Watanzania mbona msiwape taarifa makampuni ya kimataifa yanayong'ang'ania kuajiri Wakenya kwamba hawaruhusiwi

Watanzania mbona msiwape taarifa makampuni ya kimataifa yanayong'ang'ania kuajiri Wakenya kwamba hawaruhusiwi

Mkenya hajawahi kuogopa chochote na ndio maana tunatawala ukanda huu kiuchumi, kielimu, kijeshi na kila kitu....uthubutu wetu.

[emoji16][emoji16][emoji16]mnamtawala nani kijeshi na kiuchumi kama sisi ndio tunaweza kuwawekea sunction!![emoji23][emoji23]

sema mnaongoza kwa RANKS za wazungu[emoji23]
 
You have used a lot of time to write something which has simple answers, the policy is:

If you don’t get a complement Tanzanian the look elsewhere, now, How do you prove that? So many qualified Tanzanians!

Mwenyewe umejua nini umeandika????
Akikataliwa Mkenya huletwa Mwarabu au Mhindi, ingekua mnakatalia Mkenya ila anaajiriwa Mtanzania.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]mnamtawala nani kijeshi na kiuchumi kama sisi ndio tunaweza kuwawekea sunction!![emoji23][emoji23]

sema mnaongoza kwa RANKS za wazungu[emoji23]

Ni nini mnacho ambacho hakikutoka kwa wazungu, zana zote za kijeshi za kwao, hivyo hamna jeuri ya kubishia rankings zao.
Mpaka simu anayotumia rais wenu imetoka kwao, mtandao anaotumia, magari, mavazi yaani Mswahili labda kucheza vigodoro tu ndio vya kwenu.
 
Kwani wakenya ni lazima kufanya kazi Tanzania kwanza kuna Corona mnang'ang'ania nini si mkae kwenu
 
Kwani wakenya ni lazima kufanya kazi Tanzania kwanza kuna Corona mnang'ang'ania nini si mkae kwenu

Makampuni ya kimataifa ndio yanang'ang'ania kuajiri Wakenya, inapaswa mfahamu haya makampuni yanamilikiwa na wenye hisa, kawaida ya hao wenye hisa huwa hawana pumba za uzalendo, wao huzingatia ufanisi na weledi...basi.
Jaribu ujitutumue umiliki japo hata biashara ndogo ya kuchuuza madafu ndio utaelewa nini kinazungumzwa kuhusu humu.
 
achana na ujinga bana,siku hizi hakuna sehemu hamna wataalamu,ndio sababu hata kuna watanzania hata huko kwenu.
 
Kuna hizi taarifa naona zimezagaa kote kwamba kampuni ya Coca Cola imeng'ang'ania kuajiri Mkenya awe mkurungezi wa tawi lake Tanzania, ila kwamba Tanzania imemkatalia kama ambavyo imekua desturi sasa, ambapo haya makampuni ya kimataifa yanatumia hela nyingi sana kusaka nani mwenye weledi na bidii ya uchapa kazi wa kuyasimamia na kila wakiishia kuchagua Mkenya, anakataliwa na serikali ila yeyote mwingine awe Mhindi, Mwarabu au Chotara anaruhusiwa.

Inapaswa itolewe tamko rasmi kutokea kwa serikali kwamba Wakenya hawaruhusiwi tena kusimamia hayo makampuni, hapo itawarahishia hao nafasi wawe wanatangazia wahind na waarabu. Inapaswa ifahamike haya makampuni huwa hawaajiri zumbukuku au zwazwa yeyote, lazima wasake kwa mapana na marefu maana wana taratibu zao zilizopitia ukaguzi wa hali ya juu, na kama wanamkosa humo ndani ya milioni 60 ya Watanzania wanayemtaka, basi haipaswi kuwapangia.
------------------------------------------------

Dar es Salaam. Tanzania’s Immigration Department said on Tuesday, 24 November 2020 that it would issue a statement in response to claims that it had denied entry to a foreign national who was to start working as new managing director for Coca-Cola Kwanza.

Since Monday, November 23, social media platforms have been awash with news of a foreign national, assumed to be Kenyan, who was denied entry into Tanzania so he could assume his role as managing director for Coca-Cola Kwanza.

The news item originated as a tweet from fichuaTanzania_official’s FichuaTanzania, a Twitter handle that markets itself to its readers as one [a handle] that documents and exposes human rights abuses in Tanzania while also fighting for freedom of speech, truth and democracy.

“Leo 23/11/2020 Mkurugenzi mpya wa Coca Cola Kwanza akitokea Nairobi na shirika la ndege la Kenya Airways amekataliwa na mamlaka uhamiaji ya Tanzania kuingia nchini kutekeleza majukumu yake mapya kwa maelezo kuwa kazi anayokuja kufanya kuna watanzania wenye uwezo wa kuifanya,” the twit reads.

coca11

Literally, this is translated as: “The new Coca-Cola Kwanza managing director was on November 23, 2020 denied entry into Tanzania upon arrival from Nairobi on a Kenya Airways flight. The Immigration Department did not allow him in on the grounds that there were Tanzanian nationals who could perform his duties [at Coca-Cola Kwanza]”

Hii sidhani kama inatusaidia sana kama Taifa, ni bora kujiuliza ni kwanini watanzania hatuaminiki mbele ya waajiri wengi kwenye medani ya kimataifa . Ipo hatua kwenye uwajibikaji ambayo Kenya wameishaifikia lakini sisi bado sana. Hii itaendelea kutuumiza hadi siku tutakapoukubali ukweli na kuufanyia kazi. Na tatizo limeanzia kwenye ngazi ya msaidizi wa nyumbani hadi CEO wa taasisi kubwa
 
Mbna ya yule mhindi hamkuulizia CV[emoji23][emoji23][emoji23]
Wivu wa kijinga sana ndio mko nao, kwn nyinyi hapa JF ni akina nani mpka mjikute ndio board ya coca cola..
Sisi ni WaTanzania tuliowapapasa mawowowo hadi mnalialia mmenogewa na mpapaso mnalazimisha kujileta huku wakati hatuwataki
 
Inapaswa itolewe tamko rasmi kutokea kwa serikali kwamba Wakenya hawaruhusiwi tena kusimamia

Kwani lazima itolewe tamko rasmi?

Tumeonyesha kwa vitendo, matamko ya nini? Get a clue!

Hatuwataki. Point blank.

Kama mna uwezo ambao sisi hatuna basi kafungueni hayo mabiashara kwenu, tena mgundue li soda jipya la kupambana na Coca Cola.

Kwa nini mpate stress nyiiingi kushindana na Watanzania kuwauzia wazungu soda lao na nyinyi ni wakali saaaana wa biashara ????

Bakini Kenya na li drinki lenu mtakalogundua mliuze Kenya na mli-ship Tanzania mpaka Ivory Coast. Mjapani anauza magari Tanzania, ushamwona anahangaika kuomba Working Visa ya kukaa hapa kuuza magari? Anayatuma juu kwa juu, anakula bata kwao Nagasaki.

Ondokeni. Plain and simple.
 
achana na ujinga bana,siku hizi hakuna sehemu hamna wataalamu,ndio sababu hata kuna watanzania hata huko kwenu.

Hao "wataalam" wa kwenu hawajakidhi vigezo vinavyotakiwa na hayo makampuni, ndio maana mkikatalia Wakenya, hawaajiri wazawa wenu, wanafuata huko nje aidha kwa Waarabu au Wahindi, ambapo mkiletewa ngozi nyeupe mnaufyata ila akiletwa Mkenya nchi yote mnapiga ukunga.
 
KCB tanzania iko na mtz na ni benki ya kenya!!!

fafanua hilo swala kabla hatujaenda mbele.
 
Kwani lazima itolewe tamko rasmi?

Get a clue!

Tumeonyesha kwa vitendo, matamko ya nini?

Hatuwataki. Point blank.

Kama mna uwezo ambao sisi hatuna kafungueni hayo mabiashara kwenu huko tena mgundue li soda jipya la kupambana na Coca Cola.

Kwa nini mpate stress nyiiingi kushindana na Watanzania kuwauzia wazungu soda lao na nyinyi ni wakali sana wa biashara ????

Ondokeni kaazisheni li drinki lenu jipya Kenya mliuze Kenya mli-ship Tanzania mpaka Ivory Coast huko. Mjapani anauza magari Tanzania, ushamwona Mjepu anahangaika kuomba Visa ya kuishi hapa kuuza magari? Anayatuma kwenye meli anakula bata kwao Nagasaki na Kumamoto huko.

Ondokeni. Plain and simple.

Sio sisi, in fact sisi tunapiga mishe zetu freshi huku na ndio maana Kenya inaongoza ukanda wote huu kiuchumi, kielimu, kijeshi n.k.
Sema hayo makampuni ya kimataifa ndio yanang'ang'ania yanataka Wakenya, sasa hao ndio muwapigie hizi kelele zenu.
 
KCB tanzania iko na mtz na ni benki ya kenya!!!

fafanua hilo swala kabla hatujaenda mbele.

Japo benki yetu ya KCB ndio kubwa ukanda wote huu, ila haijafikia hadhi ya Coca-Cola, hivyo hawawezi wakawa na uhitaji mkubwa sana likija suala la kiuongozi, watamuweka kajamba yeyote tu na pia makao makuu hayako mbali na huko, watakua na uwezo wa kufuatilia kwa karibu kila akiboronga.
Lakini kwa Coca-Cola, ni kampuni ambayo thamani yake inazidi uchumi wa Tanzania yote bara hadi visiwani na ushee yaani $80b, huwa lazima wawe makini sana kwenye kila wanayemteua kuongoza nyadhifa zozote, hawawezi wakaajiri zwazwa yeyote tu kisa pumba za uzalendo.
 
Makampuni ya kimataifa ndio yanang'ang'ania kuajiri Wakenya, inapaswa mfahamu haya makampuni yanamilikiwa na wenye hisa, kawaida ya hao wenye hisa huwa hawana pumba za uzalendo, wao huzingatia ufanisi na weledi...basi.
Jaribu ujitutumue umiliki japo hata biashara ndogo ya kuchuuza madafu ndio utaelewa nini kinazungumzwa kuhusu humu.
Nyie mnajulikana kwa snitch na kujipendekeza kwa wazungu zaidi hamna lolote biashara ninayo ila siajili wakenya watz wanatosha
 
Nyie mnajulikana kwa snitch na kujipendekeza kwa wazungu zaidi hamna lolote biashara ninayo ila siajili wakenya watz wanatosha

Hehehe jameni mitandao ya kijamii, eti biashara unayo ila hauwezi kuajiri Wakenya, utoe wapi hadhi ya kuajiri Mkenya, kwa kauli zako humu ni wazi hata hao Watanzania labda uajiri dada wa nyumbani afue nguo zako hapo mabandani Buza.
 
Wakenya wako wengi huku mpaka wengine wanajifanya watz si ajabu ma wewe uko Tanzania umeajiliwa kampuni ya ulinzi
 
Sisi ni WaTanzania tuliowapapasa mawowowo hadi mnalialia mmenogewa na mpapaso mnalazimisha kujileta huku wakati hatuwataki
We ni bwege sana kumbe, kwhyo wakeny katika hayo makampuni wanajiajiri sio[emoji122][emoji122]
 
Mnajistukia tu na Mihemko yenu ya Kikenya plus inferiority Complex,
Nawajua Wahindi Kibao,
Waganda Kibao,
Wapakistan na Wachina Kibao walionyimwa working permits for same reasons, mtu amesoma diploma ya finance anakuja kufanya kazi Tz si ufala huo?
Kenyans mna midomo mikubwa na Mirefu kushinda hawa wote.
Mwisho wa Siku Kama unataka kufanya biashara Tanzania it's our terms and Condiotions, huwezi fungasha sepa. After all these are not serious investors aiming at exploiting, making profits and running away.
Kwani wakati wakenya wanazuia export kutoka Tanzania walitangaza kwamba hawataki biashara na Tanzania? Naona majuha humu yanashabikia Magu anawajengea kujiamini ila wahuni wanashangilia
 
Japo benki yetu ya KCB ndio kubwa ukanda wote huu, ila haijafikia hadhi ya Coca-Cola, hivyo hawawezi wakawa na uhitaji mkubwa sana likija suala la kiuongozi, watamuweka kajamba yeyote tu na pia makao makuu hayako mbali na huko, watakua na uwezo wa kufuatilia kwa karibu kila akiboronga.
Lakini kwa Coca-Cola, ni kampuni ambayo thamani yake inazidi uchumi wa Tanzania yote bara hadi visiwani na ushee yaani $80b, huwa lazima wawe makini sana kwenye kila wanayemteua kuongoza nyadhifa zozote, hawawezi wakaajiri zwazwa yeyote tu kisa pumba za uzalendo.

huu mchezo hautaki hasira.

si mko na elimu,na juhudi ya kazi!!
 
huu mchezo hautaki hasira.

si mko na elimu,na juhudi ya kazi!!

Hivyo vitu viwili ndio mtaji wetu, elimu na juhudi ya kazi ndivyo vinafanya Wakenya wasakwe hadi huku, makampuni ya kimataifa yanatung'ang'ania....
Kawaida haya makampuni huwa hayatangazi nafasi za ngazi ya juu, wao huwa na mbinu zao za kupeleleza na kusaka nani anayewafaa, yaani Mkenya yupo busy kwenye kazi zake ghafla anaalikwa mahojiano na bonge la kampuni, wanamuomba asafiri akaukwae ukurugenzi kwenye nchi ya watu.
 
Back
Top Bottom