Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima
Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?
Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?
Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake...