Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pia nchi hii huwezi igeuza mali yako, acha Mungu atuamulie hatma yetuNchi hii kamwe haitafuga maharamia Acha washinde mahakamani
Mkuu kosa La jf ni nn.unawaonea.hapa jf ni maoni ya RAIA.unazuiaje maoni ya watu.Nachoogopa ni kitu kimoja tu! Kwanini moderators hawafuti au kuzuia hizi post!!!???
Kuna baadhi ya post za fununufununu zinazoleta taharuki huwa hazikai hata dakika moja! Kwanini hizi zinaachiwa tuuu!?!? Au moderators wametekwa!!!?
Hakika safari hii Jamiiforums wakipona, watu waache kulalamika eti hakuna uhuru wa kutoa maoni!!
Utakuwa ni uoga wao tu na uzushi na uzandiki
Mi nawasoma na kuwashangaa.Idiot kabisa. Kwa taarifa yenu rais yupo mzima wa afya.
mara nyingi nakuaga pande wa upinzani. Lakini hata kama humpedi Magufuli kiasi gani huwezi ukachekelea kuumwa kwake hadharani. Hata kama moyoni kwako unataka iwe hivyo, sio kitu smart kuonyesha hisia hizo kwa umma, ni kosa moja kubwa sana kisiasa.
Ndio maana hata Tundu Lissu alipopigwa risasi Magufuli alitweet kumpa pole, japo naamini serikali yake inahusika, lakini alifanya kinachotakiwa kufanywa na mwanasiasa. Hutakiwi kushangilia ugonjwa wala kifo cha mpinzani wako hadharani.
Walichonishangaza zaidi hawa Wapinzani walikuwa wakichekelea wakati hata mtu mwenyewe haijulikani kama ana afya kweli ama mgonjwa, sasa ukishangilia halafu mtu akajitokeza mzima kabisa utajificha wapi?
Najua ni viongozi wachache wa Upinzani wamefanya hivi, lakini wapinzani wanapaswa kufundishana namna ya ku behave mbele ya public, samaki mmoja akioza watatangaza mmeoza wote, wanaangaliwa na watu wengi, na kila wanachoandika watu wanaki judge.
Hapa wanawafanya CCM kama akina Musiba hivi kuaminika zaidi kuwa Wapinzani wapo kwa ajili ya kumduru magufuli na wanashirikiana na mabeberu kufanya hivyo, yaani wanajipiga risasi ya mguuni kama sio kichwani kabisa.
Wamenisikitisha sana
Ana matako yakukalia bench? Chuma kimekuwa urojoNjoo st. Peters hapa mimi ndo niko hapa chuma kinasali hapa leo
Hata mimi jana nimepiga bia hatari sana, yani jumla nimtumia kama laki mbili hivi, Mungu ni mwemaKtk wanawake niliokuwa nawaheshim humu ni pamoja nawewe,ila ktk hili swala naona unajitoa akili sijui kwanini! Hivi unawezaje kufurahiya matatizo ya mtu mwengine? Tena yaugonjwa?
Kwani yeye ni mtu. Alishakuwa mnyama siku nyingi sana.Nawashangaa kwa kumuombea mabaya binadamu mwenzio,hata kama unamchukia kiasi gani,lakn inapofkia kumuombea kifo,hapo utu unakuwa umekutoka....u become an animal or something far than that!
Seriously?Honestly last week I had a dream of a farewell mass of mr President at St Joseph Cathedral. Mama Janet was wrapped ya in vitenge.
Hawajaanza kujidhihirisha leo, wameanza kitambo hasa ilipoanza awamu hii ya tano!!!!Hizi siku chache watu wenye roho mbaya na chuki iliopitiliza wanajidhihirisha
Mbona hata mimi nilipiga bia za kutosha, shida hapo ni nini?Hii comment naona kama hujaizingatia sana ndugu ila haifanani na mtu mwerevu kama wewe!
Una ushahidi gani kama ni wapinzani wanafanya hayo? Kama wapinzani ni wadudu basi maccm ni mataahira.Nilipata Ghadhabu sana, nikiwa kama mdau wa Demokrasia na haki za binadamu kuona kuna kiongoz anathubutu kuwaita Watanzania wenzake "wadudu " tena mbele ya kadamnasi na mbele ya media
Niliona hii ni dalili nyingine ya vijana walio aminiwa na Mh Rais JPM, lakin wanajimwambafy na kujivika mamlaka wasio kuwa nayo
Ila leo nimeamini jamaa hakukosea sana, nafuta kauli zangu za kejeli nilizotoa kwake siku ile,
Na inawezekana neno wadudu lilikuwa ni understatement
Nimeelewa kuwa
1)Ni Wadudu tu, wanaoweza kushinda mitandaoni wakifurahia jambo na wakifurahia au kusubiri kwa hamu ujio wa taarifa mbaya za mwanadamu mwenzao, tena kiongoz wao. Na tena wadudu hao sio jamii ya Nyuki, Siafu au jamii nyingine ya wadudu wenye akili, siafu, Nyuki na baadhi ya wadudu wana upendo, Ushirika, uzalendo kwa makundi na vichuguu vyao kuliko wapinzani wa Tz, wanaheshimu viongozi wao balaa, nawaza labda wadudu jamii ya nzi,mende na wengineo ambao hawana ustaarabu wa kuishi kijamii ndo watakuwa na sifa za wapinzani tulio nao Tz.
2) Ni wadudu tu ndo ambao kila kitu hupiga kelele ,liwe jema au baya, Mchukulie nzi, kutwa kucha yeye ni nzeee, nzeee, nzeee, anapiga kelele, anacholilia hukion, hujui kuwa anafurahia au anahuzunika, na mbaya zaid ni kuwa anapiga kelele bila kufanya hatua yoyote, Nzi hang'ati,
Ni aheri kama nyuki, akitulia anatengeneza asali, ukimzingua anapiga yowe kidogo, huelewi anang'ata. Sasa kuwalinganisha wapinzani wa Tz na wadudu aina ya Nyuki sio sawa, hawa hawang'ati ,na wala hawatengenezi asali ,kazi kupiga domo tu, yee yee yee ,hawa ni wadudu jamii ya nzi na mende
3)Ni wadudu tu ambao watakuwa na usahaulifu kama walio nao wapinzani wa Tz
Juzi juzi tu mtu wanae muona leo ni hero kwa kuwaletea habar za uzushi, alikuwa ameweka kambi la mashambulizi kwa mwenyekiti wao,
Mwenyekiti wao hajajibu hata hoja moja, na wala halijawa tatizo, leo hii mtu huyo kazusha ya kuzusha, Msigwa ameendelea na majukumu yake ya kutangaza teuzi, wanabak wanalalama, mbona tuhuma hazijawekwa sawa? Wadudu mbona mnakuwa wasahaulifu? Tuhuma za mwenyekiti mliweka lini sawa? Na imagine tuhuma za mwenyekiti zilikuw zinahusu majukumu yake ya kazi, tuhuma hiz za leo ni binafsi (afya ni mambo binafsi) .
Au ndo muendelezo wa yale yale ya double standards, chama mnataka kitawaliwe kidikteta, miaka nenda rud,mwenyekiti ni huyo huyo, et hakuna mwingine mwenye vigezo, ila mkiambiwa na sisi kama nchi hatuoni mwenye vigezo vya kumpokea JPM tunataka aendelee, mnaanza kung'aka kuwa haiwezekani ktk watanzani m50 akosekane mwenye vigezo, wadudu mbona mnashindwa kutumia logic ndogo tu?
Hivyo kwa heshima na taadhima, naomba nimtake radhi yule mheshimiwa alie waita wapinzani wa Tz kuwa ni wadudu, sababu siku ile nilimlaani vikali kwa kutumia maneno yasiyo na staha kwa watanzania wenzake
Ila kwa yanayoendelea leo, yamenifanya nitafakari, na kugundua kuwa jamaa alikuwa anajua kitu cha ziada ambacho mimi sikuwa na najua kwa wakati ule
Hivyo namtaka na kumtia moyo, ajitokeze aongezee na kutolea ufafanuzi kwa msisitizo kuwa wapinzani wa Tanzania ni wadudu wa jamii ya nzi Na mende, sio wadudu wa jamii zinazojielewa kama Siafu wanaopiga kazi balaa(hapa kazi tu), nyuki wanaotengeneza asali (wanaunga mkono serikali ya viwanda) Vipepeo wanaoruka na kusaidia ktk pollination (kama Bombadier zetu tu)Na wadudu wengine wa aina hii.
Viva JPM, Viva Tanzania.
UNAWEZA UKATUSAIDIA HIYO PICHA IMEPIGWA MWAKA GANI? KUNA JAMAA HAPA ANASEMA MWAKA 99.Mzuqa!
Hii Lugha ya malkia kweli ilikuja na meli. Hule mlingoti wa kupeperusha bendera nilidhani unaitwa tu flagpost kwa Kiingereza kumbe hata jina la mast linatumika kwa mfano the flag is flying half mast yani nusu mlingoti.
Aidha Kiingereza kinachanganya zaidi unaweza kutamka neno moja lakini ikawa na tofauti katika maandishi mfano morning na mourning.
Waiter kaa stendby!
View attachment 1238717
Cc Etwege Magonjwa Mtambuka
Sikuona comment yako Lisu aliposhambuliwaNaweza nisikubaliane na mambo yanavyoenda lakini siwezi kuunga mkono uchuro Wa kuombeana maovu kwa binadamu mewenzangu. Na kwa maombi yauovu tujue Mungu hapangiwi. Mungu anaweza kuwageuzia kibao wanaoomba yeyote apate yaysiypstahii.
Si atokeze sasa. Alivyompenda masifa angekuwa na afya njema ungemuona kwenye vyombo vya habari.Idiot kabisa. Kwa taarifa yenu rais yupo mzima wa afya.