Watanzania Tujitokeze Kulaani na Kukemea Vikali kauli Chafu za Mdude Nyagali kwa Rais Wetu

Ndugu zangu Watanzania,

Nawaombeni Watanzania wenzangu na Wazalendo wa Taifa letu kujitokeza hadharani kulaani na kukemea vikali sana kauli Chafu za Mdude Nyagali kwa Rais wetu. Mtu huyu hatupaswi kumkalia kimya pasipo kutoa kauli na kumkemea pamoja na kumuonya vikali sana kuacha mara moja kutoa lugha chafu kwa Rais wetu.

Mtu huyu ambaye inaonyesha alikosa malezi mazuri utotoni mwake ameshajenga desturi na utamaduni wa hovyo na ambao haukubaliki hata kidogo.ambapo amekuwa akitoa lugha za udhalilishaji, kumshushia heshima Mheshimiwa Rais na Sasa amevuka mstari kuanza kutoa lugha za vitisho kwa Rais.

Inawezekana kwa akili yake na ulimbukeni wake,na kukosa kwake adabu na heshima akawa anafikiria labda anaongopwa au anaweza kufanya lolote lile au kutamka neno na maneno yoyote yale pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Anaweza kuwa anafikiria wote wana akili za aina yake za kuunga mkono ujinga wake.

Watanzania hatupo tayari kumvumilia wala kuona mtu akimtishia Rais Wetu au kumtukana, kumfedhehesha au kumtweza utu wake au kumshushia heshima bila sababu. Ni lazima Rais wetu aheshimiwe na kama kukosolewa basi akosolewe kwa lugha za staha, adabu, heshima na zinazokubalika katika jamii yoyote ile iliyostaarabika.

Lugha na maneno mabaya anayotumia Mdude Nyagali kwa Rais wetu hayakubaliki na hayawezi kukubalika mahali popote pale hapa Duniani.hakuna anayeweza kuyavumilia maana hiyo siyo demokrasia wala misingi ya demokrasia. Haiwezekani kwake demokrasia iwe ni kumtukana na kumdhalilisha Rais wetu.

Hivyo natoa Rai kwa watanzania wote kukemea vikali sana lugha chafu za Mdude Nyagali anazoendelea kuzitoa zidi ya Rais wetu. Shambulizi na mashambulizi ya aina yoyote ile kwa Rais wetu mpendwa ni shambulizi kwetu sote watanzania na wazalendo wa Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Watanzania au mazombie wa ccm? Yaani tutoke kutetea viongozi wanaoingia madarakani kwa wizi wa kura?
 
Unajua kabisa Rais na Msude ni kama bahari za sisimizi,haupo hapa kumtetea rais ,upo hapa kutafuta huruma ya rais
 
Chukuwachakomapema WAOGA SANA SANA!
Gen Z wanakuja kwa kasi. Hata mfanye nini reform is coming, even sooner than expected!
Imekwisha!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nawaombeni Watanzania wenzangu na Wazalendo wa Taifa letu kujitokeza hadharani kulaani na kukemea vikali sana kauli Chafu za Mdude Nyagali kwa Rais wetu. Mtu huyu hatupaswi kumkalia kimya pasipo kutoa kauli na kumkemea pamoja na kumuonya vikali sana kuacha mara moja kutoa lugha chafu kwa Rais wetu.

Mtu huyu ambaye inaonyesha alikosa malezi mazuri utotoni mwake ameshajenga desturi na utamaduni wa hovyo na ambao haukubaliki hata kidogo.ambapo amekuwa akitoa lugha za udhalilishaji, kumshushia heshima Mheshimiwa Rais na Sasa amevuka mstari kuanza kutoa lugha za vitisho kwa Rais.

Inawezekana kwa akili yake na ulimbukeni wake,na kukosa kwake adabu na heshima akawa anafikiria labda anaongopwa au anaweza kufanya lolote lile au kutamka neno na maneno yoyote yale pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Anaweza kuwa anafikiria wote wana akili za aina yake za kuunga mkono ujinga wake.

Watanzania hatupo tayari kumvumilia wala kuona mtu akimtishia Rais Wetu au kumtukana, kumfedhehesha au kumtweza utu wake au kumshushia heshima bila sababu. Ni lazima Rais wetu aheshimiwe na kama kukosolewa basi akosolewe kwa lugha za staha, adabu, heshima na zinazokubalika katika jamii yoyote ile iliyostaarabika.

Lugha na maneno mabaya anayotumia Mdude Nyagali kwa Rais wetu hayakubaliki na hayawezi kukubalika mahali popote pale hapa Duniani.hakuna anayeweza kuyavumilia maana hiyo siyo demokrasia wala misingi ya demokrasia. Haiwezekani kwake demokrasia iwe ni kumtukana na kumdhalilisha Rais wetu.

Hivyo natoa Rai kwa watanzania wote kukemea vikali sana lugha chafu za Mdude Nyagali anazoendelea kuzitoa zidi ya Rais wetu. Shambulizi na mashambulizi ya aina yoyote ile kwa Rais wetu mpendwa ni shambulizi kwetu sote watanzania na wazalendo wa Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Yaani nchi hii watu wawe wanashida kujadili kauli za vijana ambao sio hata viongozi wa upinzani wakati kuna wabakaji, mikataba mibaya, treni haina umeme, wananchi wanahamihswa, migogoro !!!
 
Back
Top Bottom