Na mimi nasema hivi...
tatizo nchi si mali ya CCM ni ya Watanzania so wao ndio wataamua uelekeo wao. Yaani watu wapumbavu kama nyie mliojaa unafiki, hamjui mnakoipeleka hii nchi yetu!
The Sunk Cost Fallacy, naomba nikuulize maswali kadhaa...
- Je unajua Magufuli angekua hai hadi hii leo, makamu wake angeendelea kuwa huyu huyu Rais wa sasa?
- Je unajua kuwa Kiongozi Mkuu wetu wa sasa hakupigiwa kura na Watanzania kuwa Rasi wao!
- Je baada ya kifo cha Magufuli ilikuwakuwaje hadi aliyekuwa Makamu wa Rais akawa Rais?
The Sunk Cost Fallacy, kabla hujajibu maswali yangu naomba nikusaidie kidogo...
Tanzania tuna kitu kinaitwa Katiba...nguvu ya Katiba ndiyo ilimwezesha kuwa Rais.
Hebu kwanza sikiliza hiki kiapo...
Swali la nyongeza...kama hii Katiba aliyoapa kuiheshimu, kuitetea na kuilinda kwa makusudi akaamua kuisigina, je tuna tumaini gani huko mbele ya safari?
Kwa nini hadi leo kazuia mikutano ya vyama vya siasa kinyume na matakwa ya Katiba, je ni kwa sababu hataki wananchi wapate mawazo mbadala?
Kama hili jambo dogo tu kashindwa, huo uchaguzi huru ambao unaweza kumuondoa madarakani atauruhusu? Naomba tuwe wa kweli, tuache unafiki.