Watanzania Tujitokeze Kulaani na Kukemea Vikali kauli Chafu za Mdude Nyagali kwa Rais Wetu

Ndugu zangu Watanzania,

Nawaombeni Watanzania wenzangu na Wazalendo wa Taifa letu kujitokeza hadharani kulaani na kukemea vikali sana kauli Chafu za Mdude Nyagali kwa Rais wetu. Mtu huyu hatupaswi kumkalia kimya pasipo kutoa kauli na kumkemea pamoja na kumuonya vikali sana kuacha mara moja kutoa lugha chafu kwa Rais wetu.

Mtu huyu ambaye inaonyesha alikosa malezi mazuri utotoni mwake ameshajenga desturi na utamaduni wa hovyo na ambao haukubaliki hata kidogo.ambapo amekuwa akitoa lugha za udhalilishaji, kumshushia heshima Mheshimiwa Rais na Sasa amevuka mstari kuanza kutoa lugha za vitisho kwa Rais.

Inawezekana kwa akili yake na ulimbukeni wake,na kukosa kwake adabu na heshima akawa anafikiria labda anaongopwa au anaweza kufanya lolote lile au kutamka neno na maneno yoyote yale pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Anaweza kuwa anafikiria wote wana akili za aina yake za kuunga mkono ujinga wake.

Watanzania hatupo tayari kumvumilia wala kuona mtu akimtishia Rais Wetu au kumtukana, kumfedhehesha au kumtweza utu wake au kumshushia heshima bila sababu. Ni lazima Rais wetu aheshimiwe na kama kukosolewa basi akosolewe kwa lugha za staha, adabu, heshima na zinazokubalika katika jamii yoyote ile iliyostaarabika.

Lugha na maneno mabaya anayotumia Mdude Nyagali kwa Rais wetu hayakubaliki na hayawezi kukubalika mahali popote pale hapa Duniani.hakuna anayeweza kuyavumilia maana hiyo siyo demokrasia wala misingi ya demokrasia. Haiwezekani kwake demokrasia iwe ni kumtukana na kumdhalilisha Rais wetu.

Hivyo natoa Rai kwa watanzania wote kukemea vikali sana lugha chafu za Mdude Nyagali anazoendelea kuzitoa zidi ya Rais wetu. Shambulizi na mashambulizi ya aina yoyote ile kwa Rais wetu mpendwa ni shambulizi kwetu sote watanzania na wazalendo wa Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe ni msengerema sana mamayooh
 
Kwanza huyo Jamaa anatishia viongozi,Toka apate wafadhili wa Nje anaona Tanzania na watu wake ni Mali yake binafsi anaweza sema na kutenda lolote.
 
mkemee mwenyewe, mimi maisha magumu sifanyi kazi hiyo..hata akimpiga teke sawa tu 😎 . Kwani amezungumza hoja za uongo?mpeni majibu kama ana hoja. Alafu mtu akikosa adabu na malezi mazuri pia huwa anakuwa MWIZI, MUONGO...kwenye mali za umma anazopewa asimamie...kuwa makini..huu ni wizi mkubwa sana
 
Tujenge utamaduni wa kuheshimiana
Sativa alikuwa na kosa gani hata Rais Samia na wenzake huko CCM wampe mateso na ulemavu?

Huyo Rais wako anastahili heshima gani kwa matendo yake hayo?

Vipi kuhusu kuamuru polisi wawakamate na kuwatesa vijana wa CHADEMA waliokuwa wanakusanyana Mbeya kutumia uhuru wao kujadili mambo ya nchi yao?

Katika mazingira haya unataka mama yako huyu aheshimiwe? Unaweza vipi kumheshimu mtu ambaye yeye mwenyewe hajiheshimu wala kuheshimu taratibu na sheria na katiba?

By the way, hayo matusi ya Mdude Nyagali kwa Rais wako ni yepi kwa mfano? Maana umelalamika tu pasipo ku - justify malalamiko yako?

Chawa mkubwa Lucas Mwashambwa
 
ephen wanguu lazizi wangu karibu sana waridi wangu nakupenda mpaka nashindwa kuweka vituo katika kuandika
 
Usinifananishe na Mdude Nyagali.huko ni kunidhalilisha mimi.
Hudhalilishwi, unajidhalilisha mwenyewe kutetea ujinga na upumbavu toka kwa Rais wako na serikali yake iliyokosa mwelekeo badala ya kuukemea..

Mdude Nyagali amekemea kwa lugha kali. Bahati mbaya kwako ni kuwa umeona ni matusi kwa mama yako..!
 
Muwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais hata kama mlikosa malezi ya wazazi wenu.asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na Ulimwengu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nawaombeni Watanzania wenzangu na Wazalendo wa Taifa letu kujitokeza hadharani kulaani na kukemea vikali sana kauli Chafu za Mdude Nyagali kwa Rais wetu. Mtu huyu hatupaswi kumkalia kimya pasipo kutoa kauli na kumkemea pamoja na kumuonya vikali sana kuacha mara moja kutoa lugha chafu kwa Rais wetu.

Mtu huyu ambaye inaonyesha alikosa malezi mazuri utotoni mwake ameshajenga desturi na utamaduni wa hovyo na ambao haukubaliki hata kidogo.ambapo amekuwa akitoa lugha za udhalilishaji, kumshushia heshima Mheshimiwa Rais na Sasa amevuka mstari kuanza kutoa lugha za vitisho kwa Rais.

Inawezekana kwa akili yake na ulimbukeni wake,na kukosa kwake adabu na heshima akawa anafikiria labda anaongopwa au anaweza kufanya lolote lile au kutamka neno na maneno yoyote yale pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Anaweza kuwa anafikiria wote wana akili za aina yake za kuunga mkono ujinga wake.

Watanzania hatupo tayari kumvumilia wala kuona mtu akimtishia Rais Wetu au kumtukana, kumfedhehesha au kumtweza utu wake au kumshushia heshima bila sababu. Ni lazima Rais wetu aheshimiwe na kama kukosolewa basi akosolewe kwa lugha za staha, adabu, heshima na zinazokubalika katika jamii yoyote ile iliyostaarabika.

Lugha na maneno mabaya anayotumia Mdude Nyagali kwa Rais wetu hayakubaliki na hayawezi kukubalika mahali popote pale hapa Duniani.hakuna anayeweza kuyavumilia maana hiyo siyo demokrasia wala misingi ya demokrasia. Haiwezekani kwake demokrasia iwe ni kumtukana na kumdhalilisha Rais wetu.

Hivyo natoa Rai kwa watanzania wote kukemea vikali sana lugha chafu za Mdude Nyagali anazoendelea kuzitoa zidi ya Rais wetu. Shambulizi na mashambulizi ya aina yoyote ile kwa Rais wetu mpendwa ni shambulizi kwetu sote watanzania na wazalendo wa Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Jipambanue kama wewe si chawa ili tujue kama una moral authority ya kumsema Mdude.
Je wewe unaona yanayofanywa dhidi ya wapinzani ni sahihi? Mbona aliyechoma picha alishitakiwa, unadhani kama Mdude anatenda kosa serikali itashindwa kumshitaki? Kama wewe umemchukia usitushawishi watu wote tumchukie.
 
Back
Top Bottom