Watanzania tumekosa mtetezi kwenye suala la umeme, sasa tunaangamia

Kwenye maandamano ulikuwepo ?
 
...ukinunua sola, au ukafunga motor mbili zinazotegemeana, utapata infinity electric charge(umeme usio na kikomo). Utasahau mambo ya TANESCO, nakwambia watakusanya nguzo wauze mbao
Ni kweli usemalo mkuu lkn je ni Watanzania wangapi wenye uwezo wa kununua hizo solar?? Hao wauzaji wa solar nao wamepandisha bei karibia mara Tano ya bei ya awali baada ya kuona Kuna shida ya umeme.. bei ya jenireta kwa sasa ndo usiseme.

Kweli Watanzania tunateseka kwenye nchi yetu aisee, kumbe zile takwimu za kuzidiwa furaha na somalia ni kweli bana..
 
Usiseme nchi yetu. Sema nchi yao ( wanasiasa) wanaotengeneza haya matatizo.
 
Nakubaliana kwa uchache na mawazo Yako. Lkn point yangu kubwa ni kwamba kitendo Cha serikali kukosa ukosoaji wa maana hasa kwenye vyombo vya maamuzi wanajisahau!!!! Hata kama wapinzani Wana maslahi Yao mengine lkn mm naamini wangelikua bungeni na sehemu nyingine za maamuzi lazima wangelipigia kelele sana swala hili. Huu mgao hata kipindi cha kikwete haukua hivi bana
 
Hivi tuliambiwa kikomo cha shida ya umeme ni lini vile, naomba nikumbushwe.
Tulidanganywa miezi 6 lkn sasa mwaka unaenda kukatika na hakuna uelekeo wowote ni lini mgao utaisha. Wanafanya kutugeuzia maneno tu.

Kipindi cha kiangazi wakesema shida ni mvua nyanzo vimekauka ndio maana umeme hakuna, mungu si athumani kashusha mvua ya kutosha maji Kila mahali he!! Wakageuka Tena oohh! Mvua zimezidi ndio maana hakuna umeme!! Mungu akasema sio kesi ngoja nipunguze mvua Bado umeme hakuna. Kwa style hii furaha utaitoa wapi wewe mtanzania mwenzangu??
 
Waruhusu uraia pacha uone suala la umeme kama halitakua historia
 
Pengine kuna mikataba na wauza soral sasa ili wauze serikali isitoe umeme.maana unaambiwa mtambi umewashwa harafu keshi umeme bado haupo.
Watanzania tugomee kulipa Kodi! Unakuja kunidai Kodi Mimi kinyozi wa saloon hiyo pesa ya kukulipeni naitolea wapi????
 
Nakwambia ni balaa watu wanamapele ya joto kama wamemwagiwa upupu!! Joto Kali na hakuna umeme wa kuwasha hata ki feni.
 
Gharama zote za nini hizo?
Unajua nimekuja kugundua shida ya umeme/ ukosefu wa umeme tusilaumu shirika la Tanesco, shida iko kwa viongozi wetu wa kisiasa hasa kiongozi mkuu. Ukituliza kichwa vzr utanielewa. Mimi nahisi Tanesco wanafanya kazi kwa maelekezo ya mtu au watu flani. Watanzania tujiulize kwa Nini shida ya umeme inakuepo au kutokuepo kutegemea na kiongozi anaengoza nchi???

Kwa Nini kipindi cha magu hakukua na mgao then now mgao ni wakutisha ilihali shirika ni lile lile???

Mzee magu alifanya Nini kuhakikisha Kuna kuwa na umeme wa uhakika ambacho huyu mama hawezi kukifanya?? Tujiulize kwa pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…