Kwenye Twiga ya makinikia ya Magu asilimia ni ngapi?
Hata ufanyaje hakuna mwekezaji mjinga atakubali eti atafute yeye gas,aweke pesa na teknolojia,soko anajua yeye afu wewe from no where uje kukurupuka eti utake 50/50 hii haiwezekani kokote kule Duniani.
Miaka yote toka wazungu wako kimya hakuna Nchi imefanya ila wakija wenye mtaji na teknolojia unataka mgawane hii haipo .
Hata kwenye Bagamoyo haitoshi kusema eti tuna bandari/ardhi sasa ikikaa hivyo hivyo bila kuendelezwa inakusaidia nini? Si bora wanaoweza kuendeleza waje,wakirudisha pesa zao mali inabakia ya Tzn la sivyo na wewe weka mzigo mezani
Twiga Tanzania ina 16%, Barrick 84%. Tunagawana 50/50 of economics benefits after Barrick recoupment of capital investments. We have seats at the top table (Board level) kuangalia, kusimamia nakujua kila kinachoendelea. So far wameshatulipa kodi and royalties over $300 millions and on top of that millions in dividends.
Magu aliunda tume kusimamia na ku-negotiate kwa maslahi ya Tanzania. Mchango wetu hapo ni Ardhi yetu makinikia yetu. Na aliweka wazi makubaliano yao.
Ardhi yetu, strategic location (ndio litakuwa lango kufikia soko letu TZ na SADC, EAC). Pia kupitia hapo export hadi Dunia nzima, tax holiday, concession kwenye bill za maji, umeme etc, unafikiri hivi ni vitu kidogo.
Kuna issue ya ushindani, fair competition na viwanda vingine Tanzania.
Bidhaa zinaweza kuwa zinaletwa kutoka China zikaingizwa bila kulipiwa kodi, wakisema wamezalisha hapo kwenye Economic Zone utawapinga vipi wakati huna mamlaka ya kusimamia, kujua vitu vyote vinavyoingia na kutoka na vinavyozalishwa hapo.
Madawa ya kulevya yakiletwa kupitia hiyo bandari, pembe za ndovu na madini yakipitishwa hapo, wanyama wakitoroshwa utajuaje wakati huna mamlaka ya usimamizi.
Kwanini kuna kigugumizi kusema tutaweka vitu vyote wazi.
Mkataba uliokataliwa uwekwe wazi, unaopendekezwa uwekwe wazi, ujadiliwe.
Kuna maswali mengi Usalama wa Taifa na mali zake na watu wake, mkopo unalipajwe, tukishindwa kulipa wanachukua nini? (There is free Lunch, hatuna Shangazi wala mjomba).
Tunahakikishaje kutakuwa na fair competition na viwanda vingine vya ndani, Bandari nyingine za TZ (Dar, Tanga, Mtwara).
Maswali ni mengi sana, majibu hatuyaoni.
Ile tume iliyojadiliana na Barrick, labda wangepewa hii kazi kujadiliana na hawa. Walifanya kazi nzuri sana na income tulipata kutoka day one. Walikuwa wanatu -update everytime what wamefikia kwenye majadiliano. Maboss wao wote walikuja hapa kujadiliana.
Ni sisi ndio tunalikuwa tunaweka masharti sio kupangiwa na wengine masharti ya ajabu.