Watanzania Tufanye Maombi ya Kitaifa kumwomba Mwenyezi Mungu atupatie Mvua zenye Baraka na Neema

Sijaongelea habari za akina Mnyika hapa, maana suala lililopo hapa halichagua chama Cha mtu na Wala halihitaji kuleta uchama hapa, uwe unajuwa masuala ya kitaifa
Namaanisha hiyo nguvu inayotumika huko barabarani tuitumie kufanya mkesha wa kuomba mvua....
 
Ndugu zangu Nikiwa Kama mkulima naona Hali ya hewa imekuwa siyo nzuri, inatutisha wakulima, inatupa wasiwasi,mashaka na hofu. Mpaka Leo tunapoelekea kuumaliza mwezi huu bado hatujaona mvua, bado ardhi Haijapata mvua, bado tunaendelea kuangalia angani kila kukicha kuona Hali ya mawingu, Bado ardhi Ni ngumu Sana, bado imekauka Sana, Bado majembe yetu yanatuumiza mbavu na kuchosha miili yetu wakati huu tunapo endelea kulima taratibu wakati tunasubili mvua

Ikumbukwe kuwa mpaka mwezi huu sisi wakulima hasa huku mkoani Songwe huwa tunakuwa tumepata mvua ambazo huwa tunasema kuwa Ni mvua za kahawa, lakini mpaka Sasa mvua hizo hazijanyesha katika maeneo mengi na hivyo kuwaathiri na kutetelesha wakulima wa kahawa hasa wilaya yetu ya Mbozi,

Sote Tunajuwa kuwa asilimia kubwa Sana ya watanzania wanyonge tunategemea kilimo Cha mvua, Mvua ndio kila kitu kwetu, ndio mrija wa hewa kwetu, ndio jeuri yetu, Ndio fahari yetu, hatuoni shida kulima huku mvua ikinyesha maana tulishazoea kufanya hivyo,

Mbele za Mwenyezi Mungu Hakuna lisilo wezekana, Hata Hili linawezekana mbele za Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Fadhira ambaye amekuwa akituvusha katika nyakati zote ngumu tulizowahi kupitia Watanzania, Mungu wetu Ni msikivu na Mwenye upendo Na sisi Watanzania, Mungu wetu Hawezi kutuacha, Tupige magoti Tumlilie kwa Imani zetu ili apokee maombi yetu, Tujongee na kujinyenyekeza mbele zake, Twendeni mbele zake tukiwa Tumelibeba Taifa letu mabegani mwetu ili Tukamkabidhi mikononi mwake,

Mvua Ni Neema na baraka kwetu watanzania, Tunahitaji Baraka na Neema hizo kwa Sasa, Tunahitaji mkono wa MWENYEZI MUNGU uweze kushusha neema ya mvua hapa nchini, Tunahitaji mvua ili mabwawa yetu ya maji yajae ili tupate umeme wa uhakika wakati wote na kuliangazia Taifa letu saa 24, Tunahitaji mvua ili tupate maji Safi na salama kwa ajili ya matumizi yetu watanzania

Sanjari na Hilo tuhakikishe tunatunza mazingira yetu kwa kadri ya uwezo wetu,tupande Miti katika maeneo yetu , tusikate Miti hovyo Wala kuchoma misitu yetu, tusilime kando kando ya vyanzo vya maji yetu na tupeana elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu wakati wote, Tuyatunze na kuyalinda mazingira yetu kwa nguvu zetu zote na kwa gharama zote ili yatutunze na kutulinda zidi ya mabadiliko ya Hali ya hewa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania wanyonge kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Rubbish
 
Mkuu Mimi Ni mtu wa maombi Sana na Mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu Ndio maana unaona hata michango yangu humu haina matusi Wala dharau, ndio maana unaona hata ukinitukana Mimi siwezi nikakutukana maana moyo wangu umejaa hofu ya Mwenyezi Mungu

Kwa tabia yako ya kutetea mabaya ya CCM na kukataa kusema ukweli wewe sio mtu wa maombi. Mtu wa maombi hukemea maonevu na kusema ukweli muda wote.
 
Nani amekutukana na ni lini nimekutukana. Shida yako ukiambiwa ukweli unasema umetukanwa. Mimi nasisitiza maombi na uchawa havikai sehemu moja.
 
Hapana mkuu kwa upande wako haujawahi kunitukana na Wala sijasema kuwa wewe umewahi nitukana, lakini pia naelewa tofauti ya kukosolewa na kutukanwa
 
Kwa tabia yako ya kutetea mabaya ya CCM na kukataa kusema ukweli wewe sio mtu wa maombi. Mtu wa maombi hukemea maonevu na kusema ukweli muda wote.
Hapana mkuu Mimi nasema ukweli wa wazi kuwa CCM ndio Tumaini la Watanzania nikiwepo mini mwenyewe Hilo siwezi nikakataa na nitaendelea kuitetea CCM wakati wote maana Ni chama kilichoonyesha kuwa na uchungu na maisha ya watanzania
 
hili jukwaa zamani lilikuwa na vichwa kwelikweli ma great thinker, kwa sasa wamevamia vijana wenye macho mekundu,kila uzi unaowekwa hapa wao ni kuupinga tu !mtoa mada katoa wazo zuri sana! ila kwa sababu vijana wengi humu wako mijini hata kushika jembe hawajui wanaona kila kiv ni taarabu!
 
Ndugu zangu Nikiwa Kama mkulima naona Hali ya hewa imekuwa siyo nzuri, inatutisha wakulima, inatupa wasiwasi,mashaka na hofu. Mpaka Leo tunapoelekea kuumaliza mwezi huu bado hatujaona mvua, bado ardhi Haijapata mvua, bado tunaendelea kuangalia angani kila kukicha kuona Hali ya mawingu, Bado ardhi Ni ngumu Sana, bado imekauka Sana, Bado majembe yetu yanatuumiza mbavu na kuchosha miili yetu wakati huu tunapo endelea kulima taratibu wakati tunasubili mvua

Ikumbukwe kuwa mpaka mwezi huu sisi wakulima hasa huku mkoani Songwe huwa tunakuwa tumepata mvua ambazo huwa tunasema kuwa Ni mvua za kahawa, lakini mpaka Sasa mvua hizo hazijanyesha katika maeneo mengi na hivyo kuwaathiri na kutetelesha wakulima wa kahawa hasa wilaya yetu ya Mbozi,

Sote Tunajuwa kuwa asilimia kubwa Sana ya watanzania wanyonge tunategemea kilimo Cha mvua, Mvua ndio kila kitu kwetu, ndio mrija wa hewa kwetu, ndio jeuri yetu, Ndio fahari yetu, hatuoni shida kulima huku mvua ikinyesha maana tulishazoea kufanya hivyo,

Mbele za Mwenyezi Mungu Hakuna lisilo wezekana, Hata Hili linawezekana mbele za Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Fadhira ambaye amekuwa akituvusha katika nyakati zote ngumu tulizowahi kupitia Watanzania, Mungu wetu Ni msikivu na Mwenye upendo Na sisi Watanzania, Mungu wetu Hawezi kutuacha, Tupige magoti Tumlilie kwa Imani zetu ili apokee maombi yetu, Tujongee na kujinyenyekeza mbele zake, Twendeni mbele zake tukiwa Tumelibeba Taifa letu mabegani mwetu ili Tukamkabidhi mikononi mwake,

Mvua Ni Neema na baraka kwetu watanzania, Tunahitaji Baraka na Neema hizo kwa Sasa, Tunahitaji mkono wa MWENYEZI MUNGU uweze kushusha neema ya mvua hapa nchini, Tunahitaji mvua ili mabwawa yetu ya maji yajae ili tupate umeme wa uhakika wakati wote na kuliangazia Taifa letu saa 24, Tunahitaji mvua ili tupate maji Safi na salama kwa ajili ya matumizi yetu watanzania

Sanjari na Hilo tuhakikishe tunatunza mazingira yetu kwa kadri ya uwezo wetu,tupande Miti katika maeneo yetu , tusikate Miti hovyo Wala kuchoma misitu yetu, tusilime kando kando ya vyanzo vya maji yetu na tupeana elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu wakati wote, Tuyatunze na kuyalinda mazingira yetu kwa nguvu zetu zote na kwa gharama zote ili yatutunze na kutulinda zidi ya mabadiliko ya Hali ya hewa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania wanyonge kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

Ujinga mtupu na full rubbish.
 
Kwa tabia yako ya kutetea mabaya ya CCM na kukataa kusema ukweli wewe sio mtu wa maombi. Mtu wa maombi hukemea maonevu na kusema ukweli muda wote.
Kinacho nishangaza na kunitisha, hawa watu wanaojiita wana maombi na wenye hofu ya Mungu lakini wa sasa.. nitabia yao ya JAZBA.. ukiongea kinyume na wanachoamini wana jaa upepo hadi unajiuliza wanahofu ya Mungu yupi maana miungu wako wengi....
 
Tutaomba sana lakini tukiwa hatuna mipango mizuri hakuna mabadiliko yatakayotokea
 
Mipango mikakati Ni pamoja na kuweka juhudi endelevu za ulindaji na utunzaji wa mazingira yetu,ikiwemo upandaji Miti wa kutosha na utolewaji wa Elimu ya mazingira pamoja na utekelezaji wa Sheria za ulinzi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji
 
Ndugu zangu Nikiwa Kama mkulima naona Hali ya hewa imekuwa siyo nzuri, inatutisha wakulima, inatupa wasiwasi,mashaka na hofu. Mpaka Leo tunapoelekea kuumaliza mwezi huu bado hatujaona mvua, bado ardhi Haijapata mvua, bado tunaendelea kuangalia angani kila kukicha kuona Hali ya mawingu, Bado ardhi Ni ngumu Sana, bado imekauka Sana, Bado majembe yetu yanatuumiza mbavu na kuchosha miili yetu wakati huu tunapo endelea kulima taratibu wakati tunasubili mvua

Ikumbukwe kuwa mpaka mwezi huu sisi wakulima hasa huku mkoani Songwe huwa tunakuwa tumepata mvua ambazo huwa tunasema kuwa Ni mvua za kahawa, lakini mpaka Sasa mvua hizo hazijanyesha katika maeneo mengi na hivyo kuwaathiri na kutetelesha wakulima wa kahawa hasa wilaya yetu ya Mbozi,

Sote Tunajuwa kuwa asilimia kubwa Sana ya watanzania wanyonge tunategemea kilimo Cha mvua, Mvua ndio kila kitu kwetu, ndio mrija wa hewa kwetu, ndio jeuri yetu, Ndio fahari yetu, hatuoni shida kulima huku mvua ikinyesha maana tulishazoea kufanya hivyo,

Mbele za Mwenyezi Mungu Hakuna lisilo wezekana, Hata Hili linawezekana mbele za Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Fadhira ambaye amekuwa akituvusha katika nyakati zote ngumu tulizowahi kupitia Watanzania, Mungu wetu Ni msikivu na Mwenye upendo Na sisi Watanzania, Mungu wetu Hawezi kutuacha, Tupige magoti Tumlilie kwa Imani zetu ili apokee maombi yetu, Tujongee na kujinyenyekeza mbele zake, Twendeni mbele zake tukiwa Tumelibeba Taifa letu mabegani mwetu ili Tukamkabidhi mikononi mwake,

Mvua Ni Neema na baraka kwetu watanzania, Tunahitaji Baraka na Neema hizo kwa Sasa, Tunahitaji mkono wa MWENYEZI MUNGU uweze kushusha neema ya mvua hapa nchini, Tunahitaji mvua ili mabwawa yetu ya maji yajae ili tupate umeme wa uhakika wakati wote na kuliangazia Taifa letu saa 24, Tunahitaji mvua ili tupate maji Safi na salama kwa ajili ya matumizi yetu watanzania

Sanjari na Hilo tuhakikishe tunatunza mazingira yetu kwa kadri ya uwezo wetu,tupande Miti katika maeneo yetu , tusikate Miti hovyo Wala kuchoma misitu yetu, tusilime kando kando ya vyanzo vya maji yetu na tupeana elimu juu ya utunzaji wa mazingira yetu wakati wote, Tuyatunze na kuyalinda mazingira yetu kwa nguvu zetu zote na kwa gharama zote ili yatutunze na kutulinda zidi ya mabadiliko ya Hali ya hewa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania wanyonge kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Mijalaana nyie waTanzania
 
Ukame ni kiashiria cha utawala uliokosa kibali mbele za Mungu.

Screenshot_20221030-153658.png
 
Sidhani kama Mungu atatusikiliza kwasababu wizi wa kura 2022 ulimchukuza sana.
 
Mtanikumbuka
 
Attachments

  • 2A39BE2E-68B2-46B2-8F95-C1C42AA83354.jpeg
    2A39BE2E-68B2-46B2-8F95-C1C42AA83354.jpeg
    87.7 KB · Views: 3
Viongozi waache rushwa mambo yawe sawa....

Mahakamani Kuna rushwa na haki zinageuzwa
 
Back
Top Bottom