Watanzania tukitaka amani na nafuu ya demokrasia tujenge utamaduni wa kumchagua Rais kutoka pwani na Zanzibar, imeshathibitishwa mara tatu

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kio kwamba wakiingia kila kitu kinanyooka, la hasha!! Kuna Madudu huwa yanaendelea ila ukiweka mzani unaona wao wana nafuu hasa linapokuja suala la aman, demokrasia na maendeleo.

Mwinyi mzee wa ruksa alitutoa kwenye ujamaa wa Nyerere watu wakaanza kumiliki hata Tv (wakati huo Zanzibar washazizoea), Pia ni Mwinyi ndie alie assist kuwe na mfumo wa vyama vingi kwa mara ya kwanza nchi hii, kiuchumi nako watu walizikimata pesa aisee.

Kikwete aliweka historia ya democracy tangu tupate uhuru ndio kipindi ambacho demokrasia ya uhuru wa maoni na ushindani wa vyama vya siasa ilikuwa kubwa. Eote ni mashahidi hata kwenye suala la Katiba mpya Kikwete aliweza angalau kuruhusu kuwe na makongamano, kiuchumi vijana wengi walilamba ajira si ualimu si jeshini, pesa mtaani ilikuwepo.

Kaja Mama Samia nae tunaona nchi imerudi kwenye amani, tunaona jinsi mambo yanavyoanza kujirudi, Wapinzani wengi waliobambikiwa kesi wanaachiwa huru kwa spidi, mikutano ya hadhara pia iliyofungiwa kaanza kuifungulia, ni huyu huyu mama licha ya kuwa CCM aliweza kuweka siasa pembeni na kuwa na utu wa kwenda kumjulia hali Tundu Lissu aliefanyiwa unyama wa kutisha mno, kiuchumi nako pesa imeanza kuzunguka mitaani, zile hofu za task force zimepungua.
 
Hakuna kitu kama hicho. Ni ujinga kuwaza ukabila. Wapewe ata wachaga tupime. Maana mnawananga kila kukicha ila nina hakika wataiweza nchi na maendeleo tutayapata, tatizo hatujiamini watu wa pwani, hatupendi challenge na change tumezoea kubebana na 'sama leko' zetu.
 
Hatuangalii kabila, tunaangalia sifa za viongozi muhimu ambazo zinaleta amani na unafuu wa kidemokrasia.

1. Utu

2.kuweza kujichanganya na wananchi

3.ustaarabu
 
Hatuangalii kabila, tunaangalia sifa za viongozi muhimu ambazo zinaleta amani na unafuu wa kidemokrasia.

1. Utu

2.kuweza kujichanganya na wananchi

3.ustaarabu
Maendeleo umesahau
 
kwanini msijitenge ili mpate hao maraisi milele na milele mwisho muwe kama Iraq, Iran na ndg zenu
 
Kibaraka katika Ubora wako
 
Wew sio wa Pwani kaangalie viongozi wa kichaga walipopewa madaraka walianza kupeleka kila kitu kwao..Hawawezi kushika madaraka ng'o.
 
Waisiharamu siyo wazalendo ni mafii ya bata
 
Wanauza sana wanyama wetu maana kwao hawana.
Ndio maana nimeshasema sio kwamba wakiingia kila kitu kinanyooka, la hasha!! Madudu yataendelea tu ila ukiweka mzani unaona hao wana nafuu
 
Ndio maana nimeshasema sio kwamba wakiingia kila kitu kinanyooka, la hasha!! Madudu yataendelea tu ila ukiweka mzani unaona hao wana nafuu
Hakuna nafuu yeyote wanatuletea hasara tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…