Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Ni siku ya tatu leo kumekuwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya watuamiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu afya ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania alipokuwa ktk ziara mikoa ya kusini.

Na wengine kufika mbali kabisa kwa kuzusha kabisa taarifa za kifo kitu ambacho baadhi ya wapinzani wa kasi ya awamu ya tano wamekuwa wakifurahi na kushangilia katika mitandao na kuleta taharuki majumbani na mitaani kiasi watu wengi kuuliza Nini kinaendelea.

Taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na watz ndani na nje ya nchi wakati Ikulu haijatoa taarifa yoyote kuhusu kuwa Rais ni mgonjwa.

Nadhani tuna sheria na kanuni kuhusu kutoa taarifa hasa zinazohusu usalama wa nchi Sasa hawa wanaotoa taarifa za kuzusha tu toka katika chanzo ambacho hakijulikani na kuleta taharuki wanatakiwa kufanywa Nini na mamlaka husika kisheria.

Nadhani mamlaka husika Kuna haja ya kutoa mtu mmoja kama mfano ili liwe fundisho kwa wengine wenye nia kama hii.

Ukisoma mitandao ya kijamii ndiyo utajua Nini kinasambazwa na kuleta maneno chini kwa chini na taharuki mpaka makanisani watumishi wameanza maombi ya kukemea kinachoendelea.

Kama huna taarifa acha kuzusha taarifa na kama una taarifa sahihi basi jitoe muhanga kwa kutoa taarifa kamili inayoeleweka sio kutoa taarifa za kuwachanganya watz.

Watz wengi wanaelewa sana nia mbaya za watu kwa serikali hi na kama ndiyo kutafuta mtaji wa kura ktk uchaguzi wa November basi hapo mmepata zero kabisa.

Watu wa Cyber happy mna kazi ya kufanya kuondoa uchafu kama huu katika nchi yetu.

Ni muhimu kuwa na taarifa za kweli kuliko uzushi.....tena wakome wote wenye nia mbovu na Serikali.
Yaani hapa kunawatu wanavutiwa time kwenye huu mtego we utaniambia watapotezwa watu mpaka tunyooke. Nawasihi watanzania wasiandike vibaya itawagharimu
 
Mbona leo lugha zilizotawala ni za mafumbomafumbo tu,kuna nini?.
 
Acheni kupotosha watu tulikuwa tunafuwatilia msafara mwanzo mwisho.

Shida ilianza Masasi na sina uwakika kama watu wanao angalia afya ya Rais waliona lile tukio sisi tulio kuwa mbali tuliona kabisa baada ya pale msafara uliondoka na kwenda kijijifulan baadae ukarud ila Rais aliondoka ktk njia ambayo mpaka sasa no one know wala siwezi kuandika hapa as nimfuwasi wa kuto toa kila siri.

Usiku ule ambao nyie mnauliza yupo wapi Taifa lilikuwa kazini na nina dhani hakuna alie lala.

Ila Taifa letu lina tunu yaaman na upendo huwez amini watu walikuwa wamoja kuliko hii mambo ya mtandao kiukweli natamani kulia ila Wazee wetu amabo ni top secret number one wanampenda sana kijana wao kiukweli sina uwakika kama kuna chama kina unity kama ccm.

Nataman kulia ila navipongeza vyombo vyote vya ulinzi na usalama na top secret ya Rais kiukweli hawa ni mashujaa shime serikali yangu na taifa langu.

Tuache upotoshaji... Japo from now Rais atapunguza Ratiba za kaz nyingi nakupata muda wakupata mapumziko. Pia kam mnkumbuka anamualiko wa German kamamnakumbuka sim ya Angel kwa Rais..
Wewe mleta mada nimnafiki Sana yaan badala ya kuwamasisha watu tumuombee raisi wetu mpendwa ili asipatwe na majalibu yoyote,

Wewe unakuja na ngonjela za mialiko mialiko inasaidia Nini kwa wakati Kama huu, watanzaia sisi niwamoja na Rais wetu mungu atamtangulia kwa Kila jambo
 
Kuna tweet inasema Leo kafungua macho
Mungu ali
Nimeanza na Konyagi Mbuzi anachomwa vizuuri kabisa na nimeongea na mtaalam wangu huko Tanga nimemwambia vipi hii akasema kitu cha Kusini kimezama deep

Nikamwambia kama anaweza na yeye kupigilia msumari wa moto akacheka sana
Nguvu za giza zimeshindwa nguvu kabisa.tulishamuombea ataishi hatakufa
 
Eeeee mungu msaidie mjori wako mh.jpm arejee katika afya yake,mabaya yote yanayonenwa dhidi yake yasimfike.Wasamehe wale wote wanao mwinukia.Amen
Kumbe kuna binadamu wenye akili kiasi hiki.... Basi kumbe watanzania wanao uwezo mkubwaa wa kufikiri.... Sema hawajulikanagi... Hata ukitumia hisia tu unaweza kujua jambo...

Shida na yy alikufuru mbele ya viumbe wa mungu... Alisema kamsamehe nape madhambi yake... Sasa c mungu ndio anaye samehe mtu dhambi.. Mara aseme kama nikifa leo hakuna wa kuja kufanana na mm..

Mzee wangu kanisimulia kwamba, hata nyerere aliwahi kukufuru kwenye mkutano wa CCM kwamba hata rais wa awamu ya nne nitamuona... Atanikuta nikiwa hai... Ndio hivyo mungu akamchukua mapema...

Kwa jinsi ninavyomjua mungu wa kweli.. Muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo... Mungu wa milele, mfalme wa wafalme... Bwana wa mabwana... Baba mtakatifu... Mungu aliye hai milele na milee... Alfa na omega... Huwa havumilii mtu anapochukua nafasi yake kwa wanadamu.... Immediately huwa anafanya jambo kukufundisha kama atakupenda... Au anakupa adhabu ya moja kwa mojaa.. Kama ataona huna muda wa kujifunza...

Hivi vitu vipo... Wala msijisahau... Kujimwambafy maana yake ni kujiinua na kuliko kawaida... Kikwete alisema alikuwa hujui kama katumiwa na mungu kumjulishaa. Mungu amsamehe kama nyie mtaonesha moyo wa kumuhitaji.... Kama mtamuombea mabaya kwa mungu.... Anaweza kuwajibu mpaka mkashangaa... But mm naomba mungu umpe muda tena kiumbe wako.... Ajifunzee... Usimchukue mungu wetu mwenye rehema... Unayetoa nafasi ya pili.... Tunaomba umpe muda tena.
 
Eeeee mungu msaidie mjori wako mh.jpm arejee katika afya yake,mabaya yote yanayonenwa dhidi yake yasimfike.Wasamehe wale wote wanao mwinukia.Amen
Linafiki tu hili mkuu halina jipya zaidi ya kusubiri #breaking new, ndio maana kila muda lipo online kutegea.
 
Ni kama utamaduni au siasa ya aina fulani iliyozoeleka kila siku takatifu ya Jumapili kuona taarifa za wapi Rais wetu mpendwa ameswali, lengo kubwa huenda lilikuwa kututaarifu juu ya uimara wa Rais wetu katika maswala ya imani yake au kutaka kutuonyesha kuwa Rais ni mtu wa Mungu kwelikweli na kila kitu anachofanya basi anaongozwa na Mungu na yeye ndio muongozo wake.
Sasa tunataka kujua leo kaswali wapi na je nyinyi waumini kuna mtu kaswali naye huko?
Ni kusali sio kuswali, mkuu
 
Hivi wale waliochangamka kupinga uwepo wa ugonjwa wa zika nchini wapo wapi watusaidie kwenye hili?🤨
 
Ansbert Ngurumo,Evarist Chahali,Zitto Kabwe,anayejiita Kigogo2014,Anayejiita Mcomoro no unataka Nani mwingine
Kuugua kwa binaadamu yeyote achilia mbali viumbe vingine ni kawaida na si hatari kwa taifa. Na ndiyo maana tuna katiba iliyo tambua uwepo wa ugonjwa katika majukumu ya Rais . Achilia mbali kuwa tunaye makamu wa Rais, ambaye wamepigiwa kura pamoja . Kwa hiyo hakuna hatari kwa taifa [emoji120]
 
Ingekuwa very simple. Kwa vile Mhe Rais ni mzima wa afya, hata kama amepumzika baada ya safari ndefu, angepangiwa dakika kumi tu. Aende pale kanisani anaposali, waandishi wa habari wakiwepo. Apewe mic aongoze sala fupi kama anavyofanya maeneo mengine. Asalimie watu awaambie "Jamani wananizushia tu mimi ni mzima kabisa. Ila nimechoka kwa ziara ndefu niliyokuwa nayo
bila kupumzika. Nikaamua kuikatiza. Paroko naomba nikapumzike". Halafu aondoke. Nakwambia kanisa zima na Watanzania wote wangemshangilia na kumwombea Mungu amtie nguvu. Halafu vyombo vya dola ndio vianze kushughulika na hao waliotunga huo uongo na kumzushia rais wetu mpendwa kifo. Lakini kusema ni uongo bila kueleza ni kwa nini alikatisha ziara na yeye haonekani hadharani ndio uongozi wanazidi kuwatia watu hofu. Kama ni mgonjwa litolewe tamko. Kwani kuumwa si kawaida ya binadamu wote? Nyerere alipopelekwa St Thomas Uingereza si watu waliambiwa? Kikwete alipoenda kutibiwa Marekani si tuliambiwa? Kwani kama hayupo nchini kuna shida gani? Si kuna wasaidizi wake ambao wanatekeleza yale majukumu yake?
 
.
Screenshot_20191020-151027.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom