Watanzania naombeni mnisamehe kwa hii misimamo yangu ya kisiasa

Watanzania naombeni mnisamehe kwa hii misimamo yangu ya kisiasa

Mimi binafsi nimekusamehe mkuu, ni wajibu wetu kuendelea kuelimisha wengine wajitambue pia. Hata kama hawatajiunga na chama cha upinzani lakini wajue tu shida iko wapi, wapaze sauti kwa namna yao.
 
Wewe ni wakala wa wanasiasa.
Unaangalia kwenye unafuu kwa wakati huo.
 
Mkuu umeongea vizuri sana haswa tuhuma za familia ya kina Mbowe kujihusisha na madawa ya kulevya, huu ni ukweli kabisa na usikute mpaka leo bado wanafanya hivyo. Usipende sana kushabikia kutawaliwa na viongozi waliosoma au kuombea Chadema kuja kushika hatamu hapa Tanzania kwani viongozi wengi waliosoma hawana machungu na taifa hili, believe me they will come and destroy this country.

Angalia zama za Kikwete kwa mfano, alijitahidi kuchagua viongozi waliosoma katika serikali yake. Karibia viongozi wote aliowachaguwa walikuwa uselesss katika uongozi. Some were Professors lakini walikuwa wabovu shinda hata mtu wa darasa la 7.

Africa as a whole bado tuna matatizo sana ya utawala kwani kila kiongozi atataka kuja kutawala ili aibe na kujinufaisha yeye na ukoo wake. Binafsi sina kabisa imani na Chadema au chama cha Zitto, wote ni wasanii tu.
 
Tupo wengi na wapo wengi sana tunaojua na kufahamu CCM ndio chanzo cha matatizo mengi katika Taifa hili na ndio chanzo pia cha umasikini wa Taifa hili....

Tatizo liko hapa: wananchi tuko tayari kwa mabadiriko ila shida iko kwa hawa wanaohitaji tuwape nchi huku wanaonekana kabisa hawako tayari na wanahitaji miaka mingi ya kuwa tayari ikiambatana na mikakati mizito...CDM, ACT na vyama vingine vyote bado havijawa tayari kupewa nchi... vinahitaji kujijenga kitaasisi na kufanya uwekezaji mkubwa kwa watu, na rasirimali zake...bado wapinzani Tanzania hawajawa serious taasisi inayoweza kuaminika na kuongoza nchi kwa kushirikiana na taasisi nyinginezo... Kukabidhi madaraka sio kitu cha kubahatisha au kamari hapana hapa tunazungumzia maisha ya watu.

Historia kidogo: Mwalimu Nyerere wakati anapigania uhuru wa nchi hii na wazee wengine, waliifanya TANU kiwa taasisi kwanza yenye mizizi kila kona ya nchi na yenye watu wakuaminika na wazalendo kweli..vyama vingine pia viliundwa kwa mfumo huo ndio maana ilipozaliwa CCM imebaki taasisi imara mpaka kesho yenye kuanzia kutoka chini na vyanzo vingi vya mapato....mfumo huo wa CCM ukaenda mbali ndani ya CCM na mpaka leo wote tunaona nchi inatawalika kila mahala na serikali ipo kila mahala...Hii imekuwa nguzo kubwa ya usalama wa nchi hii na uimara wa CCM pia.

Siasa na usalama: Je CDM iko salama haina mamluki ndani yake? ina vitengo vya usalama makini, ina vitengo vya vetting, ina vitengo vya intelligensia ndani na nje? ina vyanzo vya kifedha vinavyotokana na uwekezaji wa wanachama wake na ruzuku nk?...
Hivyo vyote hapo juu vinatoa nguvu,kujiamini na kuaminika popote ndani na nje.

Nguvu hiyo inakufanya uaminike na deep state yapo matukio mengi ambayo yanaifanya jamii na deep state kitokuwa na confidence kwa CDM au upinzani wa Tanzania kupewa nchi.
 
Mpaka hiyo club billicanas kuwa chimbo la kuuza Unga pia imesababisha CCM?
Nadhani tungemuuliza Iddi Azan,Rizi1,Manji maana hao wote ni wana CCM na walitajwa kwny list ya Makonda(Mwana CCM) ya ma supplier wa hio mambo.
 
Mkuu umeongea vizuri sana haswa tuhuma za familia ya kina Mbowe kujihusisha na madawa ya kulevya, huu ni ukweli kabisa na usikute mpaka leo bado wanafanya hivyo. Usipende sana kushabikia kutawaliwa na viongozi waliosoma au kuombea Chadema kuja kushika hatamu hapa Tanzania kwani viongozi wengi waliosoma hawana machungu na taifa hili, believe me.
Unaongeleaje tuhuma za mtoto wa rais(the prince) kutuhumiwa kufanya biz ya madawa ya kulevya huku baba yake akiwa madarakani awamu Ile?
 
Kiukweli niliumia sana roho nikajisemea moyoni haiwezekani kiongozi anaruhusu ndani ya club yake biashara ya madawa ifanywe kuharibu vijana.
Mlikaririshwa na kina Bashite.. ungebaki tu CCM bi, Chokochoko bado anao mkeka wa TEUZI..😂😂
 
Kuna kipindi niliamini chama kitakachomkomboa Mtanzania ni Chadema ila nilikuja kubadilisha msimamo wangu nikaamua kushabikia CCM na sababu iliyonifanya niachane na upinzani ni kitendo cha Chadema kumsimamisha Lowasa 2015. Kiukweli niliumia sana roho nikajisemea moyoni haiwezekani kiongozi anaruhusu ndani ya club yake biashara ya madawa ifanywe kuharibu vijana.

Basi ikawa hivyo nikaamua tu kuwa upande wa CCM na kufurahia anguko la CHADEMA japo katika uchaguzi mkuu sikuunga mkono namna uchafuzi uliotokea ule haukua uchaguzi mimi mwenyewe nilikuwa msimamizi msaidizi wa kituo niliyoyaona yanasononesha.

Ila kwa sasa nimekuja kujua CCM ndio wanaotuchelewesha na kutuumiza. Sababu kubwa ni chama cha CCM kimejaa darasa la Saba wa kutosha nenda katika ngazi za wilaya huko utaona viongozi wao ni watu wa namna gani lakini chadema Kuna watu waliosoma cha ajabu hawapewi nafasi.

Kikubwa naomba msamaha kwa yote tusameheane lakini kama ni mipango tuanze sasa hivi ya kuliokoa hili taifa ni heri tufe lakini kieleweke. Kama unaniunga mkono bonyeza like na kisha tupaze sauti popote mlipo muda umewadia kishindo kimefika tusidanganyike tena.
Mnafiq mkubwa wewe baki huko huko kwenye genge la wauaji na wezi wa kura
 
Kumbe ulikua mshabiki 🤔 BTW pole sana mkuu
 
Wewe ni wale wanasiasa malkayamalaya Chadema haiwezi kuikomboa nchi wasomi uliowaona Chadema ni kama hao kina mdude kweli are serious? Unachekesha sana mkuu
Pole Sana kwa mtazamo wako. Mayopian!
 
Rudi Chadema ji-brand vizuri ukipata umaarufu wa kisiasa ukaiva vizuri basi unarudi CCM unaramba teuzi fasta unawaacha wenzio wanaendelea kupayuka huko upinzani.short & clear.
 
Back
Top Bottom