Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Nikiwa Kama mkulima naona Hali ya hewa imekuwa siyo nzuri, inatutisha wakulima, inatupa wasiwasi, mashaka na hofu. Mpaka Leo tunapoelekea kuumaliza mwezi huu bado hatujaona mvua, bado ardhi Haijapata mvua, bado tunaendelea kuangalia angani kila kukicha kuona Hali ya mawingu, Bado ardhi Ni ngumu Sana, bado imekauka Sana, Bado majembe yetu yanatuumiza mbavu na kuchosha miili yetu wakati huu tunapo endelea kulima taratibu wakati tunasubili mvua
Ikumbukwe kuwa mpaka mwezi huu sisi wakulima hasa huku mkoani Songwe huwa tunakuwa tumepata mvua ambazo huwa tunasema kuwa Ni mvua za kahawa, lakini mpaka Sasa mvua hizo hazijanyesha katika maeneo mengi na hivyo kuwaathiri na kutetelesha wakulima wa kahawa hasa wilaya yetu ya Mbozi,
Sote Tunajuwa kuwa asilimia kubwa Sana ya watanzania wanyonge tunategemea kilimo Cha mvua, Mvua ndio kila kitu kwetu, ndio mrija wa hewa kwetu, ndio jeuri yetu, Ndio fahari yetu, hatuoni shida kulima huku mvua ikinyesha maana tulishazoea kufanya hivyo,
Mbele za Mwenyezi Mungu Hakuna lisilo wezekana, Hata Hili linawezekana mbele za Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Fadhira ambaye amekuwa akituvusha katika nyakati zote ngumu tulizowahi kupitia Watanzania, Mungu wetu Ni msikivu na Mwenye upendo Na sisi Watanzania, Mungu wetu Hawezi kutuacha, Tupige magoti Tumlilie kwa Imani zetu ili apokee maombi yetu, Tujongee na kujinyenyekeza mbele zake, Twendeni mbele zake tukiwa Tumelibeba Taifa letu mabegani mwetu ili Tukamkabidhi mikononi mwake,
Mvua Ni Neema na baraka kwetu watanzania, Tunahitaji Baraka na Neema hizo kwa Sasa, Tunahitaji mkono wa MWENYEZI MUNGU uweze kushusha neema ya mvua hapa nchini, Tunahitaji mvua ili mabwawa yetu ya maji yajae ili tupate umeme wa uhakika wakati wote na kuliangazia Taifa letu saa 24, Tunahitaji mvua ili tupate maji Safi na salama kwa ajili ya matumizi yetu watanzania
Sanjari na Hilo tuhakikishe tunatunza mazingira yetu kwa kadri ya uwezo wetu, tupande Miti katika maeneo yetu , tusikate Miti hovyo Wala kuchoma misitu yetu, tusilime kando kando ya vyanzo vya maji yetu na tupeana elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu wakati wote, Tuyatunze na kuyalinda mazingira yetu kwa nguvu zetu zote na kwa gharama zote ili yatutunze na kutulinda zidi ya mabadiliko ya Hali ya hewa
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania wanyonge kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu