Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Ugaidi ndio kosa kubwa kuliko yote duniani na sio Tanzania tu.kujibu swali lako Mimi naona ni heri mwakitalu akaifuta hii kesi bila mashart yoyote, ili kumaliza Hilo suala kistaarabu.tukisema aombe msamaha nikutaka kukuza mambo watu wataanza kuhoji.
1. Amekosa nini na kamkosea Nani ?
2. Je unaweza kumu achia gaidi kwa kuomba msamaha?
Pia tukisema kesi iendelee ,inaweza kuacha madoa makubwa miongoni mwa mihimili yetu miwili Yani serikali na mahakama.mbowe akipatikana Hana hatia Hilo litajenga taswira mbaya sana kwa serikali yetu kuwa inaonea watu ,na akifungwa kwa vyovyote vile itaitikisa mahakama yetu kutokana na ugumu uliopo kumthibitisha ugaidi kisheria.maana tayari Kuna mino'ngono mitaani, kuhusu usafi na uadilifu wa mahakama yetu hasa baada ya kauli alizotoa jaji mkuu hivi karibuni ju ya watu wanao kosoa kazi za majaji.watu wameenda mbali zaidi wakihoji kwanini jaji mkuu awe na kinga yakutoshtakiwa ilihali yeye ndio msimamizi mkuu wa kutoa na kusimamia haki za watu?

Mwisho namshukuru Rais wetu Mama Samia kwa kutoka kauli yake yakusamehana sisi ni binadamu, namuomba mama yetu amuagize DPP aifutilie mbali hiyo kesi ilikulinda historia yake rais wetu pamoja na umoja wetu kama taifa. Ni heri kufanya yanayompendeza Mungu kuliko kufanya yanayompendeza mwanadamu.
 
Ila wewe jamaa kwa kweli unazeeka vibaya.
Nakumbuka miaka ya 2013/2014 nilikuwa nasoma mabandiko yako. Aisee ulikuwa JINIAZ
Ila sasa hivi nadiriki kusema umekuwa SHETANI
 
Mahakama ifanye kazi yake mpaka mwisho,kama jamaa hana kosa itajulikana na kama anakosa itajulikana tena.
 

Kama mikutano ya kukusanyika ambayo ipo kikatiba imekatazwa ulitaka wakasemee wapi?
 
Watanzania wengi walikuwa wanakitazama CHADEMA kama chama mbadala kinachoweza kupambana na CCM lakini CDM kushirikiana na wanaharakati kupandikiza CHUKI na kugawa watanzania kimepoteza ushawishi. Wananchi wanataka mabadiliko sio visasi na Chuki.
Wenye visasi na chuki ni hao wanaowaweka watu ndani kutimiza kiu yake.
 
Wewe unaishi dunia gani, hujui kuwa mikutano ya vyama vya siasa imepigwa marufuku na ni CCM tu ndiyo wanaruhusiwa kufanya mikutano.

Kama hutaki mikutano ya Space na Club House, uliwakaribisha sebuleni kwako na walikataa?
 
Had sasa kwa mwenendo wa kesi ilivyo mahakama imeisha jifua kwa kuonesha udhaifu wake
 
Nikuulize ndugu.. Hivi Kwann imebid wafanyie siasa mitandaon na sio kufanya mikutano yao kama katiba inavyosema??
 
Watanzania wengi walikuwa wanakitazama CHADEMA kama chama mbadala kinachoweza kupambana na CCM lakini CDM kushirikiana na wanaharakati kupandikiza CHUKI na kugawa watanzania kimepoteza ushawishi. Wananchi wanataka mabadiliko sio visasi na Chuki.
CWPedro mwanalumba huwezi kuwa mshauri mzuri wa Chadema.
 
Chadema ya Dr Slaa ilikuwa ya enzi za JK mikutano ikuruhusiwa na vyombo vya habari havikuwa kampuni za PR za serikali.
 
Onghwise nghwana Mayalla . Hakuna kitu kibaya kama kumuundia mtu kisa, ili kumlazimisha kusifu na kuabudu.

Ccm na viongozi wake waondokane na dhana ya chamadola. Imewakaa akilini kiasi cha kuwaona waTz wenye mtazamo tofauti na wao kama wahalifu. Wakiweza kuwaona watu wengine kama nao wanastahili , hiki kiburi cha umungumutu wa kutaka waombwe misamaha kwa michongo walioiunda wao, haitakuepo.
 
mikutano ya ndani ama ya nje ambayo wangeongea hayo unayo yaita uharakati mmeawafungia.
magazeti ama redio zitazo rusha agenda zao mnaziadhibu ama kuzifungia..
cdm vs ccm ilitakuwa kwny uwanja huru, lakn mmoja anabebwa na vyombo..

badala ya kuelekeza mtutu.wa chombo chenye brain kushindana kiuchumi na kenya, chombo kulinda rasilimali za nchi, kinafukuzana na wapinzani ama kupandikiza mamluki upinzani..

kipindi cha slaa, contacts ndani ya chombo inamwaga data kwa upinzani, na upinzani unaweka hadharani ama bungeni ama kwny mikutano ama kwny magazeti kulikokuwa huru kuongea..
mliwashulikia contacts, mnasheria ya kuzibiti hotuba za upinzani bungeni kabla hazijasomwa, mkaondoa live bunge, na kudhibiti media..

upinzani walikuwa na ni wabwekaji kwa individuals ambao ni mchwa, ni wazi kuna compromise kati ya mchwa na vyombo kwny kula keki, ndio maana hao individual ndani ya ccm na serikali wanalindwa, maana mchwa ni highly rankings.
 

definition ya gaidi ama ugaidi wazungu ndiyo wametufundisha. kwamba ili mtu awe gaidi ni lazma awe na sifa kadhaa pengine ikiwapo awe na ukaribu na makundi fulani ya kigaidi.
wakatrain watu wetu na wakutagawia facilities ikiwemo kushea intel na wao..

cha ajabu waliotufundisha, na wanaoujua huyu ni gaidi ama laa, wapo upande wa huyo gaidi na kusema aachiwe huru siyo gaidi..
hapa panae shida, ama mfundishwa hajaelewa somo la gaidi, au mfundisha kasahau alicho kifundisha.

kuomba msamaha ni admission kuwa ulikosea, hivyo kwa mbowe kuomba msamaha maana yake amekiri kosa, kwamba alikuwa gaidi.

isitoshe, kila msamaha una masharti yake..
rugemalulila alikomaa, hakukiri kosa, leo hii yupo kwny mipango ya kutonyoosha kama serikali kwny mahakama, si unajua wahaya na wapare vile wanapenda kesi..

kesi ina ichafua serikali, inachafua utalii wa nchi, inaifanya dunia ione kuwa ccm haiwezi kushindana kwa hoja, tunaanza kufananishwa na kagame, museveni nk ambao husigina wapinzani wao wa kisiasa.
 
Uzi Maridhawa ila hapa natazama kwa pande tofauti
1.Mbowe ni mtuhumiwa wa ugaidi! Sheria ya ugaidi aina mahali inasema huyu anatakiwa kupewa dhamana! Anatakiwa kukaa sehemu yenye ulinzi 24/7!
2. Kusamehe ni kuendeleza udhalimu nibora aendelee na kesi kutokana na ushahidi na vielelezo vya mahakamani Serikali imeelewa utengenezaji wa kesi kubwa kama hii kwa mtu maarudu inatakiwa kuwa umejipapanga siyo chini ya miaka 3 unakuwa na masterplan siyo unapokea maagizo unatengeneza scenario mbele utaaibika kwani sheria inakata kote kote!.
3. Labda kinachoweza kufanyika kwa sasa ni kukubali serikali ipate aibu pale DPP Atakaposema kutokana na mamlaka niliyopewa Serikali imeamua kutoendelea na hii kesi kutokana na serikali kutokuwa na vielelezo vyakutosha vya kumtia hatiani Mbowe pamoja na ushahidi uliotolewa bado autoshi kumfungulia Mbowe mashitaka ya ugaidi.

Hilo kwangu naona linaweza kuwa na mshiko kuliko hii ya sasa!
 
Umemsikia Salumu Mwalimu? Kasema anamaliza kufanya ziara yake nchi nzima hamna hata polisi aliyemuuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…