Watanzania Tufanye Maombi ya Kitaifa kumwomba Mwenyezi Mungu atupatie Mvua zenye Baraka na Neema

Halafu zikinyesha nyingi tutarudi tena kumuomba atuepushe na mafuriko ...
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu na Mbwa Mwitu
 
Sawa mkuu Nimepokea ushauri wako Kama mwanaccm na nitaendelea kusoma maoni yako Kama navyo somaga siku zote
 
Aminaaaa Nashukuruuu Sanaa mkuu
 
Uharibifu mazingira afu utegemee Mungu akuletee mvua??....
 
Hapo kwenye huo wingi "utusamehe" naomba mimi nisijumuishwe

BTW endelea kumkumbusha atekeleze majukumu yake asijisahau sana mpaka watu waanze kumkubusha kumbusha kwa maombi
 
Halafu zikinyesha nyingi tutarudi tena kumuomba atuepushe na mafuriko ...
Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu na Mbwa Mwitu
Nimeandika kuwa tumwombe Mungu Atupatie mvua za Baraka na Neema
 
Unafikiri hayo maziwa na mito ipo kila mahali na kwa kila Shamba Hadi huku kwetu Mbozi? Umefikiria suala la gharama? Au unafikiri wakulima wote Ni matajiri na wenye uwezo wa kufanya kilimo Cha umwagiliaji? Umewahi kufika mashambani? Unajuwa yaliko mashamba? Unafikiri kwote Kuna hiyo mito?
 
Wewe kubali tu serikali yako ya ccm haina vipaumbele vya kueleweka! Na badala yake imewekeza zaidi nguvu kubwa kwenye siasa! Ingekuwa imewekeza kwenye kuwainua wananchi wake kiuchumi, nakuhakikishia tungekuwa mbali sana kama Taifa.

Halafi utambue gharama za kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji hufanyi wewe! Na badala yake hufanywa na serikali kupitia kodi yako, na pia ile mikopo kutoka nje na ambayo utatakiwa kuja kuilipa wewe na vizazi vyako. Hivyo usitafute visingizio mfu.
 
Hiki Ni kipindi ambacho serikali imeshuku kwa mwananchi na kumgusa moja kwa moja mwananchi, kwa kumtumikia na kumtatulia kero zake. Ni kipindi hiki ambacho serikali imejikita katika kuinua maisha ya mtanzania mnyonge, Ndio maana unaona hata katika kilimo namna serikali ilivyotoa mabillioni ya Ruzuku na kupelekea kushuka kwa Bei sokoni
 
Ujinga tu umetujaa, huo mkataba ni Biblia? mbona Ethiopia pamoja na matisho yooote wameendelea kujaza bwawa lao la Benishangul-Gumuz maji?..... kutwa kukimbizana na kina John Myika barabarani... ok ingalikuwa sisi ndo Marekani ungewaeleza huo upuuzi wa @!*&? MKATABA....
 
Jamani tunaangamia kwa kukosa maarifa.
Tabia ya nchi ikibadilika na sisi tunapaswa tuwe tayari kubadilika nayo. Wasomi wetu mahiri wako wapi?
Tabia ya watu nayo ibadilike maana ushoga unavyosambaa kwa kasi ndivyo ukame unazidi.
Tutubu makosa tuliyofanya katika uchaguzi wa 2020 maana kwa sasa tunavuna tulichopanda!
 
Unakata miti 2.7m alafu kesho unapiga magoti kumuomba Mungu inyeshe?
 
Sijaongelea habari za akina Mnyika hapa, maana suala lililopo hapa halichagua chama Cha mtu na Wala halihitaji kuleta uchama hapa, uwe unajuwa masuala ya kitaifa
 

Leo ndio umekumbuka Kuna maombi?.
 
Hatukufanya makosa 2020 Bali tulionyesha faida ya chama kuwekeza kwa wanyonge ambao ndio waliyopiga Kura kwa wingi
 
Mvua Tanzania hasa ukanda wa pwani zimeanza kuadimika hii miaka 3 baada ya mwehu mmoja kufyeka mamilioni ya miti ili awaletee umeme wananchi wake na wananchi wakamshangilia.
 
Leo ndio umekumbuka Kuna maombi?.
Mkuu Mimi Ni mtu wa maombi Sana na Mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu Ndio maana unaona hata michango yangu humu haina matusi Wala dharau, ndio maana unaona hata ukinitukana Mimi siwezi nikakutukana maana moyo wangu umejaa hofu ya Mwenyezi Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…