Watanzania nawaomba tuache sifia Kila kinachotoka katika kinywa cha Rais tutaangamia wote

Watanzania nawaomba tuache sifia Kila kinachotoka katika kinywa cha Rais tutaangamia wote

Kipi kitakacho tuangamiza?? Kutaangamia kwasababu tunamsifia Rais ama??
Kwahiyo tusipo msifia tukimpinga, kumponda, kumpuuza, dharau, matusi n.k ndio tutakuwa salama??
Tushauri Sasa mkuu nani tumsifie badala yake.?
Mkuu watanzania kazi zao ni mbili tu
1. Kumlipa rais mshahara na marupurupu yake
2. Kumuongeza mkataba au kushitisha mkataba wake wa kazi
Hayo ya kusifia ni ujinga and unafiki.
 
Rais Magufuli ni nahodha bora
Nahodha Bora hujitosa vhombo kinapoenda mrama?Mbona kajifungia ndani(Chato)huku akisisitiza Sisi tufanye kazi.Yupo likzo/mapumziko ya zaidi ya mwezi sasa,hivyo ndiyo unapima ubora wake?
 
Mkuu watanzania kazi zao ni mbili tu 1. Kumlipa rais mshahara na marupurupu yake
2.kumuongeza mkataba au kushitisha mkataba wake wa kazi
Hayo ya kusifia ni ujinga and unafiki.
Japo tumemuandika kazi Raisi Magufuli lakini hatuna uwezo wa kumwajibisha katika kipindi akiwa Raisi wetu na hata akishastaafu.Ni mfalme kwa katiba tulio nayo.

Ukiongezea wabunge na madiwani wa upinzani waliounga mkono na kuhamia CCM hakamatiki.

Kama hiyo haitoshi bunge ni mali ya CCM ambaye Magufuli ni mwenyekiti wake huwezi kuwaza impeachment hata kidogo.
Kama ulitegemea CC na NEC ya chama kumhoji au kumwadabisha sahau kabisa,kaifumua kabisa CC na NEC na kuondoa mbegu za JK.hata wale walionekana bado wana ndoto za akina Bernard Membe wameishafyata mikia,wanaendelea kuunga juhudi za Raisi.

Subiri 2025 atakapomaliza ngwe yake ya kipindi cha pili, lakini akiamua kuongeza miaka miwili hadi mitatu ili kukamilisha miradi iliokumbwa na majanga ya Corona umma utaunga mkono.

Kwa ufupi bila katiba mpya tutegemee huruma ya mtawala.
 
Soma vizuri makala yangu. Sijamkandia nasema kutokana na wakati. Je tukae kimya au tuwe kama akina Mwigulu ili kesho tuwe wajinga?
Ujinga wa Mwigulu uko wapi?. Na huo ujinga umeanza kuuona lini? Kwa taarifa yako ni kuwa wateuliwa wa Rais wako hawajawahi kuwa wajinga hata siku moja, ila wanafanya vile boss wao anataka na anavyopenda, sasa hapo mwenye matatizo ni mteuliwa au mteuaji?
 
Back
Top Bottom