Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Kama china anataka kuifanya Tanzania a strategic investment area kwa ajili ya maslahi yake ya kibiashara kwenye eneo la afrika haiwezi kuwa kwa ujanja ujanja, lazima hiyo mikataba iwekwe wazi ambayo ina reflect interest na maslahi yetu kama nchi kwenye huo uwekezaji, full stop.
Sgr umeiweka wazi? Ndege je? Mkataba gani Tzn hii ccm wamewah weka wazi?
 
Hayo maneno wewe umeyatoa wapi? Ardhi bure itakuwa na mipaka gani? Hiyo ardhi ataipeleka China?

Hivyo viwanda na Bandari zitajengwa China au Tzn? Propaganda za kijinga alizowalisha yule mharibifu

Nani kasema hayo? Au ndo unamrefer yule jamaa mwongo?
Pambafff! kama mmekula pesa za mchina mtazitapika hiyo project haifanyiki....
 
Mkuu, labda kama utakuwa hukunielewa kabisa. Tambua kuwa:

1. Ninatambua kuwa kulikuwa mradi wa bandari ya Bagamoyo ulioasisiwa na JK awamu #4.
2. Ninatambua pia kuwa mradi huo ulipigwa munda "unceremoniously" na JPM awamu #5.
3. Mimi na wewe hatujui contents za mradi ule.
4. Ninakusoma wewe vyema kwa nini mradi ulipigwa chini.
5. Sizikatai sababu ulizozitoa, ila tu ninakwenda mbele kukuunga mkono kwa mshangao kuwa, kwamba inawezekana je?

View attachment 1832409

Kwamba kwa mujibu wako JPM aliamua kuwakomoa wachina kwa kuuzima mradi wote kwa sababu tu hawakuwa wamevutiwa na mradi wa SGR?

Hebu zirejelee kuona kama sababu hizo siyo za kitoto kabisa?!
Hata ningekuwa mimi siwezi maana Road and Belt yao ilitaka wafanywe hiyo miradi yote wao kwa pamoja ndio maana JK alimalizana nao ila Magu kavinja
 
Kubwa jinga ktk ubora wako!!eti ufadhiri , miaka hii kuna nchi inaweza kufadhiri mradi wa matrilion?na kwani inakuwaje donor cantri kulilia ufadhiri wakati unajiweza hahaa!!mataga masalia bwana!!yaani kwa akili yako hii inaonekana hata hujui chochote kitu kwenye mradi huo wa bandari!!Hadi sasa hujaamini kuwa hiyo bandari itajengwa?!pole sana !!nadhani shule mnafungua wiki ijayo sio mbali!!eti china ina eneo kubwa sana kwanini wasijenge huko?daaaa, mwendazake alifanikiwa sana kuwa washbrain !!
Mbona wao na baba zao hawatoi ufashili? 😆😆😆😆
 
Wanatuambia Tanzania itapata kodi kwenye bandari ya wachina bagamoyo, lakini hawatuambii likizo ya kutokulipa kodi
/tax holiday ni miaka mingapi? Ajira za bandarini ni za makuli!! wabeba mizigo! Sehemu zote nyeti watatajaa wachina maana huwezi kumpangia mtu na mali yake!!

Akikuweka mfukoni day 1 huwezi kuwa mjanja day 2!! Zaidi ya hapo blackmail itafanya kazi!! Watakutishia kukufichua!! Angalia huko Sri Lanka, wachina wamebeba bandari na ardhi inayozunguka na hawatalipa kodi kwa miaka 32!! Hapa keetu itakuwa zaidi ya hapo!! Sri Lanka wanalia lakini hawana jinsi!

On Friday Sri Lanka's parliament approved wide-ranging tax concessions for the port deal, including a tax holiday of up to 32 years for the Chinese firm, that opposition parties objected to.
Usiwe mjinga wewe na kutoa mfano wa kijinga ,Slilanka na Bagamoyo ni project mbili tofauti,hapa ni wabia wa pande 3 sasa kwani wabia wakikubaliana ku bear risks kuna shida gani?

Afu hayo maneno ya kutunga umetoa wapi au ni kwa yule jizi mwendazake? 😆😆
 
Shida moja kwenye haya mambo, hata mama akiwategemea wataalamu wake kumshauri, nao wataangalia msimamo wa mama kwanza, yaani hatutapata USHAURI ule wa kitaalamu. Mwendazake aliishatwambia kuhusu masharti yale ya bandari ya Bagamoyo, wengi wanaompinga hawasemi kama alicho twambia ni uongo au laa, wanampinga kwa chuki tu.

Ni vema tukajua in and out, kama yale aliyasema mwendazake ni ya kweli au uongo, kama ni ya kweli, kwanini tukimbilie Bagamoyo ilihali Tanga, Mtwara pia zipo? Kwanini tusi suspend operations za bandari moja wapo halafu tukafanya ukarabati wa KUFA mtu huko then tuendelee kuliko kuanzisha kitu kipya ilihali kuna vya kuendeleza? Unless, tuambiwe mwendazake alitudanganya
Wewe na akili zako mbovu unaweza muamini dikteta uchwara? Yaani mtu mwongo na Mzee wa propaganda za kijinga kwa ajili ya maslahi yake ndio reference? Mbona unakamatiwa akili kirahisi Sana?

Mzee wa Korona ya kwenye mapapai mbona hakuweka hadharani japo vipengele kadhaa tujisomee akaishia kupayuka tuu?
 
Nguvu ya umma bado ni kubwa, watu wanaweza kuweka pressure uwekwe wazi mkataba.

Tusirudie mambi ya mradi wa gesi (90% inaenda kwa wawekezeji), IPTL na Tanesco scandal, mikataba hovyo ya madini na Acacia, Meremeta, radar mbovu.

Imetugharimu na inaendelea kutugharimu matrillioni ya shilingi.
Kwenye Twiga ya makinikia ya Magu asilimia ni ngapi?

Hata ufanyaje hakuna mwekezaji mjinga atakubali eti atafute yeye gas,aweke pesa na teknolojia,soko anajua yeye afu wewe from no where uje kukurupuka eti utake 50/50 hii haiwezekani kokote kule Duniani.

Miaka yote toka wazungu wako kimya hakuna Nchi imefanya ila wakija wenye mtaji na teknolojia unataka mgawane hii haipo .

Hata kwenye Bagamoyo haitoshi kusema eti tuna bandari/ardhi sasa ikikaa hivyo hivyo bila kuendelezwa inakusaidia nini? Si bora wanaoweza kuendeleza waje,wakirudisha pesa zao mali inabakia ya Tzn la sivyo na wewe weka mzigo mezani
 
Sisi tuna bahati moja. Kuna nchi nyingine zimefanya makosa, zikajikuta zime-surrender vipande vya ardhi China hivyo tumeshajua hawa jamaa siyo watu wazuri. Lakini ajabu naona mama Samia ndiyo yuko mbele kuwakumbatia. Tutakuja kujuta sana.
Tumeshayasoma sana ya Sri-Lanka, Zamba, Kenya... Huyu mama anatunyima furaha na confidence kuwa taifa letu na mali zake zipo salama... Tumekosa furaha, tunahisi kuuzwa... Wakati anaelekea kweye hayo maamuzi, japo atuhakikishie na kutupa matumaini kuwa Tanganyika yetu ipo salama mikononi mwake
 
Hata ningekuwa mimi siwezi maana Road and Belt yao ilitaka wafanywe hiyo miradi yote wao kwa pamoja ndio maana JK alimalizana nao ila Magu kavinja
Sikio la kufa huwa alisikii dawa

Kwenye proposal ya port na industrial hub ya Bagamoyo serikali ya Magufuli aikuwa na shida na miradi mingine itayojengwa hapo
zaidi ya bandari tu.

Kwanza serikali walikuwa awataki ubia kwenye ivyo viwanda vingine wala kujua vitaendeshwa vipi kila kitu wafanye wenyewe na kumiliki wao wenyewe wachina 100% subject to adhering to Tanzania investment laws ata kesho wanaweza anza huo uwekezaji mwingine.

Magufuli yeye alikuwa interested na aspect za port peke yake na umiliki wake hapo ndio kwenye shida.

Wachina ndio wanaolazimisha hiyo miradi mingine (industrial park) iwe sehemu ya makubaliano ya bandari na wapewe concessions ambazo wawekezaji wengine awapewi katika uwekezaji wa viwanda vya kawaida.

Sasa hilo swala on economic side itafanyaa bidhaa zinazo zalishwa hapo kuwa cheap kushinda washindani zao ndani ya EAC maana wanamisamaha ya kodi, maji na umeme karibu bure ndio vitu wanavyotaka wapewe na kupunguza production costs zao.

In other words wanauza gunia ambalo 20% mchele na 80% mahindi kwa bei ya mchele. Serikali aitaki kununua gunia lote wanachotaka ni huo mchele 20% hiyo 80% wakauze kwengine.

So kama mnadhani industrial park itachochea uchumi wachina hawajuzuiwa kuanza, isipokuwa wao ndio hawataki kutofautisha huo uwekezaji na bandari; wanataka vyote vipewe same preferential treatments.

Nyie watu muwe mnasikiliza hoja za watu wa serikali walichokuwa wanapingana nacho kwenye huo mkataba ni kitu gani haswa; kuliko kuokoteza uongo wa mtu kama Zitto.
 
Tumeshayasoma sana ya Sri-Lanka, Zamba, Kenya... Huyu mama anatunyima furaha na confidence kuwa taifa letu na mali zake zipo salama... Tumekosa furaha, tunahisi kuuzwa... Wakati anaelekea kweye hayo maamuzi, japo atuhakikishie na kutupa matumaini kuwa Tanganyika yetu ipo salama mikononi mwake
Kuna watu wanajiona wajanja kwenye hili kisa wametanguliza maslahi yao, hii inaweza kuleta political crisis ambayo haijawahi kushuhudiwa......hapo mchina amedinda na mkataba wake wa miaka 99 hasikii la mtu.
 
Sikio la kufa huwa alisikii dawa

Kwenye proposal ya port na industrial hub ya Bagamoyo serikali ya Magufuli aikuwa na shida na miradi mingine itayojengwa hapo.

Kwanza serikali walikuwa awataki ubia kwenye ivyo viwanda wala kujua vitaendeshwa vipi kila kitu wafanye wenyewe na kumiliki wao wenyewe 100% subject to adhering to Tanzania investment laws ata kesho wanaweza anza huo uwekezaji.

Magufuli yeye alikuwa interested na aspect za port peke yake na umiliki wake hapo ndio kwenye shida.

Wachina ndio wanaolazimisha hiyo miradi mingine iwe sehemu ya makubaliano ya bandari na wapewe concessions ambazo wawekezaji wengine wapewe.

In other words wanauza gunia ambalo 20% mchele na 80% mahindi kwa bei ya mchele. Serikali aitaki kununua gunia lote wanachotaka ni huo mchele 20% hiyo 80% wakauze kwengine.

So kama sijui kama industrial hub itachochea uchumi wachina hawajuzuiwa kuanza, isipokuwa hawataki kutofautisha huo uwekezaji na bandari.

Nyie watu muwe mnasikiliza hoja za watu wa serikali walichokuwa wanapingana nacho kwenye huo mkataba ni kitu gani haswa; kuliko kuokoteza uongo wa mtu kama Zitto.
Kumbuka huu mradi ni PPP na utaratibu wa PPP unajulikana,mambo mengine yako negotoatable na nimesoma somewhere kwamba Wachina wako tayari kwa lease ya miaka 33 na mambo mengine ya kikodi na yatajadiliwa yawekewe sawa.Ule uzushi wa eti ni marufuku kuendeleza bandari zingine ni upuuzi tuu wa Mwendazake

Sioni shida hapo so long as mradi ni PPP na una multiplayer effects kubwa kuliko kuangalia kwa jicho la kisiasa badala ya kiuchumi
 
Wewe ni mjinga kabisa. Wewe unadhani kuwapa watu lango la kuingia nyumbani kwako walijenge halafu walimiki na kuliendesha ndiyo bora? Si bora hata hao walichokuwa mkopo? Wewe unafikiri mchina ni mjinga awekeze matrilioni ya fedha wakati anaona kutakuwa na hasara?
Mkuu 'macho_mdiliko'
Nami nilitaka kuanzisha mada juu ya hii 'project' ya Bagamoyo, lakini zimekuwepo nyingi kiasi kwamba huenda mada nitakayoanzisha itaishia kwenye kuunganishwa na hizi ndefu na kuishia bila kusomwa.

Ni dhahiri, mradi huu una makundi yenye maslahi wanaouchochea kuupa nguvu, hasa hawa wa upande wa wachina, bila kujali maslahi ya Tanzania.

Mimi ningependa kuuliza na kupata maoni ya wachangiaji juu ya ugumu wa mradi huu kuufanya uwe wetu halafu tuwakaribishe wawekezaji wafanye wanavyotaka kuwekeza kwenye mradi wetu.

Hapo majirani Kenya na mradi wao wa Lamu wameuanzisha wenyewe, baada ya kuona kwamba wakitegemea wawekezaji ndio wauanzishe, huenda mradi huo usiwepo kabisa.

Kenya wamejenga Ghati tatu sasa; moja iko tayari na mbili hazipo mbali. Bandari inaweza kuanza kufanya kazi, na atakayetaka kwenda kuwekeza hapo kwa kujenga ghati nyingine, hadi zitimie 32, anakaribishwa.

Bagamoyo, kwa hakika ina sifa tofauti zaidi ya Lamu, sifa zinazovutia kwa uwekezaji; kama hali ya usalama, na ukaribu zaidi na nchi zitakazotumia bandari hiyo.

Je, sisi hatuna uwezo, hata kama utakuwa ni kukopa, kuanza ujenzi wa ghati chache hapo Bagamoyo, na wakati huo huo tukiiuza kwa wawekezaji, hata hao wachina waje kuwekeza, kama wanavyotaka kuwekeza sasa?

Mpangilio huu utakuwa na masharti tofauti na haya tunayokabiliana nayo wakati huu na huyu mwekezaji anayetaka bandari iwe ya kwake.

Nadhani katika hoja zinazotolewa kwenye mijadala hapa ukumbini, kuna mambo pia watu wanayasahau kwamba yapo.
Kwa mfano: Mchina hawekezi kwa asili mia katika mradi wa Bagamoyo, yeye anazo asili mia kadhaa atakazowekeza kwenye mradi huo, na yeye atatafuta wawekezaji wengine waje wawekeze chini ya himaya yake.

Mchina hatoi hiyo $30 bilioni, siku tutakayomkubalia kuwekeza hapo. Mu-Oman yeye za kwake zinajulikana ni asili mia kumi za mradi unaopangwa hapo, na hata sisi Tanzania tukisema tuwekeze zaidi ya hicho kiasi cha mchango wa ardhi kitakachohesabika kuwa ndizo hisa zetu katika uwekezaji, hilo pia linawezekana (sijaona popote linapokatazwa). Hata matajiri wetu hapa, akina Bakhresa, huenda watajitosa kuwekeza wakitaka, lakini kwa kwa hali ya sasa, uwekezaji huo utakuwa ni chini ya himaya ya mchina na siyo yetu (Tanzania).

Ninachoomba kujuwa, kuna tatizo lipi la kuufanya mradi huo uwe wetu? Bila shaka majibu mengi yatahusu hilo la uwezo wetu kujenga hizo ghati za mwanzo, lakini mbona Kenya wameweza?

Wengine watahoji tutawapataje wawekezaji ambao bado hawajaonekana Lamu - ukweli hapa ni kwamba Bagamoyo inauzika sana, ndiyo maana wachina hawabanduki kwenye mradi huo, vinginevyo ungekwishasikia wamekimbilia Lamu au kwingine.

Kama hatutaweza kupata mkataba wenye maslahi stahiki kwa nchi yetu, napendekeza, tuwe jasiri, tuuanzishe huu mradi wenyewe, halafu , kama tunavyofanya juhudi za kuwakaribisha wawekezaji nchini mwetu kwenye sekta hizi nyingine, tuweke jitihada kubwa za kutafuta wawekezaji kokote watakakopatikana, waje wawekeze kwenye eneo hilo kama ilivyopangiliwa katika uwekezaji wa sasa.
 
Sikio la kufa huwa alisikii dawa

Kwenye proposal ya port na industrial hub ya Bagamoyo serikali ya Magufuli aikuwa na shida na miradi mingine itayojengwa hapo
zaidi ya bandari tu.

Kwanza serikali walikuwa awataki ubia kwenye ivyo viwanda vingine wala kujua vitaendeshwa vipi kila kitu wafanye wenyewe na kumiliki wao wenyewe wachina 100% subject to adhering to Tanzania investment laws ata kesho wanaweza anza huo uwekezaji mwingine.

Magufuli yeye alikuwa interested na aspect za port peke yake na umiliki wake hapo ndio kwenye shida.

Wachina ndio wanaolazimisha hiyo miradi mingine (industrial park) iwe sehemu ya makubaliano ya bandari na wapewe concessions ambazo wawekezaji wengine awapewi.

In other words wanauza gunia ambalo 20% mchele na 80% mahindi kwa bei ya mchele. Serikali aitaki kununua gunia lote wanachotaka ni huo mchele 20% hiyo 80% wakauze kwengine.

So kama mnadhani industrial park itachochea uchumi wachina hawajuzuiwa kuanza, isipokuwa wao ndio hawataki kutofautisha huo uwekezaji na bandari.

Nyie watu muwe mnasikiliza hoja za watu wa serikali walichokuwa wanapingana nacho kwenye huo mkataba ni kitu gani haswa; kuliko kuokoteza uongo wa mtu kama Zitto.
China angeonyesha mfano kwa kuiruhusu marekani ijenge na kuendesha bandari nchini kwao bila wao kujua kinachoendelea, hapo tungejua china kakomaa kweli kwenye international diplomacy....
 
Kumbuka huu mradi ni PPP na utaratibu wa PPP unajulikana,mambo mengine yako negotoatable na nimesoma somewhere kwamba Wachina wako tayari kwa lease ya miaka 33 na mambo mengine ya kikodi na yatajadiliwa yawekewe sawa.Ule uzushi wa eti ni marufuku kuendeleza bandari zingine ni upuuzi tuu wa Mwendazake

Sioni shida hapo so long as mradi ni PPP na una multiplayer effects kubwa kuliko kuangalia kwa jicho la kisiasa badala ya kiuchumi
Hiyo ni sehemu ya bandari tu

Kwenye viwanda serikali wala hawajawapa masharti hayo wawekeze tu kama wawekezaji wengine ata kesho.

Wao ndio hawataki kwa sababu wanataka raia wao wataoenda kufanya kazi hizo sehemu wasisumbuliwe kupata vibali vya kazi, viwanda vipewe maji na umeme kwa bei nafuu na tax holidays.

Sasa ukishafanya ivyo na machine zake za kuzalishia ajalipia kodi halafu za kisasa zinauwezo wa kuzalisha a lot with minimal manpower hata huyo Bakhresa hatoweza shindana nae kwenye low prices.

Muwe mnafikiria vitu mnavyotetea Magufuli is dead , Tanzania lives on. Chuki zenu kwakwe zisiwape upofu what is at stake kwenye huu mradi nchi ikikubali kila takwa la mchina.
 
Hata ningekuwa mimi siwezi maana Road and Belt yao ilitaka wafanywe hiyo miradi yote wao kwa pamoja ndio maana JK alimalizana nao ila Magu kavinja

Magu alidhani ana uwezo wa kuwaburuza wengine wote kama ambavyo angetaka.

Dalili za malezi mabovu katika makuzi yake.
 
China angeonyesha mfano kwa kuiruhusu marekani ijenge na kuendesha bandari nchini kwao bila wao kujua kinachoendelea, hapo tungejua china kakomaa kweli kwenye international diplomacy....
Swala la bandari ya Bagamoyo hilo halina ubishi lazima ijengwe; Dar aiwezi kuwa expanded anymore it’s reaching its saturation point.

So either Bagamoyo
anajenga mchina au Tanzania; upande wa serikali wao walilenga kulinda mapato yao yasipotee vile.

Icho ndio ilichokuwa inataka serikali iliyopita win win situation.
 
Back
Top Bottom