Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Makala zako hazina maana yoyote.

Kwa lipi lililokugusa kwamba wamesamehe?

Kama wafungwa hawajasamehewa sikukuu ya uhuru sembuse porojo za kisiasa wakitafuta uungwaji mkono.

Amewaumiza wengi kwa vitendo vyake vinavyochochewa na ninyi wapiga debe maslahi
 
Kabla hatujapeana Hongera tupeane pole kwa maisha yetu (kusamehewa au kuhukumiwa) kuwepo mikononi mwa mtu na sio taasisi au sheria
 
Umemsikia Salumu Mwalimu? Kasema anamaliza kufanya ziara yake nchi nzima hamna hata polisi aliyemuuliza.
CWPedro ziara ni sehemu ndogo sana ya uwanja wa vyama vya siasa kufanya kazi zake.
 
Kama ina ushahidi, bado mahakama sijasema kweli Mbowe ni gaidi kwani kesi haijafikia hata hatua ya kusema kama watuhumiwa wana kesi ya kujibu au la. Ni wao tu anasema vitu ambavyo wanataka ila havina ushahidi, kama ile kauli kuwa wapo waliohukumiwa kwa kesi hiyo na wako jela, aliyepo ni kwavile alitoroka nchi.
Hapo kinachotakiwa ni kumwachia bila kuona aibu na si kumsamehe.
Inasikitisha kuwa umeacha wakati wa JPM kuhusu kusamehe ilhali aliwaachia hata babu Seya na wanawe. Naye JPM kuna aliowasamehe, hata lina Nape na wenzake waliokuwa wakimteta na kumsema vibaya. Kuacha kutambua hayo ya JPM ni husuda tu labda kwavile ulikuwa bungeni kujieleza wakati wa enzi yake.
Mwisho, kumbuka hii no mwendelezo wa awamu ya TANO si awamu ya sita, kama anavyosisitiza mwalimu Polepole darasani kwake.
 
Kuna wimbo wa Ambassadors of Christ wanasema "Dunia umebadilika, aliyekosewa hubadilishwa mwenye makosa". Aliyekosewa kwa kuharibiwa mashamba yake, kuvunjiwa Billicanas yake, kuvunjwa mguu, kufungiwa accounts zake, kudhulumiwa uchaguzi wa ubunge, kubambikwa kesi kubwa....halafu huyo ndo aombe radhi! ALIYEKOSEWA HUBADILISHWA MWENYE MAKOSA(Ambassadors of Christ).
 
Ukizuia mikutano ya hadhara, mbinu zingine zinaibuliwa. Hata hiyo Space nayo ikazimiwa internet, ikaibuliwa VPN. Kuhangaika kwa serikali kutazidi kuibua mbinu hadi ukombozi kamili.
 
"Mbogamboga wanaruka na kupoteana"
Alisikika jamaa mmoja anaitwa Pep

Freeman Mbowe aombwe msamaha

1. Mbowe, mashamba yake yaliwahi kuteketezwa kwa uonevu.

2. Mbowe, club yake ya Bilcanas iliwahi kunyang'anywa kwa uonevu.

3. Mbowe amewahi kuwekwa mahabusu mara nyingi kwa uonevu.

4. Mbowe amewahi kuhukumiwa kulipa mamilioni ya pesa kwa uonevu.

5. Mbowe amewahi kubambikiziwa kesi zisizo na vichwa mala miguu kwa nia tu ya kumkomoa.

6. Mbowe akaunti zake za benki ziliwahi kufungiwa kwa uonevu.

7. Mbowe, hoteli yake ya familia imewahi kubambikiziwa kodi zinazozidi mapato maradufu.

Haya maoni yaliyojaa busara nyingi yametolewa na one of the most respected JF-Expert Members, Bams
 
Watanzania wengi walikuwa wanakitazama CHADEMA kama chama mbadala kinachoweza kupambana na CCM lakini CDM kushirikiana na wanaharakati kupandikiza CHUKI na kugawa watanzania kimepoteza ushawishi. Wananchi wanataka mabadiliko sio visasi na Chuki.
Kwa mara ya kwanza umekiri kwa kinywa chako kama CHADEMA ni chama kinachotazamwa na watanzania wengi kama chama mbadala, HONGERA KWA KUJITAMBUA.
Siku utayojitambua rasmi ni siku utayokubali kwa kinywa chako pia kuwa CHADEMA hawajawahi endekeza visasi na chuki bali wamekuwa wakihubiri amani miaka yote.
CHUKI ZINAPANDIKIZWA NA KULAZIMISHWA NA CCM.
 
Aombwe msamaha na kijani kibichi wamlipe fidia.


Alisikika kijana Pep anayewadis sana wale wa shati za mbogamboga
 
Kwani vile vyeo bado vipo au vilienda nae?
 
Ukifuatilia mwenendo wa kesi ya Mbowe,namna ushahidi unavyotolewa,namna utetezi wanavyowasilisha hoja zao,na namna upande wa mashitaka wanavyotumia nguvu nyingi kuhalalisha hoja zao,lazima upate mashaka juu ya hili jambo la Mbowe.Wanaohusika watakuwa wamepata somo namna bora ya kushughulika na mambo kama haya yanayovuta hisia za watu wengi.Siasa ni Imani na siku zote kucheza na imani za watu, ni Sawa na kuiingiza nchi katika majaribu yasiyo ya lazima kabisa.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…