemsapoti mk 254 Kwa upumbavu aliouandika kua Uswisi uchumi wake unaweza kununua nchi ya Kenya, Tanzania, Uganda na Ethiopia na chenji ikabaki sasa huu si uwendawazimu huu
Nionyeshe ni wapi nimesema hivyo. Mimi tatizo langu ni huyo wazimu Naton Jr kuhesabu madini yaliyo ardhini kama sehemu ya utajiri. Chimba madini kwanza kisha uihesabu. Kama ni kweli Naton anavyosema basi DR Congo ingekuwa nchi tajiri zaidi duniani. Kamwe huwezi hesabu kuku kabla mayai hayajaanguliwa.
 
Katiba gani ambayo polisi wanau raia kila siku?katiba gani ambayo mmeshindwa kumaliza ukabila?katiba gani imeshindwa kutatua swala la njaa? Moja ya kazi ya Rais ni kutatua matatizo ya wananchi,anapokuwa anasikiliza wananchi,japo sio wote,anapata hali halisi ya mwananchi,pia Rais wetu hayupo ikulu kuwasikiliza wazungu na wala rushwa kama ilivyo huko kwenu.Uhuru hujitokeza kupiga picha na wananchi pale anapotafuta kura.Alafu ss sio,wa "copying"and "pasting" Tuna utaratibu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…