Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Lazima kuna kitu amekufanyia
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] uwiiiiiiiih leo full burudani, nadhan hata uncle ameelewa kuwa mwanae na yeye hawapendwi.
 
Nimeshangazwa sana kuangushwa kwa Makonda na wana ccm. Hata yeye mwenyewe ameshangazwa sana! Amesema kuwa jambo hili limemuumiza sana! Kiasi kwamba akasema kuwa anamuachia Mungu! Na akawa anajiuliza kwamba amekoswa wapi?

Lakini hili limenifanya nijiulize maswali mengi. Mojawapo haswa, ni hili la Makonda kusifiwa kwa uchapa kazi sambamba na boss wake! Hata alipokuwa akilalamikiwa na wapinzani, yeye alimwambia “nenda kachape kazi”. CCM wenyewe kuanzia waziri mkuu, makamu wa Rais na hata Bashiru, hawakuwa na sauti mbele zake, wala ushawishi zaidi yake mbele za boss mkuu!

Yoye tisa, kumi, ni pale Bashiru alipokataa kumpa fomu ya kugombea urais mwana chama yoyote yule wa ccm zaidi ya boss mkuu. Hapa swali jingine nililojiuliza, ni je ni kwanini alikumbwa na wasiwasi mkubwa kama ni kweli boss mkubwa anakubalika sana ndani ya chama kwa uchapa kazi wake, wasiwasi wa nini hadi kuzuia wanachama wengine wasichukuwe fomu? Hili ni wazi kabisa kuwa wasiwasi wake umetokana na yeye kutokuwa na uhakika kuhusu vikao vya kumpitisha pamoja na kura za maoni ndani ya ccm.

Makonda yeye mwenyewe ameshindwa kutetewa na boss huku kwenye kura za maoni. Lakini bado ana kanafasi kengine majina yakipelekwa kwa boss. Lakini tayari hali inaonekana siyo shwari kama wanavyotaka tuamini. Ninaamini wengi wako kwa nidhamu ya woga. Hivyo siwezi kushangazwa Membe akifuatiwa na wengine kuisambaratisha ccm. Kivumbi zaidi kitakuja kama ikitokea kuwa majina yaliyopelekwa, yakakatwa baada ya boss kuamka kivingine!

Huu ni ule mwaka wa kuona mengi. Tuombe amani.
 
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima

Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?

Wengi wa watanzania hawakubaliani na baadhi ya mambo ya kundi lile dogo! Na kama wataonyesha maamuzi hayo kwenye sanduku la kura, basi 'Jechalisation' lazima ifanyike ili kundi lile dogo linusurike.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuruka na kukanyagana tyuuuh hakuna namna
 
Siyo "ku-influence" bali nimetoa rai kwa vikao vya juu viheshimu maamuzi yaliyofanywa na kikao cha mapendekezo cha wanaccm wa jimbo la Kigamboni
ujumbe wameupata kaka huna shaka kuhofia lolote lile ..watajuana wenywe
 
tusihishi maisha ya peponi wakati tuko duniani...midomo tuchunge sana kuna muda watu wananyamaza tu lakini ww utajutia maamuzi siku moja
 
Swali fikirishi hivi mwaka huu wabunge wa kuteuliwa na mkulu watakuwepo?
 
'Paulo sitaki kucheza na wewe una mikono michafu' ni kibwagizo au kichwa cha wimbo tulikuwa tukiimba darasa la kwanza au la pili enzi hizo. Simkumbuki mtunzi wala jina la kitabu.
Matokeo ya primaries za CCM Kigamboni yamenikumbusha wimbo huu. Ni kama vile wana-Kigamboni walikuwa wakiimba wimbo huu.

Hata huyu jamaa amekumbuka wimbo huu fadhili malima - @mkuranga Twitter Profile and Downloader | Twaku
 
Swali fikirishi hivi mwaka huu wabunge wa kuteuliwa na mkulu watakuwepo?
Yes, hao wabunge wa kuteuliwa wasiozidi 10, wapo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo hilo halina shaka kuwa Rais ataitumia Katiba hiyo
 
Sabuni ni dawa hutaki kunawa,una mikono michafu.
Paulo usije kucheza na sisi.
 
Naoma kulike mara elfu moja
 
Ni ujumbe kuwa Makonda na Magufuli aliyemkumbatia muda mwingi tumewachoka.
Ndio maana Magufuli alihakikisha anasimama mwenyewe kwenye kura za maoni.
Angeacha kampenyo tu asingetoboa
Kweli kabisa
 
Kama makonda naye ni mtu katika nchi hii Kama alivyokuwa kwenye serikali ya Magu ,basi sisi kuwa masikini Kama taifa na mtu mmoja mmoja ni halali yetu maana wote tutakuwa tu empty heads
 
Yes, hao wabunge wa kuteuliwa wasiozidi 10, wapo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo hilo halina shaka kuwa Rais ataitumia Katiba hiyo
Kwa mantiki hii mpango B unaweza kutumika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…