Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Lina ukweli,Ila ni Hadi ashinde October,siasa ni upepo sio hesabu chochote chaweza tokea.
 
Kutumia Kodi zetu kwenda kupendezesha dodoma then kusiwe na tija kiuchumi na kuacha vipaumbele muhimu vya kuchochea uchumi lengo tu ni kutafuta kukumbukwa ni matumizi mabaya ya Kodi zetu ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana.
 
Wengi wanamchukia Makonda kwa sababu ya wivu tu. Makonda sio lazima awe Mbunge hiyo ndio ilikuwa nia yake lakini Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema amependezwa zaidi afanye kazi nyingine. Ukiona nchi kubwa kama USA inadiriki kumpiga marufuku kwenda USA ati kwa sababu amekataa ushoga kuenea kwenye mkoa wa dar Es Salaam au madawa ya kulevya aliweza kupambana nayo lazima ufahamu kwamba alitimiza wajibu wake kuendeleza gurudumu la kuendeleza imani na tamaduni zetu. Makonda hawezi kukata tamaa atafanya kazi nyingine kama Mtanzania yoyote yule.

Kuvunjika kwa ungo sio mwisho wa kupepeta.
 
Makonda alichanga vibaya karata zake alikuwa anatakiwa Jimbo la Ukonga kule angeshinda sababu waitara alishakimbia Jimbo lipo wazi.Thus wameona wampe Jerry
 
Kwa hiyo Marekani hawana akili kumzuia kukanyaga USA?
 
Kwahiyo hayo yote uliyoorodhesha kama mafanikio una hakika ni kwa juhudi zake? Halafu mkuu yaani kama huelewi kwanini watu hawampendi basi umeamua tu kutoelewa, kama sivyo basi kuna tatizo la msingi.
 
Usiwape chochote kwa sasa mpaka baada ya vikao vya juu maana yule ni kipenzi cha Mwenyekiti wa hivyo vikao na ni homeboy. Awamu hii kila kitu kinafanikiwa kutokana na watu wanavyoamka siku ya tukio.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema.
Kiongozi akionekana na mama wa barabarani huyo hafai kuwa kiongozi. Aliyemchagua anatakiwa kuweka mtu mwingine badala yake bila hata kumjulisha.
Kuhusu Mh. Makonda, shutuma zilizokuwa zinatolewa kwake bila kujali ni za uongo au kweli na hasa za kielimu na zinazohusu uhai wa watu ni shutuma mbaya sana na zinaharibu image ya mtu mbele ya umma na hata kwa vizazi vijavyo.
Hakuna shutuma mbaya kama ya kumsingizia mtu kuwa anatoa uhai wa mtu mwingine. Ni ngumu sana kumsafisha na yeyote anayetoa tuhuma kama hizi ni ngumu pia kusema nilikosea.
Yaliyotokea kwa mh Makonda ni ajali ya Kisiasa kama ilivyomtokea Lowasa wakati wa Sakata la Richmond.
NI uongozi wa pamoja lakini inapotokea dosari ni lazima moja awajibike.
Pia hakuna jambo baya kama kiongozi kutumia kofia ya mkubwa katika kutawala watu ( kuwa na father god). Watu watakuheshimu kwa sababu ya uwezo wako katika utendaji kazi lakini watu watakuogopa kama unatumia madaraka ya Rais wa INCHI katika kuwatawala.
 
Hilo ni somo kwa magufuli kwamba itakua hivi pia kwake siku akiondoka
Ingekuwa hivyo kwake Kama Chama chake kisingeona hilo mapema na kutoruhusu watia nia wengi wa nafasi ya Urais kushinda nae. Kwake kura ya ndiyoooo iliyozoeleka ndo ilitumika na kupitishwa.
 
Mimi binafsi namkubali sana makonda,ni kijana ambaye ametuwakilisha vizuri sana . hao wanaomchukia ni wivu tu unawasumbua
 
Kwahiyo hayo yote uliyoorodhesha kama mafanikio una hakika ni kwa juhudi zake? Halafu mkuu yaani kama huelewi kwanini watu hawampendi basi umeamua tu kutoelewa, kama sivyo basi kuna tatizo la msingi.
Kwa juhudi za nani sasa mimi huwa sina prejudice napenda kiongizi anayejihusisha na matatizo ya wananchi moja kwa moja, mambo aliyefanya Makonda yaliwashinda viongozi wengi tu na ndio point inayombeba hayo mengine mimi kama mwananchi wa kawaida siyajui, mimi nazungumzia uwezo wake wakufanya kazi na kusimamia haki katika jamii anayoiongoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…