Watanzania tujiulize busara ya kugomea $450m ya MCC, kisha kukubali $300m toka kwa wezi.

Za juu juu tu. Vipi, nimeteleza wapi?
Hizo hizo za juujuu, nikupe 16 percent free shares, I mean FREE SHARES, then tugawane faida 50/50. With no capital injection from your side? Hii nadhani ni ya kwanza kutokea Duniani.

Nadhani tuendelee kushangilia tuu, mengine yatakaa sawa huko mbeleni.
 
Kwani hizi walizotupatia zinatosha kununua NOAH Moja kwa Kila Mtanzania???
 
Tusishangilie sana kwa sababu profit inapatikana baada ya kutoa:

* costs za mining,

* halafu wawalipe investors wote dividends zao (na ACACIA/BARRICK wana majority shares wakati TZ ina 16%)

* halafu kinachobaki ndicho kinachogawiwa 50-50 na serikali.

Sio kikubwa sana lakini ni hatua ya kujivunia.
 
Kuna post ukisoma unajua tu huyu mtu ufahamu wake ni mdogo. Anaweza kuwa na vyeti ila intelectual capacity yake ndoogo. Huyu anafananisha biashara ya madini na msaada. Just imagine !!
 
Mkuu hii ya 50/50 bado naona ni danganya toto,hivi shares 16% faida 50/50 labda kwenye other concentrates siamini hata kidogo
Yote hayo yamekuja kwa sababu ya ile pesa tunayowadai ni nyingi sana. Kama wangetulipa kiasi kile wangelikuwa wanamda mfupi sana wa kusavaiv, ndo maana wakakubali hivyo ("heli ya nusu shari kuliko shali kamili" wanaamini ACASIA)
 
jamani na upande Wa pili nao wamekiri kutoa hiyo hela isiwe mbwembwe tu kama za 37 t za kipindi kile mie accasia wakilipa naombeni Noah yangu
 
Mkuu vipi ulitegemea Serikali iburuzwe MIGA na ICSID?
 
Mkuu hii ya 50/50 bado naona ni danganya toto,hivi shares 16% faida 50/50 labda kwenye other concentrates siamini hata kidogo
Wenye upeo mdogo wa kufikiri wataamini,hii ni danganya toto asee,50/50 ni ndoto.
 
Yaani wewe katika vipengele vyote vile vya makubaliano umeona hiyo $300m tu? Halafu ukiitwa nyumbu au lofa unakasirika. Samahani kama nimetumia lugha isiyopendeza lakini.

Kokolo looote sababu ni shekeli

Mwenye akili ataanza na figure sio blabla
 
Hahahahhahahahah. Boss rule of the game hujaijua. Muda utahukumu
 
Mtaelewa tu..c ndo watawala wenu...me ngoja nitafute ugali wangu...

NOTE:: LAKIN AKIPATIKANA MTAWALA MZALENDO NA MUADILIFU. MSIACHE NITAARIFU NIMSAPORT....
 
Hii ndo main point huko kwengine kote umeandika pumba tuu,umeshasema pesa za masharti sisi tumekataa hayo masharti shida ipo wapi??Hizi pesa za ACACIA sio za msaada na wala sio za masharti ni haki yetu.
Wapi wameandika hizo pesa ni haki yenu? Acacia wametoa hizo pesa hili mfunge mdomo.
 
Hivi mkuu huwa unajiuliza kwa kina madhara ya misaada kutoka nchi fedha ya kimataifa?
 
Ccm ilishatufanya misukule hatujitambui kabisa.
 
Tujiulize nini sasa wakati huo ndio uwezo wetu wa kufikiri umefikia hapo. Tufanyeje kama Mungu hakutupa uwezo wa kufikiri zaidi ya hapo?
 
Uyu mtoa uzi atakuwa ni wale wa Peacock Hotel
 
Yes, Lissu was very right! Soma sheria ya madini uone ni madini gani ambayo mwelezaji anapaswa ku-declare kutoka kwenye concentrates.
Kamuulize Lissu kama he was very right mbona hawajatushtaki huko MIGA kama alivyosema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…