Watu wanailaumu CCM bure. Tatizo kubwa lipo kwetu Sisi Watanzania ambao hatujui tunasimamia wapi.
Hebu tujiulize nchi za wenzetu zilizoendelea kama China,Marekani,Japan,Urusi n.k watendaji na Wananchi wao wanafanyaje kwa maendeleo ya nchi zao.
Hapa Bongo ukiwa Kiongozi sehemu yeyote ukakaza katika utendaji mfano kusimamia taratibu zilizowekwa utapigwa vita vibaya mno. Watanzania kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu katika sehemu wanapojishughulisha wanawaza kuiba kwa maslai ya familia zao.
Hebu jiulize mtu anayediriki kuiba vyuma kwenye daraja ama transformers ambapo anajua kabisa ni kwa ajili ya maslahi ya nchi.
Tanzania hii hata wapewe Chadema,ACT,CUF ,TLP bado umaskini hautaisha.
Tanzania hii hamna Kiongozi yeyote wa Upinzani mwenye uchungu na maendeleo ya nchi. Wote ni wachumia tumbo tu.
Tukitaka Tanzania iendelee inabidi watu wengi waumie. Maana watu washazoea kufanya mambo kwa utamaduni ambao kubadilishwa panahitajika nguvu za ziada.Kuna watendaji serikalini kuanzia ngazi za chini inabidi wawekwe pembeni. Magereza nazo inabidi ziongezwe maana majizi ni mengi. Yaani unakuta ofisi ya uma kuanzia secretary hadi Kiongozi wa juu ni mwendo wa dili na rushwa tu. Watu hawapo serious na maendeleo ya nchi. Watu wanapeana nafasi nyeti za kiutendaji na kimaamuzi kindugu,kirafiki,kikanda,kikabila na hata kiitikadi za dini.
Kiufupi tuna safari ndefu sana kuja kuwa developed country.