Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Eti rais Mnangagwa aliweza kutafsiri neno moja tu kwenye hotuba yote ya Jiwe. Mwaka(year), alafu aliitafsiri kwa kiingereza kama season(msimu). [emoji38][emoji38][emoji38] Sasa hotuba yote ndefu hivyo ilikuwa ya nini kama mzee alikuwa haeleweki na yeyote? Wabongo buana!
A catalyst is a substance that alters the rate of chemical reaction but remains unchanged (chemically) at the end of reaction. Well, as an African leader he altered the norms by answering questions in Swahili.I didn’t know that he was ze catalyst even in Zimbabwe.
alafu eti jamaa kaandika thesis yake ya phd kwa hicho kingereza aischoweza kukizungumza, jamani eeh waswahili...how can you write in a language you cannot speak? ama alishushiwa hiyo thesis apo uni of dar kama mtume s.a.w (pbuh) akitoka mecca to madina kwenye hijra!
Labda hukuwahi kusoma kemia, ila kama uliwahi kuisoma mpaka level ya juu utaelewa kuwa ni mambo ya ku balance equations na ku cheza na laws. Mda mwingi unatumia maneno kama dynamic equilibrium, disturbed conditions, electrochemical series, vapor pressure n.k. na katika mfumo wa elimu Tanzania mtu anaweza akaacha masomo ya kuandika insha (Historia) toka kidato cha tatu.Na eti alifanya PhD in Chemistry pale Dar slum University 😂😂
Mshukuru sana kwa niaba ya wakenya. Sasa subirini muone jinsi huu mchezo huchezwaJPM alifanya maksudi tu, ni mfanya biashara mzuri!
Lengo lake kubwa ilikua ni kuuza lugha ya Kishwahili na alifanikiwa, kote huko alikopita ameshapata order ya kupeleka waalimu wa kufundisha hii lugha pendwa....
Alters? Alter is to change, right?A catalyst is a substance that alters the rate of chemical reaction but remains unchanged (chemically) at the end of reaction. Well, as an African leader he altered the norms by answering questions in Swahili.
Labda hukuwahi kusoma kemia, ila kama uliwahi kuisoma mpaka level ya juu utaelewa kuwa ni mambo ya ku balance equations na ku cheza na laws. Mda mwingi unatumia maneno kama dynamic equilibrium, disturbed conditions, electrochemical series, vapor pressure n.k. na katika mfumo wa elimu Tanzania mtu anaweza akaacha masomo ya kuandika insha (Historia) toka kidato cha tatu.
Sasa wewe inakuhusu nini? Hivi Kenya matatizo yameisha hadi uwekeze muda wako wote kuwaza Nani anaongea Kiinfereza Tanzania?
Yes.Alters? Alter is to change, right?
InsaneKawaida huwa mnajiliwaza kwamba sio lazima mkijue kingereza maana hata rais wa China akija Afrika, yeye huongea Kichina, lakini mnasahau kwamba yeye huambatana na wakalimani, kuna hizi habari za rais wenu akiwa Zimbabwe, ambapo alihutubia waandishi wa habari kwa Kiswahili ila watu wakaambulia patupu maana hapakua na mkalimani, ikambidi rais wa Zimbabwe atafsiri kidogo alichokua anapatia patia.
Waandishi pia wakashindwa kuuliza maswali maana wao walitegemea waulize kwa kingereza na maswali yajibiwe kwenye hiyo hiyo lugha. Sasa bila mkalimani watu wakabaki bubu wote na kutazamana.
Hehehe ila kwa kweli kingereza huwa kinawatesa, lakini mikijipanga itaondoa aibu ndogo ndogo kama hizi, aajiriwe mkalimani ikulu ambaye atakua anatiririka ung'eng'e kila mnapowatembelea hao majirani zenu na kukumbana na waandishi wa habari, maana kusoma hotuba iliyoandikwa kwa kingereza ni jambo moja na rahisi (maana unaweza ukakesha chumbani ukirudiarudia kuisoma hadi uwe bora), ila kupambana na maswali ya waandishi wa habari, ni mziki unaotaka uwe umejiamini na umejiandaa kutema yai tena kwa miaka kadhaa.
--------------------------------------
By Idah Mhetu
SWAHILI speaking Tanzanian leader John Pombe Magufuli, on Wednesday turned President Emmerson Mnangagwa into a translator, after it emerged none among the aides at the State House function in Harare could do it except for the Zanu PF leader.
Magufuli was in Zimbabwe on a two-day State visit and in his final address to the media, spoke mainly in Swahili, the biggest language in East Africa forcing his host to help bemused local journalists with translation.
He was set to depart for home but was reportedly said to have extended his stay.
The Tanzanian leader was announcing his government had a maize surplus and was ready to help hunger stricken Zimbabwe.
After speaking exclusively in his native Swahili, Magufuli turned to the journalists present and said: “I know you will cut some of the words.”
Mnangagwa’s spokesperson George Charamba tried to translate but could only manage one word.
“I just heard ‘mwaka’ meaning season,” Charamba said before Mnangagwa, noticing the handicap among his countrymen, turned translator.
Earlier on Tuesday, at a banquet held at State house, Magufuli told the media that he could not find a translator for his speech hence would read his written speech which was in English.
Introducing him to the media, Mnangagwa jokingly said President Magufuli was ready for questions but only spoke Swahili.
“With me here is President Magufuli of the Republic of Tanzania, who came here by invitation reciprocating my visit to Tanzania. We have had discussions to promote, deepen and to consolidate relations, he is at your disposal if you want to ask questions but he speaks only Swahili,” Mnangagwa said.
Mnangagwa had asked Magufuli if he had a translator among his staffers to which the Tanzanian responded in the negative before carrying on.
Translating his first brief, Magufuli further said he came to Zimbabwe to cement bilateral relations between the two nations. He said the two leaders had agreed on several issues which included trade, tourism and infrastructure.
“I came here to cement bilateral relations between Zimbabwe and Tanzania. I am only a catalyst and I am confident that the talks between the two nations will continue,” he said resorting to Swahili before breaking into laughter.
During the liberation struggle Mnangagwa operated as a guerrilla in Tanzania were Zanu had several bases from which he probably learnt Swahili.
![]()
Magufuli turns Mnangagwa into a translator - NewZimbabwe.com
Spread This NewsBy Idah Mhetu SWAHILI speaking Tanzanian leader John Pombe Magufuli, on Wednesday turned President Emmerson Mnangagwa into a translator, after it emerged none among the aides at the State House function in Harare could do it except for the Zanu PF leader. Magufuli was in Zimbabwe...www.newzimbabwe.com
Nishakwambiaga, acha miraa, it is messing up your brain.Nimekuelewa boss, formular na chemical equations za phd thesis ya mzee alizisomea na kuziandika kwa kisukuma.
Kwa kweli Magu anatia aibu ingefaa kusema mapema kwamba naweza mudu maneno machache tu ya kingereza afu mengine awe na mkalimani badala ya kujifanya unajua unatuaibisha,sasa sijui huko kwa wazungu maana kuwaelewa tu wanapoongea kwa ile rafudhi yao ni shidaI didn’t know that he was ze catalyst even in Zimbabwe.
Kamdanganye Bibi yako mkuu,huku Tzn familia zenye vipato wanapeleka watoto wao shule zinazofundisha kwa kiingereza kuanzia nursury hadi secondary tena usikute na wewe wanao wako huko hakuna asiyependa kiingerezaSijawahi kuona watu washamba na limbukeni duniani kama Wakenya! Yaani ni Wakenya pekee duniani ndio ambao wanaonea fahari "kuifahamu" lugha ya mkoloni wao aliyewatandika bakora na kuua mababu zao kwa miaka kadhaa!! Ajabu, hata Waganda ambao wapo vizuri kwenye Kiingereza kuliko Wakenya; ni nadra sana kuwakuta wakionea fahari kukifahamu Kiingereza zaidi ya lugha zao za asili kama vile Kiganda! Na ukweli ni kwamba, Wakenya mpo vizuri kwenye lugha zenu za asili kuliko Kiingerza, na ndio maana ukitoka nje ya miji mikubwa, utaeleweka zaidi kama unajua lugha za asili, au angalau Kiswahili kuliko Kiingereza! Lakini ushamba na ulimbukeni unaotokana na kuaminishwa kwamba Mzungu ndo kila kitu ndo maana haishangazi kuwaona kila wakati mkionea fahari lugha ambayo hata hivyo, hamjai-master!
Huku Tanzania, watu aina yenu walikuwepo ambao ukikutana nao, watakuambia "nimesoma la nane la Mwingereza" na wakati wote, ili kujaribu kuonesha ni namna gani waliosoma "la nane la Mwingereza" walikuwa bora, basi atataka muongee Kiingereza! Kwa bahati mbaya, wengi wao ama wameshakufa au kwa sasa ni wazee sana kuweka kukutana nao mitaani!! Inahuzunisha kuona kuna kizazi kipya cha Waafrika lakini bado wanawaza sawa na mababu zetu zetu waliozaliwa enzi ya Mjerumani!!!
Hivi unaelewa Kiswahili wewe?! Hao wanaopeleka shule za Kiingereza ni imani yao tu kwamba hizo shule zinatoa elimu mzuri, ingawaje wapo pia washamba miongoni mwao wanaodhani Kiingereza ndio elimu mzuri! Kuwa na uwezo wa kifedha hakumfanyi mtu kutokuwa mshamba na ulimbukeni! Wengine ushamba ndo kipaji chao cha kuzaliwa! Lakini pia wapo wenye uwezo lakini sio washamba na limbukeni na ndio maana unakuta wana-opt kuwapeleka watoto shule kama Feza, ambako mtaala wao ni huu wa akina Kayumba, na dogo akitoka hapo yupo fit kuliko akina nyie mnaoabudu lugha ya mkoloni!Kamdanganye Bibi yako mkuu,huku Tzn familia zenye vipato wanapeleka watoto wao shule zinazofundisha kwa kiingereza kuanzia nursury hadi secondary tena usikute na wewe wanao wako huko hakuna asiyependa kiingereza
Kingereza cha kuongea ndio kinasumbua watz wengi kwa vile hakuna mazingira ya kupractise kuongea,na ndio lugha rasmi ya kazi za maofisini
Kiswahili to the world [emoji7][emoji7][emoji7]Hongera JPM Kwa kuongea kiswahili, hao waandishi walitaka waulize maswali.Haiwahusu uliwa cut short, hata Uingereza uiongee.
Mkuu hakuna mashindano ya essay,Kama kingereza sio dili kwa nini kitumike kama official language? Matokeo ya hii ndo hayo ya akina Magu kuzingua huko kwa watu Namibia,Zimbabwe si akomae na Kiswahili watu watafsiri kuliko kuzinguaHivi unaelewa Kiswahili wewe?! Hao wanaopeleka shule za Kiingereza ni imani yao tu kwamba hizo shule zinatoa elimu mzuri, ingawaje wapo pia washamba miongoni mwao wanaodhani Kiingereza ndio elimu mzuri! Kuwa na uwezo wa kifedha hakumfanyi mtu kutokuwa mshamba na ulimbukeni! Wengine ushamba ndo kipaji chao cha kuzaliwa! Lakini pia wapo wenye uwezo lakini sio washamba na limbukeni na ndio maana unakuta wana-opt kuwapeleka watoto shule kama Feza, ambako mtaala wao ni huu wa akina Kayumba, na dogo akitoka hapo yupo fit kuliko akina nyie mnaoabudu lugha ya mkoloni!
Lakini vile vile issue sio kupeleka watoto shule wakakifahamu Kiingereza bali issue ni kuonea fahari Kiingereza! Unafika mahali unataka watu wakujue kwamba unakijua Kiingereza ingawaje kwa Wakenya hata Kiingereza chao chenyewe hata kuvutia hakivutii kjutokana na lafudhi yao mbovu!! Hata huko maofisini ingawaje Kiingereza ni official language, utakuwa mshamba na limbukeni kuongea Kiingereza na wafanyakazi wenzako Waswahili eti kisa tu ni lugha rasmi ya kiofisi! Kiingereza kinatumika pale inapobidi; lakini mtu atakuwa mwehu yupo pale Kaunta ya CRDB anakuja mteja na kuanza "Hi! How can I help you!" Huo ni ushamba! Tena kuna malofa wengine unakuta yupo na Mzungu anajitahidi kuongea Kiswahili lakini lenyewe linalazimisha kuongea Kiingereza! Sasa kama sio ushamba tuite nini!
Na tukirudi upande mwingine, sio kwamba Wakenya hawakifahamu Kiswahili! Wanakifahamu sana tu ila wakikutana na Watanzania; sana na Watanzania, ndipo wanataka kujifanya hawakifahamu Kiswahili! Hawawezi kumtambia Mganda kwa sababu Waganda ni wazuri kwenye Kiingereza kuliko Wakenya lakini wanapenda sana kuongea lugha yao!! Aidha, tatizo la Wakenya na Kiswahili ni tabia yao ya kupenda kuchanganya sana na Kiingereza kutokana na ushamba ule ule niliousema hapo awali! Ukitaka kujua Wakenya Kiingereza sio chao sema tu ushamba na ulimbukeni, nenda vijijini au hata kwenye miji midogo na hicho Kiingereza chako kama hujakutana na Kipokoti pamoja na Kiswahili! Wakitoka Upokotini na kuingia Nairobi, ndani ya mwezi mmoja wanajifanya hawakijui Kiswahili!
Ndiyo maana hataki kwenda ulayaKwa kweli Magu anatia aibu ingefaa kusema mapema kwamba naweza mudu maneno machache tu ya kingereza afu mengine awe na mkalimani badala ya kujifanya unajua unatuaibisha,sasa sijui huko kwa wazungu maana kuwaelewa tu wanapoongea kwa ile rafudhi yao ni shida