Watanzania lazima Tufahamu Rais wa nchi siyo Sawa na Rais Wa Bendi ya Mziki kiulinzi na Kiusalama

Watanzania lazima Tufahamu Rais wa nchi siyo Sawa na Rais Wa Bendi ya Mziki kiulinzi na Kiusalama

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Kuna watu wanaleta ujuaji Sana hapa nchini, Kuna watu wanafikiri kila kitu ni siasa, Kuna watu wanafikiri kila kitu ni sawa na wanavyowaza, kuna watu wanamchukulia Rais Kama raia wa kawaida, kuna watu kwa upeo wao mdogo wanamlinganisha Rais na sisi, Kuna watu wanazani uzito wa Rais Ni Sawa na uzito wa Mwenyekiti wa chama kilicho kama Saccos.

Lazima Tufahamu kuwa Rais wa nchi Ni mkuu wa nchi na kiongozi wa Serikali, Ni Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Akishakupigiwa kura na kuapishwa hawi Kama yule uliyekuwa unamfahamu, hajiamulii mambo Kama alivyookuwa anajiamulia kiusalama, Haendi kila sehemu aliyokuwa anaenda awali, hapiti kila eneo alikokuwa anapita awali, Hali chakula kila mgahawa alikokuwa anakula awali, hasalimiani na kila mtu Wala hasogeleani na kila mtu hata Kama alipanga msitari kumpigia kura katika uchaguzi, Wala hapandi kila gari na kupita popote pale na njia yoyote ile.

Lazima Tufahamu kuwa kila kitu kinawekwa katika utaratibu maalumu, utaratibu wa kijasusi,utaratibu wa kiusalama na kiulinzi, lazima Tufahamu kuwa usalama na ulinzi wa Rais wa nchi Ndio Jambo la muhimu kuliko kitu kingine chochote kile hapa nchini, amani na utulivu wa nchi hauwezi ukatenganishwa na usalama wa Rais na familia yake.

Rais hawezi akayumba kiafya halafu utegemee nchi isiyumbe, lazima iyumbe, itetemeke, ipepesuke, mambo lazima yatetereke na kusua sua, lazima idara zisimame kazi zake, lazima watu watege masikio juu ya Hali ya Rais, lazima mawazo ya watu yawe mahali pamoja tu, lazima kila muda iulizwe Hali ya Rais ikoje, lazima ufanisi wa kazi upungue makazini kwote na kila idara, mpaka Rais atakapo toka hadharani kulipungia mkono na kulisalimu Taifa ama kulihutubia Taifa letu ndipo mioyo ya watu itapona na kupata amani na Kuendelea na kazi kwa moyo wote.

Hivyo tusiwafundishe Wala kuwaingilia katika kazi watu waliopewa dhamani juu ya ulinzi na usalama wa Rais wetu, Tusiwachanganye Wala tusiwaone Ni wajinga, Mwenyezi Mungu alitupatia maarifa wanadamu hivyo lazima maarifa yote yatumike katika kuhakikisha Rais anakuwa salama muda wote, hiyo ni kazi yao. Ni wajibu wao wakufa na kupona kuhakikisha Rais Ni salama. Tusilete uanaharakati kwa kila Jambo.

Macho yetu lazima tujuwe Ni vipofu linapokuja suala la ulinzi na usalama wa Rais, sisi tunaona kwa macho haya ya nyama pekee, macho ya kukosoa, ambayo yanafumba hata upepo ukipita, macho yetu siyo Kama ya wale tuliyowapa dhamani ya ulinzi wa Rais wetu mpendwa, wao wanaona mbali, wanao hata tusivyoweza kuona kwa macho ya kawaida, wanaona hata kabla ya kukaa, wanaona hata mioyo yetu, wanaona hata ishara zetu, wanaona hata mifuko yetu, wanaona hata katikati yetu. Wakati sisi hata tukizibwa na mtu mrefu mbele yetu hatuwezi kusimulia kilichokuwa mbele yetu hatua chache.

Tuache ujuaji na kukosoa kila kitu, tuache uanaharakati kwa kila kitu, tuache utalaamu kwa vitu ambavyo hata darasni hatujawahi kukaa kujifunza, tuache umbilikimo wa kifikira na kimawazo, tuache werevu wakati ni vipofu wa masuala ya usalama, Tuache idara zetu za usalama zifanye kazi zake, zitekeleze wajibu wake.

Idara yetu ya ulinzi na usalama wa Rais Rai yangu kwenu ni kuwa endeleeni na majukumu yenu Wala msiyumbishwe Wala kuondolewa katika mstari wenu ,Wala kufundishwa kazi, Wala kuelekezwa na mtu wa nje kipofu wa masuala ya ulinzi na usalama, tunachohitaji Ni kuona Rais wetu ni salama kwa gharama zozote zile, tunampenda Rais wetu na tumewakabidhini ulinzi na usalama wake muutekeleze ipasavyo na kwa weledi mkubwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu mtoa njia maarifa.

Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Hayo ndo madini sasa. Yaani watu wnapokutana na kiongozi asopebda kusikia lawama za kila jambo wanaanza kelele, tumieni vema nafasi hii ya kiongozi anaeruhusu kila jambo kusemwa kwa maendeleo ya nchi. Mtu anahoji kwa Nini Rais kapandishwa Coaster, na bila shaka hata Angepandishwa chombo gani wangehoji tu, mara kitu kanisani. Hayo yanatuhusu nni kama nchi? Kuna mambo ya kufuatilia siyo hayo mambo ya kitoto.
 
Haya ni matumizi mabaya ya muda, umeandika upuuuuuzi weeeee, hakuna hata pointi ya maana na huyo Rais wako. Watanzania tunateseka kwa hali ngumu ya maisha, maji ya bomba hakuna, huduma za afya mbovu, barabara mbovu, chakula bei juu, Polisi kumejaa rushwa, Mahakamani kunanuka rushwa, mahospitalini kumeshamiri rushwa, ardhi ndo usiseme ni uozo wa rushwa halafu unakuja na ngonjera zako hapa za uchawa, mbona huyo Rais wako Londan alipandishwa daladala na akawahi siti ya dirishani.
 
Pale unapotoa ulimi kama wote halafu hata tone la asali halikudondokei.
russ.png
 
Uzi una lengo gani???
Rais lazma akimbilie chato akajilogeze au akajiweke quarantine ya Corona huku akidai hamna korona
Binadamu wengine ni majanga matupu.Amepewa maarifa ayakabili mazingira halafu yeye anakimbilia mafusho.
 
Yani uzi mzima umeandika kutujuza kwamba Rais ni Amir jeshi mkuu? Kwamba ndiye mkuu wa nchi? Dah Tanzania bhana
Ukiendelea kumpa ushauri wa kuandika sentensi fupifupi katika paragrafu chache hivi atanuna.Jamaa anajua kujieleza mambo mengi kwa pointi moja tu.😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom