Watanzania mngekuwa na mtizamo kama wangu CCM ingekuwa imeondoka tangu 1995 na nchi hii tungekuwa mbali kimaendeleo

 
Watu wanailaumu CCM bure. Tatizo kubwa lipo kwetu Sisi Watanzania ambao hatujui tunasimamia wapi.
Hebu tujiulize nchi za wenzetu zilizoendelea kama China,Marekani,Japan,Urusi n.k watendaji na Wananchi wao wanafanyaje kwa maendeleo ya nchi zao.
Hapa Bongo ukiwa Kiongozi sehemu yeyote ukakaza katika utendaji mfano kusimamia taratibu zilizowekwa utapigwa vita vibaya mno. Watanzania kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu katika sehemu wanapojishughulisha wanawaza kuiba kwa maslai ya familia zao.
Hebu jiulize mtu anayediriki kuiba vyuma kwenye daraja ama transformers ambapo anajua kabisa ni kwa ajili ya maslahi ya nchi.
Tanzania hii hata wapewe Chadema,ACT,CUF ,TLP bado umaskini hautaisha.
Tanzania hii hamna Kiongozi yeyote wa Upinzani mwenye uchungu na maendeleo ya nchi. Wote ni wachumia tumbo tu.
Tukitaka Tanzania iendelee inabidi watu wengi waumie. Maana watu washazoea kufanya mambo kwa utamaduni ambao kubadilishwa panahitajika nguvu za ziada.Kuna watendaji serikalini kuanzia ngazi za chini inabidi wawekwe pembeni. Magereza nazo inabidi ziongezwe maana majizi ni mengi. Yaani unakuta ofisi ya uma kuanzia secretary hadi Kiongozi wa juu ni mwendo wa dili na rushwa tu. Watu hawapo serious na maendeleo ya nchi. Watu wanapeana nafasi nyeti za kiutendaji na kimaamuzi kindugu,kirafiki,kikanda,kikabila na hata kiitikadi za dini.
Kiufupi tuna safari ndefu sana kuja kuwa developed country.
 
Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hata Zanzibar huchaguliwa na sanduku la kura?
Ktk wote waliokaa kwenye kiti tangu nipate akili,
Huyu wa sasa simwelewi hasa swala la Bandari,
Siku hizi nikiona msafara wake au taarifa ya habari kwenye tv ama radio nakuwa sitaki hata kumsikiliza nakuwa najisikia kusononeka moyoni.
Sioni uzalendo, uwezo, umakini, uchapa kazi ndani yake.
 
Ccm wala sio wajinga bali wajinga ni sisi tunaotawaliwa.
 
Una hoja yenye mashiko sana. Kitu walichowin CCM ni kuwapatia elimu ya kijinga watanzania. Elimu ya kutojua kuhoji masuala mtambuka ya nchi yetu. Umasikini wa fikra na kipato ndio kaburi letu, maana wengi wanaishia kuwa ombaomba na machawa ili wakumbukwe. Hata wale waliosoma na kuwa maprofesa, hawana jipya la kuondoa hili ombwe. Kimsingi we are doomed until tuamshwe na ari zetu kwa umasikini huu huu. Kqma sivyo wau wa aina yako mtaemdelwa kuumia huku mamia wakiendelea kuwa msukule.
 
Nadhani kwenye hii nchi inawezekana nikawa Mtanganyika namba moja ninayeichukia hii kitu inayoitwa ccm kutoka moyoni! Tangu enzi na enzi, mimi na ccm ni chui na paka.

Na nina sababu lukuki, na za msingi kabisa za kuichukia.
Kwa mfano Mimi sipo CCM sijawahi kuwa CCM na sitakuja kuwa CCM eee mwenyezi Mungu nisaidie kuniepusha na huyu mshauri wa shetani CCM!
 
Ingekuwa ishu ni kusombwa na lorry tu usingemuona mtu huko, ishu ni bakshishi inayoambatana na huko kusombwa
 
Tupo pamoja na sijawahi kuipigia kura CCM katika nafasi yeyote ile, ila vijana wameanza kuamini ajira muhimu ni uchawa,na Raisi wanamwita mama wanaamini mama ndio anatoa pesa zote ile nchi na sio Kodi wanayolipa wao, safari bado ni ndefu
 
Bora umeujua ukweli tu, siku ambapo tutaweka utaifa mbele na si maslahi yetu na familia zetu ndipo ambapo tutaondokana na huu mkwamo.

Mihimili ile mitatu itakapotenganishwa na kila mmoja kusimama kivyake ndipo tutaposonga mbele. Ila Kwa style hii ya bunge kuburuzwa Kwa hisani za Ikulu pamoja na mahakama na majeshi yetu kuwa in favour ya interests za Magogoni na sio welfare ya raia tutakuwa na miaka 1000 ya mateso
 
What's wrong with you? You must be a wark or a spiv. Yaani unaishi maisha ya peke yako ndoto peke yako unaota 50% ya Watanzania wawe wajinga kama wewe?
 
INASIKITISHA WALLAH
 
Tatizo kubwa TZ ni wanawake asilimia 70% ya kura za CCM zilitoka kwa wanawake...ila kwa sasa huyu haramia sa100 hakubaliki hata na wanawake kutokana na upumbavu uliotukuka alio uonyesha dhidi ya
1) taifa letu .
2)tanganyaka
3)uzalendo
4)kukumbatia mafisadi wa aina zote
5)dharau kwa wananchi kwa kuwaona kama manyani tu yanayo stahili kutawaliwa na mabeberu na wajomba zake wa kiarabu ....mambo ni mengi sana ya kishenzi yanayo fanywa na serikali hii dhalimu ya awamu ya 6
 
Nadhani kwenye hii nchi inawezekana nikawa Mtanganyika namba moja ninayeichukia hii kitu inayoitwa ccm kutoka moyoni! Tangu enzi na enzi, mimi na ccm ni chui na paka.

Na nina sababu lukuki, na za msingi kabisa za kuichukia.
Hutufikii mimi na bwana Tindo...CCM ni laana kwa Watanzania,imeua NDOTO na MAISHA ya watu wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…