ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Kuna kipindi niliamini chama kitakachomkomboa Mtanzania ni Chadema ila nilikuja kubadilisha msimamo wangu nikaamua kushabikia CCM na sababu iliyonifanya niachane na upinzani ni kitendo cha Chadema kumsimamisha Lowasa 2015. Kiukweli niliumia sana roho nikajisemea moyoni haiwezekani kiongozi anaruhusu ndani ya club yake biashara ya madawa ifanywe kuharibu vijana.
Basi ikawa hivyo nikaamua tu kuwa upande wa CCM na kufurahia anguko la CHADEMA japo katika uchaguzi mkuu sikuunga mkono namna uchafuzi uliotokea ule haukua uchaguzi mimi mwenyewe nilikuwa msimamizi msaidizi wa kituo niliyoyaona yanasononesha.
Ila kwa sasa nimekuja kujua CCM ndio wanaotuchelewesha na kutuumiza. Sababu kubwa ni chama cha CCM kimejaa darasa la Saba wa kutosha nenda katika ngazi za wilaya huko utaona viongozi wao ni watu wa namna gani lakini chadema Kuna watu waliosoma cha ajabu hawapewi nafasi.
Kikubwa naomba msamaha kwa yote tusameheane lakini kama ni mipango tuanze sasa hivi ya kuliokoa hili taifa ni heri tufe lakini kieleweke. Kama unaniunga mkono bonyeza like na kisha tupaze sauti popote mlipo muda umewadia kishindo kimefika tusidanganyike tena.